Bado kuna tumaini dogo kwa Italia au Chile kufuzu kwa fainali zijazo za Kombe la Dunia nchini Russia, yote ni kwa sababu ya muswada uliopelekwa katika Bunge la Peru utakaofanya Shirikisho la Soka la nchi hiyo kujiaonda moja kwa moja Fifa.
Chile ‘La Roja’ ilipoteza nafasi hiyo baada ya kufungwa 3-0 na Brazil katika siku ya mwisho na timu hiyo kumaliza nafasi ya sita, Wakati Italia wenyewe walifungwa bao 1-0 na Sweden katika mchezo wa mtoano na kuaga mashindano hayo.
Tofauti na Peru iliyofanikiwa kufuzu kwa fainali za mwakani baada ya kushinda 2-0 dhidi ya New Zealand.
Hata hivyo, Peru ‘Libero’ sasa wanaweza kupoteza nafasi hiyo, endapo serikali itaingilia masuala ya soka jambo litakalofanya Peru kupoteza tiketi yake ya kucheza Kombe la Dunia.
Mazingira hayo yanafungua mlango kwa timu za Italia au Chile kupata nafasi ya kufuzu kwa fainali za mwakani

No comments:
Post a Comment