Saturday 27 January 2018

Alichokisema Mr T kuhusu Darassa kuwa teja



Baada ya kimya cha muda mrefu kwa msanii Darassa ambaye mwaka juzi 2016 alitingisha sana na wimbo wake 'Muziki' kumeibuka tetesi kuwa msanii huyo naye amejiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya, jambo ambalo limewashtua wengi. 

Kufuatia tetesi hizo mtangazaji wa kipindi cha Bongo fleva Top 20 ya East Africa Radio, Jr Junior alimvutia waya msanii huyo lakini bahati mbaya hakuweza kupokea simu yake jambo ambalo lilimfanya kumpigia simu mtu wake wa karibu ambaye ni producer wake Mr T Touchez ili kufahamu ukweli juu ya tuhuma au tetesi hizo. 

Baada ya Mr T Touchez kupigiwa simu alisema yeye hafahamu lolote juu ya jambo hilo na kukiri kuwa kwa sasa hajakutana na msanii huyo muda kidogo, hivyo hafahamu lolote kuhusu hicho kinachoelezwa kutumia dawa za kulevya. 


Kikosi cha Yanga VS Azam FC

                                            Kikosi cha Yanga kitakachovaana na Azam FC leo

Kabila ataja mwezi wa kufanyika uchaguzi DR Congo

Rais Joseph Kabila amepinga ukosoaji unaotekelezwa na jamii ya kimataifa kuhusu kucheleweshwa kwa uchaguzi katika jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika mkutano na wanahabari kuadhimisha miaka 17 madarakani, aliahidi kwamba uchaguzi huo utafanyika mwisho wa mwaka huu.

Kulingana na mwandishi wa BBC Alex Duval Smith mkutano huo na vyombo vya habari mjini Kinshasa ulikuwa wa kwanza katika kipindi cha miaka mitano.Na ulichukua saa tatu.

Aliikosoa Monusco akisema ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa hauko nchini DRC ili kuendesha shughuli za taifa hilo.

Katika shutuma dhidi ya muungano wa Ulaya na Marekani, ambao wamekosoa makabiliano dhidi ya waandamanaji, alisema: DRC sio koloni .Taifa hili lazima liheshimiwe.

Alionekana akilikumbusha kanisa katoliki akisema kuwa maandamano yanayofanywa na wakristo dhidi ya serikali yake yanafaa kuruhusiwa lakini waandalizi ni lazima washtakiwe.

Serikali hiyo hivi majuzi ilitangaza kwamba uchaguzi utafanyika tarehe 23 Disemba, ikiwa ni miaka miwili baada ya kukamilika kwa muda wa utawala wa rais huyo.

Kampuni ya Mugabe yaingia kwenye matatizo

Kampuni moja ya rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe inatakiwa kuondoka katika kipade kimoja cha ardhi kinachomilikiwa na shule moja la sivyo ishtakiwe.

Kampuni hiyo kwa Jina Gushungu Holdings inadaiwa kunyakuwa kipande hicho cha ardhi chenye ukubwa wa hekari 23 katika eneo moja la makaazi ya mji wa Harare.

Kanisa la Reform linasema kuwa ardhi hiyo inamilikiwa na kundi la shule zake la Eaglesvale.

Wakili wa shule hiyo Rodney Makausi aliambia BBC kwamba mwaka 2016 serikali ilichukua ardhi hiyo kwa nguvu.

Serikali baadaye ikaondoa madai yake baada ya swala hilo kuwasilishwa mahakamani.

Lakini mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Enos Chomutiri anasema kuwa mahindi yalipandwa katika shamba hilo mwaka uliopita na bango kubwa la shule hiyo likaondolewa.

Mawakili wametaka kampuni hiyo kuondoka katika shamba hilo mwisho wa mwezi huu ama ishtakiwe.

Sio mara ya kwanza familia ya Mugabe imetuhumiwa kuchukua mali kwa nguvu.

Awali, familia hiyo imekuwa na mgogoro na wakulima masikini kuhusu ardhi moja inayodaiwa kuwa na utajiri wa dhahabu ,pia familia hiyo imetuhumiwa kwa kunyakua shamba moja linalalozalisha ndimu zinazouzwa nje ya taifa katika eneo hilo hilo.

Bodi ya Ligi yaipiga rungu Mbeya City

Timu ya Mbeya City

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania kupitia Mkurugenzi wa Ligi Boniface Wambura imetangaza kuipiga faini ya jumla ya shilingi milioni moja klabu ya Mbeya City kwa makosa mawili tofauti.

Wambura amebainisha hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam na kusema timu hiyo ilitenda kosa la kutumia mlango usio rasmi kuingilia uwanjani katika mechi iliyofanyika Januari 1,2018 Jijini Mbeya ambapo kitendo hicho ni kosa kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu na kutozwa laki 5 kama adhabu yao.

Aidha, Wambura alisema Kamati iliiagiza Sekretarieti ya Bodi ya Ligi kutoa waraka kwa wamiliki wa viwanja kuhakikisha timu zote zinaingia uwanjani kwa kutumia milango rasmi nasio vinginevyo.

Mbali na hilo, Wambura amesema Klabu hiyo pia imepigwa faini ya laki 5 kutokana na mashabiki wake kuingia uwanjani na kumzonga mwamuzi kwa madai alikataa kutoa 'penalti' kwa timu hiyo.

Kwa upande mwingine, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania kupitia Mkurugenzi wa Ligi Boniface Wambura imetangaza kumfungia kocha wa timu hiyo Ramadhani Mwazurimo mechi mbili na kupigwa faini ya laki 5 kutokana na kutoa lugha ya kashfa katika mechi ya Tanzania Prisons dhidi ya Mbeya City iliyochezwa Januari 14, 2018 kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Lowassa amnadi Salum Mwalimu Kinondoni

Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu wa Chama cha Demokrasia na  Maendeleo CHADEMA, Edward Lowassa jioni leo amemnadi Mgombea wa Ubunge wa Kinondoni kupitia chama hicho, Salumu Mwalimu huku akiwataka wakazi wa Kinondoni kuacha kumuongelea mgombea wa CCM, Maulid Mtulia maana amekuwa msaliti kwao.

Lowassa alitumia wakati huo pia kuwashukuru wananchi wa Kinondoni kwa kumpigia kura wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, na kuwaomba zile kura walizompigia 2015 basi wazielekeze kwa Mwalimu ambaye anaamini ni msomi mwenye kuweza kuwatetea wakazi wa Kinondoni.

" Msiogope vijana wa Kinondoni wenzetu wamekuwa wajanja wakilinda kura zao sasa na sisi kama ambavyo wazungumzaji wengine wamesema basi tunaomba mlinde kura zetu ikiwezekana tulale katika vituo vya kupigia kura kuhakikisha hatuibiwi.

Nae Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya tatu, Fredrick Sumaye alisem, " Hakikisheni mnamchagua Mwalimu huyu ndie mtu safi wa kuhakikisha analeta maendeleo katika jimbo lenu,"

Kwa upande wake Mwalimu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, alisema " Achaneni na wao wanaosema mimi sio mkazi wa hapa nachoomba ni kura zenu ambazo zitanifanya nikawatetee kuwajengea shule, kuhakikisha ajira kwa vijana,"

Kampeni za chama hicho zitaendelea kesho katika eneo la Kigogo jijiji Dar es Salaam ambapo zitaongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe.

Taliban watumia 'ambulance' iliojaa vilipuzi kuwaua watu 95 Afghanistan

Mlipuaji wa kujitolea mhanga amewaua takriban watu 95 na kuwajeruhi wengine 158 katika mji mkuu wa wa Afghanistan Kabul, kulingana na maafisa.

Washambuliaji waliendesha ambyulensi iliokuwa imejaa vilipuzi kupitia kizuiazi cha polisi hadi katika barabara ambayo ilikuwa imetengewa wafanyikazi wa serikali.

Kisa hicho kilitokea katika jumba la wizara ya maswala ya ndani na afisi ya Muungano wa Ulaya na baraza kuu la amani.

Kundi la wapiganaji wa Taliban linasema kuwa walitekeleza shambulio hilo ambalo ni baya zaidi katika kipindi cha mwezi mmoja.

Walioshuhudia wanasema eneo hilo ambalo lina majumba ya balozi nyingi pamoja na makao makuu ya polisi mjini humo, lilikuwa na watu wengi wakati bomu hilo lilipolipuka siku ya Jumamosi .

Maafisa wanasema kuwa idadi ya waliofariki inaendelea kuongezeka huku majeruhi wakipelekwa hospitalini kwa matibabu.
Shirika la kimataifa la msalaba mwekundi limesema kuwa utumizi wa 'ambulence' unakera.Wiki moja iliopita ,wapiganaji wa Taliban waliwaua watu 22 katika hoteli moja ya kifarahari mjini Kabul.

Hili ndilo shambulizi baya zaidi kuwahi kufanyika mjini Kabul katika kipindi cha miezi kadhaa.

Mnamo mwezi Oktoba, watu 176 waliuawa katika shambulio la bomu mjini Afghanistan katika kipindi cha wiki moja.

Vikosi vya maafisa wa usalama vya Afghanistan vimeshambiliwa pakubwa na wapiganaji wa Taliban ambao wanataka kuweka sheria ya kiislamu katika taifa hilo.

Mnamo mwezi Mei, takriban watu 150 waliuawa na mpiganaji wa kujitolea mhanga mjini Kabul.

Kundi la wapiganaji wa Taliban walikana kutekeleza shambulio hilo lakini serikali ya Afghanistan inasema kuwa kundi la Haqqani ambalo ni mshirika wake lilitekeleza shambulio hilo kupitia usaidizi wa Pakistan.

Pakistan imekana kusaidia kundi lolote la wapiganaji linalotekeleza mashambulizi nchini Afghanistan .

Mwezi huu, Marekani ilikatiza usaidizi wake wa usalama kwa Pakistan, ikisema kuwa taifa hilo limeshindwa kuchukua hatua dhidi ya makunni ya kigaidi katika ardhi yake.


Matapeli wa Viwanja DSM kukiona

Serikali ya Mkoa wa Dsm Imetangaza rasmi vita dhidi ya Matapeli wa Viwanja na Nyumba ambao wamekuwa wakitumia mbinu mbali mbali ikiwemo ofisi za mawakili ,mahakama pamoja na Madalali kuwadhulumu wajane pamoja na watu wasiokuwa na Uwezo.

Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul makonda akizungumza na waandishi wa habari baada ya kwenda kwa familia ya Bi,Stella Bejumula pamoja Mume wake ambao ni watumishi wastaafu wa serikali ambao wametapeliwa nyumba kwa zaidi ya Miaka sita na kuishi maisha ya Kutangatanga na kutegemea Misaada ikiwemo chakula kutoka kwa watu mbali mbali..

Aidha Familia hiyo ya Bejumula ilitoa mtiririko mzima wa kadhia ya Kutapeliwa ambapo mwaka 2012 walikopa bank ya Crdb Mkopo na kufanikiwa kurejesha zaidi ya asilimia 80,na kubaki million ishirini ambayo alitokea Mtu mmoja kuwakopesha kwa riba lakini baadae akadaiwa kutengeneza Mkataba bandia wa mauzo kuwa familia hiyo imemuuzia kwa milion 96 Huku nyumba hiyo ikiuzwa kwa mtu mwingine katika kipindi cha siku 4 tu baada ya deni kulipwa.

Aidha Makonda alikwenda katika nyumba iliyopo kitalu B namba 91 ambayo ilikuwa ikimilikiwa na mzee na Bi,Bejumula na kutoa agizo la mmiliki aliyeuziwa eneo hilo kufika ktika ofisi za Mkuu wa Mkoa na nyaraka alizofanikisha kununua eneo hilo.

Makonda pia aliwakabidhi wazee hao wastaafu vyakula mbali mbali ikiwemo,Mchele,mafuta,unga, ngano na sukali huku akimtaka mfadhili anayewasaidia malazi aendelee kuwasaidia wakati akishughulikia suala hilo hali iliyozua simanzi eneo hilo …

Yanga SC yavunja rekodi ya Azam FC Chamazi

Mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara baina ya mabingwa watetezi klabu ya Yanga dhidi ya Azam FC umemalizika katika uwanja wa Azam Complex Chamazi kwa mabingwa hao kushinda jumla ya mabao 2-0.

Kwa ushindi wa Yanga SC unaifanya timu hiyo kuvunja rekodi ya wana lamba lamba Azam FC ya kutokupoteza hata mchezo mmoja toka kuanza kwa ligi kuu soka Tanzania Bara msimu huu wa mwaka 2017/18.

Wafungaji katika mchezo alikuwa Shabani Chilunda wa Azam FC wakati kwa upande wa Yanga SC akiwa Obrey Chirwa na Gadiel Michael.

Kwa matokeo hayo inaifanya mabingwa watetezi Yanga SC kufikisha jumla ya pointi 28 wakiwa nafasi ya tatu, Azam FC ikisalia na alama zake 30 nafasi ya pili huku Simba SC ikiongo katika msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 32 na mchezo mmoja mkononi ambao unatarajiwa kupigwa hapo kesho siku ya Jumapili.

Katika michezo mingine iliyopigwa hii leo timu ya Mbeya City ikiwa nyumbani imekubali kutoka sare ya mabao 0 – 0 dhidi ya Mtibwa Sugar wakati Mwadui FC ikiwa nyumbani imelizimishwa sare ya magoli 2 – 2 na Njombe Mji wakati Kagera Sugar ikitoka suluhu ya bila kufungana dhidi ya Lipuli FC.

Mtulia kuweka hadharani mikakati yake Kinondoni

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CCM Wilaya wa Kinondoni, Harold Maruma amesema mgombea ubunge wa Kinondoni kwa tiketi ya chama hicho, Maulid Mtulia atatumia uzinduzi wa kampeni kueleza mikakati yake ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

CCM inazindua kampeni leo Jumamosi Januari 27,2018 kuanzia saa 10:00 jioni katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.

Maruma amesema baadhi ya changamoto zitakazozungumzwa na mgombea huyo ni barabara na mikopo kwa akina mama.

"Tunaomba wakazi wa Kinondoni kujitokeza  kwa wingi na Jeshi la Polisi limetuhakikishia kuwa hakuna mtu atakayedhurika wakati wa kampeni na wakati wa kurudi nyumbani," amesema.

Wengine wanaoshiriki uzinduzi wa kampeni hizo ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba na wabunge wake wa mkoa wa Dar es Salaam.

Tayari viongozi wakuu wa chama hicho tawala waliofika katika uwanja wa Biafra wametambulishwa na kuipisha bendi ya bendi ya TOT inayotoa burudani ya nyimbo za  kuhamasisha wana CCM.

Watu 30 Wapoteza Maisha Katika ajali ya moto Korea Kusini

Imethibitika zaidi ya watu 30 wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya moto uliotokea katika Hospitali moja nchini Korea Kusini.

Hata hivyo maafisa wa nchi hiyo wanasema idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka kutokana na baadhi ya watu kujeruhiwa vibaya.

Imefahamika kuwa moto huo ulianzia katika chumba cha dharura cha Hospitali ya Sejong, kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Zaidi ya majeruhi 100 wanasemekana wamo katika jengo la hospitali hiyo.

Mwaka jana watu 29 walikufa katika mji wa Echeon, Korea Kusini, na wengine kujeruhiwa baada ya moto kuzuka katika sehemu ya mazoezi ya wazi.

VIDEO: Makonda Aangua Kilio


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda  leo ametembelea na kutoa pole  kwa Familia ya Wastaafu ya Bwana Edward Bejumula na Bi. Stella Bejumula walioteseka kwa Miaka Sita bila Makazi baada ya kudhulumiwa Nyumba yao ambapo ameahidi kulivalia njuga suala hilo kuhakikisha haki inatendeka bila kuvunja sheria.

 TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI .....USISAHAU KUSUBSCRIBE



VIDEO: Full Video CCM Wakizindua Kampeni Kinondoni


Chama cha Mapinduzi CCM kimezindua kampeni zake za Ubunge wa jimbo la Kinondoni huku Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba pamoja na Waziri wa zamani wa Maji, Steven Wassira wakimnadi mgombea wa Chama hicho, Maulid Mtulia.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USISAHAU KUSUBSCRIBE

Kauli ya Jaji Mkuu yaamsha upya hoja ya mgawanyo wa madaraka


Kauli ya hivi karibuni Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma kuwa viongozi wa Serikali na wanasiasa wasiingilie Mahakama na kudharau amri za mhimili huo, imeamsha upya hoja la mgawanyo wa madaraka baina ya mihimili mitatu ya dola ambayo imekuwa mjadala kwa muda mrefu.

Mjadala kuhusu mgawanyo huo wa Serikali, Bunge na Mahakama umekuwapo nchini kwa muda mrefu hasa wakati wa mchakato wa mabadiliko ya Katiba kuwa inaonekana Serikali ama inaizidi nguvu au inaingilia shughuli za mihimili mingine, licha ya kwamba yote hiyo inatakiwa kuonekana sawa.

Hata hivyo, baadhi ya watu huamini kwamba mhimili wa Serikali ambao unaongoza dolo ndio wenye nguvu kwa kuwa unasimamia mapato na matumizi ya mihimili mingine.

Hata Rais John Magufuli alipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu suala hilo Novemba 2016, alisema, “Mihimili hiyo (Bunge, Serikali na Mahakama) inaweza ikalingana, lakini inawezekana kuna mhimili ambao umechimbiwa zaidi kwenda chini.”

Akisisitiza jibu lake, Rais alizungumzia jinsi alivyokwenda kwenye shughuli ya mahakama na akaombwa fedha na uongozi wa mhimili huo kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli zake kwa kutambua kuwa, Rais ndiye mwenye uwezo wa kuwapatia fedha hizo.

Ndani ya mjadala huo, pia yamekuwapo madai miongoni mwa wananchi kupitia maoni yao wakati wa mchakato wa Katiba, wanasiasa, wanaharakati kuwa Serikali imekuwa inaingilia shughuli na mihimili mingine – Bunge na Mahakama, jambo ambalo linaathiri uhuru wake.

Pengine ni kutokana na madai hayo au mengine, ndipo Jaji Mkuu anaibuka na ujumbe mahususi kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria kwa Serikali;

“Nawasihi viongozi wote wa Serikali wenye mamlaka za kikatiba na kisheria, wabaki ndani ya maeneo yao ya kikatiba na wajiepushe na kuingilia maeneo yaliyo ndani ya haki, hadhi na mamlaka ya Kikatiba ya Mahakama.”

Akaongeza kwamba kuanzia sasa (Mahakama) watakuwa wakali kwa mtu atakayeingia katika anga zao, huku akiwataka mahakimu na majaji kuchukua hatua kwa watu wanaodharau amri zao, kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, mamlaka ya utoaji haki ni ya Mahakama pekee.

Hata hivyo, akijibu kwa nini aliamua kutoa kauli hiyo, Jaji Mkuu anasema ni kutokana na taarifa za vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikiripoti matukio hayo ya amri za Mahakama kuvunjwa.

Hakuishia hapo, Jaji Mkuu akawataka mahakimu ambao kwa bahati mbaya amri zao zinavunjwa na wanaonekana hawachukui hatua waanze kufanya hivyo kama Bunge linavyofanya, kwamba ukiingia katika anga zake, utaitwa mbele ya kamati, utaulizwa maswali na hatua zinachukuliwa.

Jaji Mkuu anasema Mahakama ina nguvu kama hiyo na si Jaji Mkuu mwenye nguvu hiyo pekee bali kwenye kila Mahakama; mahakama za mwanzo, mahakama za wilaya na mahakama za hakimu mkazi na asitokee mtu akajivika kofia ya kimahakama, atachukuliwa hatua.

Jaji Juma anasema kwa mujibu wa Katiba, sheria ndio inayotakiwa ipewe nguvu na si masuala ya kisiasa kwa kuwa nguvu ya Serikali ni sheria na si mtu.

“Sheria ikikupa nguvu unaitumia, ikikupa mamlaka unayatumia. Siasa haikupi nguvu, sheria ndio inakupa nguvu na tujaribu tubaki ndani ya sheria na ndani ya Katiba hakutakuwa na mvurugano. Vilevile tunawataka wale ambao wamepewa mamlaka yao, wabaki huko waliko na tukifanya hivyo hatutakuwa na migongano yoyote,” anahitimisha.

Kauli hiyo ya inaungwa mkono na Ibara ya 107 A (1) ya Katiba ya Tanzania inayosema: “Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Mahakama ya Tanzania na Mahakama ya Zanzibar, na kwa hiyo hakuna chombo cha Serikali wala cha Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki.”

Mjadala mtandaoni

Muda mfupi baada ya maelezo hayo, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, “Mh Jaji Mkuu kauli kuhusu wanasiasa na watendaji wa Serikali kutokuingilia Mahakama ni kauli muhimu kwa wakati huu, lakini Mahakama ambayo ni imara katika haki inawezaje kukubali kuingiliwa? Mahakama inapaswa kujitazama zaidi. Mahakama ikiyumba Taifa linayumba.”

Si Lema tu aliyezungumzia hilo, wananchi wengine mbalimbali walitoa maoni yao kuhusu kauli hiyo kupitia ukurasa wa Facebook wa Mwananchi, Twitter na Instagram, huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kumtaka Jaji Mkuu kuwaeleza maneno hayo wafuasi wa CCM, wakidai kwamba wapinzani hawana jeuri ya kuingilia Mahakama.

Kwa jinsi mjadala ulivyokwenda ni wazi kuwa Jaji Mkuu Profesa Juma ameona kuna kitu ambacho pia wananchi wanakiona hakiendi sawa na kuamua kufikisha ujumbe wake kwa njia hiyo.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanatafsiri kauli ya Jaji Mkuu kama “kuchoshwa kwa mhimili huo kuingiliwa na hivyo ameamua kufikisha ujumbe kwa wenye tabia hizo ili waache mara moja.

Hatua ya Jaji Juma bila shaka ni ya kupongezwa kwani si tu imeonyesha kwamba mahakama imezinduka na kutambua wajibu na nguvu zake na hivyo inafungua pazia la demokrasia na mgawanyo wa madaraka baina ya mihimili hii mitatu ya dola.

Hatua hiyo ikizingatiwa na kutekelezwa itasaidia kuifanya mahakama iaminike na kiwe chombo pekee kimbilio kwa kila mtu kwa ajili ya utoaji haki.

Ingawa Jaji Mkuu hakutoa mifano ya matukio ya kuingilia uhuru wa mahakama, mifano ipo mingi, mfano wameshuhudiwa baadhi ya watendaji wa Serikali wakiamuru ubomoaji wa nyumba ambazo inadaiwa zimejengwa katika hifadhi ya barabara, zikiwamo zilizokuwa na amri ya mahakama ya kuzuia zisibomolewe.

Mbali na mahakama, hivi karibuni Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe aliwakaririwa akisema hata Bunge limekuwa likifanya kazi kwa kuingiliwa na Serikali.

“Maneno na vitendo vya Rais vinaashiria kuwa Bunge halina uhuru wake na mimi kama mbunge nina wajibu wa kuonyesha kutopendezwa kwangu,” alisema Zitto kupitia mtandao wa Twitter na kuongeza kuwa “Ni dalili ya wazi ya kufifisha sauti ya Bunge na kupandisha sauti ya Serikali.

Moja ya matukio ambayo mbunge huyo alitaja kama kuingilia mhimili huo ni kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge kwa kigezo cha gharama, huku hata vituo binafsi ambavyo vilipanga kurusha Bunge moja kwa moja bila malipo vikizuiwa.

Akijadili suala la uhuru wa mahakama na kauli ya Jaji Mkuu, Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa anasema kwa muda mrefu wanasiasa na watetezi wa haki wamekuwa wakipigia kelele suala hilo lakini halikuonekana kufanyiwa kazi, hivyo hatua ya Jaji Mkuu italeta matumaini yalikuwa yametoweka.

Anasema katika suala la utoaji haki, Mahakama inapaswa kusimama kwa miguu yake isishurutishwe na isiingiliwe; majaji wazingatie sheria wakati wa kutoa hukumu.

Haiingii akilini kwamba mahakama inatoa amri fulani, lakini watendaji walioko chini ya Serikali wakapuuza na wakaendelea na shughuli zao kana kwamba hakuna amri yoyote,” anasisitiza.

“Jaji Mkuu yuko sahihi kama kweli anamaanisha. Kwa muda mrefu tumeshuhudia viongozi mbalimbali wakiwamo wakuu wa wilaya wakijitokeza kuingilia mhimili huo na kusababisha ama kupingana au kuwagawa na matokeo yake wanashurutishana na kutishana hadharani.”

Onesmo anasema hata kama Mahakama imekosea, kuna utaratibu wa kisheria wa kufuata ili kuipinga na si kama hali ilivyo sasa.

Anasema kuwa jambo hilo la kuingiliwa Mahakama likiachiwa liendelee litasababisha athari kuu tatu kwa jamii na kuzitaja kuwa ni pamoja na kuvunja Katiba.

Mosi, anasema mahakama ni chombo cha kutoa haki na endapo haitakuwa huru, ni wazi kuwa Katiba itakuwa inavunjwa na mwananchi atakosa haki zake za msingi.

Pili, anasema tatizo jingine ni kutengeneza Taifa lisilo fuata utawala wa kisheria na kwamba watu wataamua wanavyotaka wao, jambo ambalo litakuwa si zuri kwa mustakabali wa nchi.

“Jingine, ni kuingia katika migogoro isiyo na tija; itafika wakati wananchi watachoshwa na matendo hayo na kusababisha migogoro mikubwa na matokeo yake hayatakuwa mazuri,” anasisitiza Mratibu huyo wa masuala ya haki za binadamu.

Ni kutokana na umuhimu huo na mjadala mpana katika mchakato wa Katiba ikawekwa ibara ya 169 inazungumzia kwa kina uhuru wa mahakama.

Katiba inayopendekezwa

196 (1) Katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki, Mahakama zote zitaongozwa na masharti ya Katiba hii na hazitaingiliwa ama kwa kudhibitiwa, kushinikizwa au kupewa maelekezo na mtu au chombo chochote.

(2) Nafasi ya madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano haitafutwa wakati wowote ule ikiwa kuna mtu ambaye kwa wakati huo anashikilia nafasi hiyo.

(3) Mishahara na malipo mengine ya Majaji wa Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano yatalipwa kutoka katika Mfuko Mkuu wa Hazina.

(4) Mshahara na malipo mengine yanayolipwa kwa Jaji wa Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano hayatabadilishwa kwa maana ya kumuondolea faida Jaji husika.

(5) Malipo ya mafao ya kustaafu ya Jaji wa Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufani au Mahakamu Kuu ya Jamhuri ya Muungano hayatabadilishwa kwa maana ya kumuondolea faida Jaji husika wakati wote wa uhai wake.

(6) Jaji wa Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufani, Mahakamu Kuu ya Jamhuri ya Muungano au Mahakama Kuu ya Zanzibar hatashtakiwa kwa jambo lolote alilolifanya au kutolifanya kwa nia njema katika   

Mwananchi. 

Chadema yazidi kukimbiwa na madiwani wake



Wimbi la madiwani wa Chadema kujivua uanachama na kujiunga na CCM limezidi kukikumba chama hicho kikuu cha upinzani nchini baada ya leo Januari 27, mwaka 2018 madiwani wake wanne kujiunga na chama tawala, wakiwemo watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo  mkoa wa Kilimanjaro.

Wakati diwani wa Kimara (Chadema), Pachal Manota akitambulishwa katika uzinduzi wa kampeni za ubunge za chama hicho jimbo la Kinondoni zilizofanyika viwanja wa Biafra, wenzake watatu walitambulishwa kwenye mkutano wa kampeni za ubunge jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro uliofanyika eneo la Makiwaru.

Madiwani hao ni Juliana Malamsha, Martha Ushaki (wote Viti maalum) na Frank Umega (kata ya Kelamfua).

Wametambulishwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo wakati akimnadi mgombea ubunge wa chama hicho jimbo la Siha, Dk Godwin Mollel.

Mpogolo amesema viongozi wa upinzani wanajiunga na CCM baada ya kubaini ajenda ya kuwahudumia wananchi, kuwaletea maendeleo ipo katika chama tawala pekee .

"Kuna  wimbi kubwa la viongozi wa upinzani kujiunga na CCM. Hii inatokana na viongozi hao kubaini kuwa ajenda ya huduma na maendeleo iko katika chama hiki pekee. Tupeni Dk Mollel ili tuweze kutekeleza agenda hii muhimu,” amesema Mpogolo.

Uamuzi wa madiwani wa Chadema kuhamia CCM mpaka sasa umeziweka Halmashauri tano zilizo chini ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuwa hatarini kuchukuliwa na CCM.

Halmashauri hizo ni Arusha, Arumeru, Hai, Siha na Iringa ambazo madiwani wake, hasa kutoka Chadema wametimkia CCM kutokana na sababu tofauti, kubwa ikiwa ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais John Magufuli.

Ahadi ya Jafo Siha yafananishwa na rushwa


Wasomi wameifananisha na rushwa ya uchaguzi ahadi iliyotolewa kwa wananchi wa Jimbo la Siha kuwa watapata neema iwapo watamchagua mgombea wa CCM, Dk Godwin Mollel ambaye anatetea ubunge aliouachia mwishoni mwa mwaka jana kwa kujivua uanachama wa Chadema.

Ahadi hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Selemani Jafo wakati akimnadi mgombea Dk Mollel.

Wamesema kauli hiyo inaweza kusababisha ushindi wa Dk Mollel kupingwa, huku Profesa Abdallah Safari akienda mbali zaidi na kufananisha kauli hiyo na iliyowahi kutolewa na mawaziri kadhaa wakati wa uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga mwaka 2011 na kusababisha ushindi wa aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk Dalali Kafumu kubatilishwa na Mahakama.

Akiwa jukwaani, Jafo alisema CCM ndicho chama chenye Serikali na ndicho kinachoweza kutatua changamoto na shida za wananchi, na kwamba akishinda Serikali itafanya kila njia kuboresha maisha ya wananchi.

Jafo alisema ikiwa wananchi watamchagua Dk Mollel ambaye hivi karibuni alijiondoa Chadema na kugombea tena nafasi hiyo kupitia chama tawala, Serikali itashirikiana naye na miaka miwili iliyobaki Siha itakuwa moja ya wilaya ambazo zitapiga hatua kubwa na kufanya vizuri katika utekelezaji wa maendeleo.

Lakini ahadi hiyo ya Waziri Jafo kwa wananchi wa Siha haijapokelewa vizuri na wasomi waliohojiwa na Mwananchi.

“It is a sort of (ni kama-rushwa) kwa wapiga kura kupitia miradi ya maendeleo ya Serikali, anaposema Dk Mollel akishinda ndipo hospitali ijengwe,” alisema Dk Hamad Salim, mhadhiri wa sayansi ya siasa wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Dk Salim alisema kauli hiyo inaashiria rushwa na kushauri mawaziri watenganishwe na vyama vya siasa.

“Kuna haja ya kutenganisha mawaziri na vyama vya siasa. Mawaziri wanapaswa kuwa watendaji wa Serikali. Kauli ile inakera mno. Ni afadhali tu angesalimia na kuongea kama mwana CCM kuliko kuihusisha Serikali,” alisema.

Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Richard Mbunda alisema kauli ya Jafo inakwenda kinyume na sheria ya gharama za uchaguzi.

“Sheria ya gharama za uchaguzi iliyoanzishwa mwaka 2010 haikusikika sana kwenye uchaguzi wa 2015, lakini inaeleza vizuri. Kifungu cha 21(a) na (c) vinakatza hata mgombea tu kuahidi kutoa zawadi ili achaguliwe, kwa sababu itahesabika kama rushwa?” alisema Dk Mbunda.

Naye Profesa Safari alisema ikiwa mgombea wa Chadema katika jimbo hilo, Elvis Mosi atashindwa katika uchaguzi huo, wataitumia kauli ya Jafo kupinga matokeo mahakamani.

Katika ufafanuzi wake, Profesa Safari alisema kauli ya Jafo inaashiria utoaji wa rushwa na inaweza kusabababisha kesi kama ya Jimbo la Igunga.

“Hiyo ni corruption (rushwa) kabisa na ndiyo maana ile kesi ya Igunga tulishinda,” alisema Profesa Safari ambaye ni makamu mwenyekiti wa Chadema-Bara.

“Ni kauli mbaya sana na inaweka mazingira ya kupinga uchaguzi huo endapo mgombea wa CCM atashinda. Kesi ya Igunga imekuwa ikirejewa katika kesi nyingi tu.”

Hata hivyo, mkurugenzi wa taasisi ya Fordia, Buberwa Kaiza amesema kauli ya Jafo inaweza isihesabike kama rushwa kwa sababu hospitali yenyewe haijajengwa, japo kimaadili kutoa ahadi kama hiyo ni kosa.

“Maadili ya uchaguzi yanazuia kabisa mtu kutumia mali za Serikali kufanyia kampeni chama cha siasa. Maadili pia yanazuia kabla na baada ya uchaguzi kutumia majukumu ya Serikali kama ahadi ya uchaguzi,” alisema.

“Kama ilani ya uchaguzi ya CCM ilisema watajenga hospitali na yeye alikuwa akikumbushia, sawa. Lakini kama alisema mgombea wao akichaguliwa ndipo watajenga, hilo ni kosa.”

Wakimbizi kutoka Kongo wazidi kumiminika nchini


Zaidi ya raia 800 kutoka jamhuri ya kidemikrasi ya Kongo wamewasili mjini kigoma kuomba hifadhi ya ukimbizi nchini wakidai kukimbia vita katika nchi hiyo.

Raia hao wa DRC ambao wengi ni wanawake na watoto wametokea mashariki ya nchi hiyo na wamewasili kwa maboti kwa nyakati tofauti katika bandari ndogo ya Kibirizi mjini kigoma na kueleza kuwa hali ya vita katika nchi hiyo ni mbaya na kuomba serikali ya Tanzania kuwapokea.

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa amefika katika eneo hilo na kueleza kuwa wamewapokea lakini serikali inafanya tathmini ya ujio wao.

Ujenzi wa reli ya kisasa watarajiwa kuanza Machi mwaka huu


Serikali imesema ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge) kutoka Morogoro hadi Makutopora mkoani hapa ambao utaanza kabla ya Machi mwaka huu, utagharimu dola 1.923bilioni za kimarekani (sawa na Sh4.3 trilioni).

Meneja Mradi huo wa Kampuni Hodhi ya Raslimali za Reli (Rahco) Mhandisi Maizo Mgedzi amesema mradi huo unatarajia kuanza wakati wowote kabla ya Machi.

Amesema  treni hiyo ina uwezo wa kwenda kilometa 160 kwa saa itahifadhi mazingira na kwamba itaweza kubeba mzigo mkubwa kwa zaidi ya mara tano ya reli ya sasa.

“Pia itaweza kubeba watu na mizigo kwa usalama kwa maana  hakutakuwa na ajali zinazosababishwa na ubovu wa miundombinu,” amesema

Meneja wa Kampuni ya Yapi Merkezi iliyopewa zabuni ya mradi huo, Abdullah Kilic amesema kuwa jiwe la msingi la mradi huo litawekwa wakati wowote kuanzia sasa.

“Tunachosubiri ni utaratibu wa Ikulu lakini jiwe la msingi tutaliweka wakati wowote kuanzia sasa,”amesema.

Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini, Antony Mavunde amesema Serikali ingependa mradi huo ulete matokeo chanya kwa watu wa Dodoma na si laana.

“Matokeo haya yasiwe laana kwa maana tusije kuiacha reli hii ipite tu hapana. Sisi tunataka kwa watu wa Dodoma reli hii iwe kichocheo cha kwanza cha uchumi ikiwezekana kubadilisha mji,”amesema.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kongwa alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Deogratius Ndejembi amesema viongozi watawapa ushirikiano wa kutosha katika kipindi cha miaka mitatu cha ujenzi wa reli hiyo na kurekebishana kwa baadhi ya mambo.

“Wamesema asilimia 80 (watu 3000) watachukua watu wa Dodoma kwa hiyo ni jambo kubwa sana. Hii ni fursa kubwa hata kipindi hiki cha ujenzi,”amesema.

Friday 26 January 2018

Audio | Lava Lava – Tattoo | Mp3 Download

Audio | Lava Lava – Tattoo | Mp3 Download

Audio | Lava Lava – Tattoo | Mp3 Download

Audio | Foby – Ngangana | Mp3 Download

Audio | Foby – Ngangana | Mp3 Download

Audio | Foby – Ngangana | Mp3 Download

Rais Trump aombwa kuchukua choo cha dhahabu


 
Choo cha dhahabu alichopendekezewa rais Donald Trump
Jumba la kumbukumbu la Guggenheim mjini New York limekataa ombi kutoka kwa rais Donald Trump la kutaka kupewa mchoro wa msanii Van Gogh ili kuwekwa katika ikulu ya Whitehouse kulingana na vyombo vya habari.

Jumba hilo liliomba msamaha kwa kutoweza kupeana picha hiyo na badala yake likaomba kumpatia rais Trump choo cha dhahabu kulingana na gazeti la The Washington Post.

Lakini jumba hilo la kumbukumbu lilipendekeza limpatie rais Trump kiti hicho cha choo chenye dhahabu karati 18.

Ikulu ya Whitehouse haijatoa tamko lolote.

Kulingana na gazeti hilo,mhifadhi wa vitu katika jumba hiloi Nancy Spector aliojibu ombi hilo la Ikulu mwezi Septemba.

''Naomba msamaha...kukujulisha kwamba hatuwezi kushiriki katika kukupatia picha hiyo kwa kuwa ni miongoni mwa mkusanyiko wa Thannhauser ambao hawaruhusiwi kutoka nje ijapokuwa kwa maswala yasio ya kawaida'', aliandika katika barua pepe.

Picha hiyo ya 1888 ya Van Gogh, barua hiyo iliongezea itaonyeshwa katika taasisi dada kutokana na ruhusa kutoka kwa wamiliki wake.

Hatahivyo , muhifadhi huyo ameongezea kwamba choo hicho cha dhahabu kilichotengezwa na msaani wa Itali Maurizio Cattelan kiko tayari kwenda Ikulu kwa ''mkopo wa muda mrefu''.

Ni jambo la kawaida kwa marais wa Marekani na wake zao kuomba kazi za usanii ili kupamba baadhi ya vyumba katika Ikulu ya Whitehouse.

Tambwe kuivaa Azam FC kesho?


Straika wa Yanga, Amissi Tambwe raia wa Burundi ameshindwa kufanya mazoezi ya pamoja na wenzake kutokana na majeraha ya goti.

Hali hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu arejee na acheze mechi dhidi ya Mwadui FC kabla ya kuwavaa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar. Mshambuliaji huyo akiwa amekaa nje ya uwanja huku wenzake wakiendelea na mazoezi.

Mshambuliaji huyo, alipata majeraha hayo juzi Jumatano katika mazoezi ya timu hiyo baada ya kugongana na beki wa pembeni, Juma Abdul na kushindwa kuendelea na programu nyingine.

Kutokana na Tambwe kushindwa kufanya mazoezi ya mwishoni ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo huo, upo uwezekano wa Mrundi huyo kuikosa mechi dhidi ya Azam FC.

Katika mazoezi hayo ya jana, benchi la ufundi la timu hilo, lilionekana kuwaandaa baadhi ya washambuliaji watakaocheza nafasi yake ambao ni Juma Mahadhi na Yohana Nkomola.



Rais Magufuli,Mama Janet wamchangia Wastara Fedha za matibabu




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mke wake Mama Janet Magufuli hii leo wamemchangia muigizaji wa filamu Tanzania Wastara Juma shilingi milioni 15, kumsaidia katika matibabu yake.

Fedha hizo ambazo Wastara amekabidhiwa na Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike , sambamba na kiasi kingine cha milioni moja na laki tisa ambayo ni michango kutoka kwa wasaidizi wa Rais.

Msanii huyo amekuwa akisumbuliwa na mguu kwa muda mrefu na alikuwa kaomba msaada wa watanzania mitandaoni ili aweze kwenda nchini India kupatiwa matibabu.

Rais Magufuli anakuwa mtu wa kwanza kutoa fedha nyingi kwa msanii huyo, tangu aanze kutoa rai ya kuomba michango, ambapo wiki iliyopita waziri wa Habari, sanaa, michezo na utamaduni Dkt. Harison Mwakyembe alimkabidhi shilingi milioni moja.
Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi fedha Wastara

Kesi ya Tido Mhando yaahirishwa hadi Februari 23


Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando amepata dhamana baada ya kukidhi masharti na kutakiwa kurejea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Februari 23, mwaka huu.

Tido alifikishwa mahakamani hapo saa 5:22  asubuhi na aliingizwa katika ukumbi wa mahakama ya wazi kabla ya kusomewa mashtaka matano.

Leo Januari 26, mwaka 2018 wakili wa Takukuru, Leonard Swai amedai mbele ya hakimu mkazi mkuu wa makahama hiyo,  Victoria Nongwa kuwa Mhando anatuhumiwa kwa mashtaka matano.
Swai amesema Juni 16, 2008 katika maeneo ya Dubai, United Arab Emirates (UAE), Tido akiwa mwajiriwa wa TBC kama Mkurugenzi Mkuu kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa makubaliano kwa ajili ya kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 group Corporation ( BV1) bila ya kupitisha zabuni kinyume  na sheria ya manunuzi na kuisababishia BVl kupata manufaa.

Shtaka la pili, Tido anadaiwa Juni 20, 2008  katika maeneo ya utekelezaji wa kazi yake alitumia madaraka vibaya kwa kusaini makubaliano (wakuu wa makubaliano) kwa utangazaji wa digital duniani kati ya TBC na BVl.

Shtaka la tatu, Agosti 11, 2008  na Septemba 2008 katika maeneo hayo, Tido anadaiwa kutumia  vibaya madaraka yake kwa kusaini mkataba wa makubaliano (kuongeza wakuu wa mkataba ) kwa ununuzi, usambazaji kufunga vifaa vya usambazaji na mnara wa utangazaji kati ya TBC na BVI na kuisababishia BVI kupata faida.

Shtaka la nne, Tido anadaiwa Novemba 16,2008 akiwa Dubai, United Arab Emirates alitumia vibaya madaraka yake kwa kusini mkataba wa makubaliano (kuongeza wakuu wa mkataba ) kwa kuendesha miundombinu ya utangazaji (DTT broadcast infrastructure) kati ya TBC na BVI na kusababisha BVI kupata manufaa.

Katika shtaka la tano, Tido anadaiwa kati ya Juni 16 na Novemba 16, 2008 katika maeneo hayo ya United Arab Emirates aliisababishia hasara TBC ya Sh 887, 122,219.19.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Tido ambaye anatetewa na wakili Ramadhani Maleta alikana mashtaka yote.

Swai alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Hakimu Nongwa alimtaka mshtakiwa kutoa fedha taslimu mahakamani hapo Sh444 milioni ama hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Mbali na sharti hilo, pia awe na wadhamini wawili ambapo watasaini hati ya dhamana ya maneno yenye thamani ya Sh500 milioni na asitoke nje ya nchi bila ya kuwa na kibali cha mahakama.
Mshtakiwa alikamilisha masharti hayo kwa kuwasilisha hati za mali na wadhamini wawili nyakati za saa sita mchana na kuondoka.

Kesi imeahirishwa hadi Februari 23, 2018 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (PH).
Kuhusu dhamana hiyo, DPP alipeleka hati ambayo inaipa mamlaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuisikiliza kesi hiyo.

Mhando ni miongoni mwa waandishi wa habari na watangazaji mahiri na wakongwe ndani na nje ya nchi ambaye amewahi kufanya kazi Shirika la Utangazaji Uingereza (BBC).
Pia amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) inayochapisha magazeti ya Mwananchi, Mwanspoti na The Citizen na sasa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media.

Nyumba za Askari Magereza zatakiwa kukamilika ndani ya miezi mitano


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali mstaafu, Projest Rwegasira ametoa miezi mitano kwa Wakala wa Majengo (TBA) kukamilisha ujenzi wa nyumba za askari wa Jeshi la Magereza zilizoko Ukonga jijini Dar es Salaam.

Ametoa agizo hilo leo Ijumaa Januari 26,2018 alipofanya mazungumzi na maofisa wa TBA na wa Jeshi la Magereza baada ya kukagua ujenzi huo.

“…fanyeni juu chini mhakikishe mradi huu unakamilika ndani ya miezi hiyo mitano mliyosema. Ongezeni nguvu ili mkamilishe mradi huu kwa wakati,” amesema katika taarifa iliyotolewa na wizara.

Fedha za ujenzi wa nyumba hizo unaogharimu  Sh10 bilioni zilitolewa na Rais John Magufuli baada ya kufanya ziara Ukonga mwishoni mwa mwaka 2016.

Soma: Waziri Mkuu aagiza wakala wa majengo Mara kukamatwa

Ujenzi ulianza mwaka jana badala ya Desemba 19, 2016.

NEC yatoa orodha ya wagombea wa udiwani



Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa majina 27 ya wagombea udiwani walioteuliwa na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kuwania nafasi hizo katika kata 10.

Uchaguzi mdogo katika kata hizo utafanyika Februari 17,2018 kutokana na baadhi ya madiwani kujiuzulu nyadhifa zao na vifo.

Katika uteuzi huo wanaume waliojitokeza kugombea nafasi hizo ni 24 na wanawake ni watatu.

Taarifa iliyotolewa na NEC leo Ijumaa Januari 26,2018 imesema wagombea wa kata nne waliteuliwa Januari 20 na wengine wa kata sita waliteuliwa Januari 24,2018.

Wagombea waliojitokeza kuwania udiwani katika kata ya Buhangaza iliyoko wilayani Muleba mkoani Kagera na vyama vyao ni Jenitha Tibihenda (CCM), Nelson Makoti (Chadema) na Grayson Aniceth (NCCR Mageuzi).

Katika Halmashauri ya Siha iliyoko mkoani Kilimanjaro ambako kuna kata tatu zitakazofanya uchaguzi mdogo, wagombea katika kata ya Gararagua ni Zakaria Lukumai (CCM) na Agness Lasway (Chadema). Kata ya Donyomuruak wagombea ni Lwite Ndossi (CCM) na Daniel Molle (Chadema), wakati katika kata ya Kashashi wagombea ni Suzan Natai (CCM) na Immanuel Saro (Chadema).

Mkoani Mwanza ambako kuna kata mbili, wagombea wa kata ya Kanbyelele iliyoko Halmashauri ya Misungwi ni Marco Yela (ACT Wazalendo), Daniel Makoye (CCM) na George Mhoja (Chadema). Kata ya Isamilo iliyoko wilayani Nyamagana wagombea ni Nyamasiriri Marwa (CCM), John Kisyeri (Chadema), Hashim Ramadhan (CUF), Georgina Kibendegele (DP) na Ramadhani Mtoro (UDP).

Kwenye kata ya Mitunguruni iliyoko wilayani Singida wagombea ni Abdallah Mkoko (CCM), Manase Kijanga (Chadema) na Abdallah Kinga (CUF).

Wagombea wa Kata ya Madanga iliyoko wilayani Pangani mkoani Tanga ni Mohamed Abdallah (ACT Wazalendo), Athuman Tunutu (CCM) na Swaibu Mwanyoka (CUF).

Mkoani Dodoma ambako pia kata mbili zitafanya uchaguzi, kata ya Manzase iliyoko wilayani Chamwino wagombea ni Amos Mloha (CCM), Alex Chalo (Chadema) na Ndahani Mazengo (Chaumma), wakati kata ya Kimagai wilayani Mpwapwa mgombea ni Noah Lemto aliyepita bila kupingwa.


Hospitali ya Bugando yanufaika na mashine za CT-SCAN


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amezindua huduma za mashine ya CT – SCAN katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa Bugando jijini Mwanza,ambazo zilisimama kwa muda wa miaka minne iliyopita, baada ya mashine iliyokuwepo awali kuharibika mwaka 2014.

Mashine hiyo ya kisasa,iliyonunuliwa nchini Ujerumani kwa gharama ya shilingi Bilioni 1.7,imesimikwa na kufanyiwa majaribio na uhakiki kutoka tume ya mionzi Tanzania na kuthibitika kuwa na uwezo wa kufanya kazi ipasavyo.Mashine hiyo kwa mujibu wa daktari bingwa wa mionzi Dk.Godfrey Kasanga itakuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa 100 kwa siku.

Askofu wa jimbo katoliki la Geita,Mhashamu baba askofu Flavian Kasala,ambaye amemwakilisha Mwenyekiti wa bodi ya uendeshaji ya hospitali hiyo,Mhashamu Askofu Mkuu jimbo kuu la Mwanza Yuda Thadei Rwaichi,amewataka watumishi wa kitengo kitakachosimamia huduma za mashine hiyo kuitunza na kuacha kuihujumu.

Kwa upande wake,Mkurugenzi mkuu wa hospitali ya rufaa ya Kanda ya ziwa Bugando Dk.Abel Makubi ameiomba serikali kuanzisha taasisi ya moyo katika hospitali hiyo ili kupunguza idadi ya wagonjwa kutoka mikoa ya kanda ya ziwa wanaokwenda Dar es Salaam kutafuta matibabu ya moyo katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete.


Wazazi wavamia shule kudai kurejeshewa michango yao


Baadhi ya wazazi katika halmashauri ya mji wa wa Mbinga mkoani Ruvuma wameshindwa kulielewa agizo la Rais John Magufuli la kufuta michango katika shule za msingi na sekondari na  kuvamia shule wakidai kurejeshewa michango yao.

Kufuatia hali hiyo Baraza la halmashauri ya mji wa Mbinga limeitisha kikao cha dharura kujadili changamoto hizo na nanmna ya kuzitatua huku Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Mbinga Donald Msigwa akiwataka madiwani kutopingana na agizo la Rais katika majadiliano hayo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Mbinga mheshimiwa egno Kipwere amesema agizo la Rais halijahalalisha wananchi kudai kurejeshewa michango waliyochangia na halijafuta michango waliyokubaliana wenyewe kuchangia.

Wenger ajigamba kuhusu usajili wake


Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema timu hiyo haitauza mchezaji bila kununua mchezaji huku pia akiongelea usajili wa Aubameyang kuwa bado haujakamilika.

Kocha huyo mkongwe ameyasema hayo leo alipokuwa akitoa ripoti ya majeruhi na programu za timu kwa ujumla, ambapo amesisitiza nyota wake Olivier Giroud hauzwi kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa.

''Kwasasa hauzwi mchezaji yoyote bila kununua mchezaji wa kuchukua nafasi yake, tumemuuza Sanchez lakini tumempata Mkhitaryan hivyo timu iko vizuri na kikosi cha wachezaji waliopo'', amesema Wenger.

Pia Mfaransa huyo ameongeza kuwa milango pekeee itakayokuwa wazi ni kwa timu za vijana ambapo kuna baadhi watatolewa kwa mkopo na wengine watapandishwa kwenye kikosi cha wakubwa.

Kuhusu kumsajili nyota wa Gabon na Borussia Dortmund Pierre Aubameyang, Wenger amesema bado hawezi kusemea lolote kwasababu hakuna kilichokamilika na mchezaji huyo bado ni mali ya Dortmund.



Kumbe CCM wenyewe wanasubiri kuapishwa tu?

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amefunguka na kusema kuwa wagombea wa Ubunge kupitia chama chake katika uchaguzi wa marudio katika majimbo ya Kinondoni na Siha wanasubiri kuapishwa tu na kuingia bungeni.

Polepole amesema hayo alipokuwa akihojiwa na moja ya kituo cha habari na kusema kuwa kwa jinsi ambavyo wana CCM wamefanya kazi nzuri sana Kinondoni na Siha kuhakikisha wanawanadi na kuwauza wagombea wao hivyo wana uhakika wa kushinda uchaguzi huo kwa kishindo.

"Kwa utafiti tunaofanya na kazi nzuri tuliyofanya tunasubiri kutangazwa washindi katika majimbo yote mawili pale Kinondoni na Siha" alisisikika Polepole akisema

Mbali na hilo Polepole amekanusha chama hicho kuwa na mvurugano wa wenyewe kwa wenyewe kufuatia kusimamisha wagombea katika majimbo hayo ambao hawana muda mrefu katika chama hicho wakitokea upinzani na kusema kwa CCM kila mwanachama ana haki sawa na wanachama wengine.

Chama Cha Mapinduzi kimemsimamisha Maulid Mtulia kugombea Ubunge kwa jimbo la Kinondoni wakati katika jimbo la Siha kimemsimamisha Dk Godwin Mollel ambao wote walikuwa ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokea vyama vya upinzani, lakini walijivua uanachama kwenye vyama vyao na kujiunga na CCM.

Unaambiwa kesho Simba wataishangilia Yanga



Watani wa jadi Simba na Yanga, kesho Jumamosi watakuwa kitu kimoja kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaowakutanisha Azam na Yanga kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Watani hao watakuwa kitu kimoja kwani Simba inahitaji kuendelea kukaa kileleni bila ya wasiwasi, huku Yanga ikihitaji kuzisogelea timu zilizokuwa juu yake katika harakati zake za kutetea ubingwa wa ligi hiyo.

Kwenye msimamo wa ligi hiyo, Simba inaongoza ikiwa na pointi 32, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 30, huku Yanga ikiwa na pointi 25 katika nafasi ya tatu.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema: “Tumesikia Simba kesho watakuja kutushangilia, niseme tu hii si mara ya kwanza wao kutushangilia, wameshatushangilia mara nyingi, ni jambo jema, sisi ni watani wa jadi na hakuna uadui kati yetu.

Wanaovamia Maeneo Ya Serikali Kukiona Cha Moto Dar


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wananchi wanaopenda kuvamia maeneo ya Serikali yakiwemo maeneo ya shule kuacha na kuondoka mara moja kwani hatua Kali za kisheria  dhidi yao zitachukuliwa ikiwa pamoja na kufikishwa mahakamani.

Makonda amesema hayo leo jijini Dar es Salaam, alipokuwa anazindua uezekaji paa wa Ofisi za Walimu katika shule ya Msingi Mapinduzi iliyopo katika manispaa ya Kinondoni  na kusema kuwa kutokana na shule kutokuwa na uzio watu  wamekuwa wakijiamulia kujenga au kufanya makazi katika maeneo ya shule kitendo ambacho si sahihi.

"Wale wanaojipangia kuhamia au kuvamia maeneo yaaliyo wazi ya Serikali yakiwemo maeneo ya shule, hospitali na mengineyo  na kufanya makazi  kuacha mara moja tabia hiyo kwani kwa kufanya hivyo hatua Kali za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kufikishwa mahakamani".Amesema Makonda.

Amesema watu wakihamia na kujenga maeneo ya shule watoto wao watasomea wapi hivyo tujiulize  kuvamia maeneo ya shule na kujenga ni kosa na wanaofanya hivi wachukuliwe hatua na kufikishwa mahakamani kwa yeyote atakaye uza au kununua maeneo hayo.
Aidha amesema wanaboresha mazingira ya kazi kwa walimu ikiwa ni kuendelea kusupoti kauli ya Rais Magufuli ya Mpango wa Elimu bure bila malipo wameamua kuboresha mazingira ya kazi kwa Walimu katika Mkoa huo kwa kujenga ofisi zipatazo 402,ambapo Leo Amezindu uzwkaji Paa katika ofisi hizo katika shule hiyo manispaa ya Kinondoni.

"Lazima mpishi awe anapika vizuri ili walaji waweze kula ivyo tunaboresha mazingira ya walimu wetu ili waweze kufanya kazi kwa uledi na ufanisi mkubwa ili watoto wetu waweze kufaulu vyema"Amesema

Kwa  upande Meya wa Mnispaa ya Kinondoni Mhe.Benjamani  Sitta memshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuangalia suala la Ofisi pamoja na nyumba za kwa Mkoa huo kwani ilikuwa ni changamoto kubwa sana kwa walimu walikuwa hawana ofisi kitendo kinachopelekea walimu kukaa chini ya miti na kufanya kazi zao.




VIDEO: Makonda Ampigia Debe Mtulia


Mkuu wa Wa Mkoa wa Dra es salaam Paul Makonda amewataka Wananchi katika jimbo la Kinondoni kuamchagua mgombea ambae atatekeleza ahadi na kero zao, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa anazindua uezekaji paa wa Ofisi za Walimu katika shule ya Msingi Mapinduzi iliyopo katika manispaa ya Kinondoni.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Breaking News: Tido Mhando afikishwa kizimbani Leo


ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa  Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Tido Mhando amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar leo kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka wakati akiwa TBC.


Mourinho aongeza Mkataba Man U


Kocha Jose Mourinho sasa ataifundisha Manchester United hadi mwaka 2020.

Mourinho raia wa Ureno ameongeza mkataba huo wa miaka mitatu kwa mwaka mmoja zaidi.
Pamoja na kwamba mashabiki wamekuwa wana hofu huenda ataondoka lakini uongozi unaonekana kumuamini zaidi.

VIKOMBE ALIVYOBEBA AKIWA NA UNITED:

Community Shield (2016)
League Cup (2016-17)
Europa League (2016-17)

Huu ndio ujumbe wa Mh.Lema kwa Jaji Mkuu wa Tanzania


Baada ya Jaji Mkuu wa Tanzania,Prof. Ibrahim Juma kuwataka wanasiasa na viongozi wa serikali wenye mamlaka ya kikatiba na sheria kutoingia utendaji wa Mahakama na kuheshimu Muhimili huo. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema Mahakama ambayo ni imara katika haki inawezaje kukubali kuingiliwa?.

Lema amemwambia Jaji Mkuu huyo kuwa Mahakama inapaswa kujitazama zaidi huku akimueleza kuwa Mahakama ikiyumba taifa limeyumba pia.

“Mh Jaji Mkuu kauli kuhusu wanasiasa na Watendaji wa Serikali kutokuingilia Mahakama ni kauli muhimu kwa wkt huu, lakini Mahakama ambayo ni imara ktk haki inawezaje kukubali kuingiliwa ?Mahakama inapaswa kujitazama zaidi.Mahakama ikiyumba Taifa linayumba,” ameandika Lema kwenye mitandao yake ya kijamii.

Jaji Ibrahimu alisema hayo, January 23 mwaka huu jijini Dar es salaam, wakati akifafanua siku ya maadhimisho ya siku ya sheria nchini yatakayoadhimishwa Februali Mosi Mwaka huu.

Nelly atetewa na Mpenziwe kuhusu kesi ya ubakaji

Msanii wa muziki nchini Marekani Nelly, huwenda akapona katika sakata linalomkabili la kumfanyia unyanyasaji wa kingono binti mmoja wakatiwa tour yake mwaka 2017.

Mpenzi wa msanii huyo Shantel Jackson, ameeleza kuwa mwanadada anayedai kubakwa na rapper huyo sio kweli kwani hata yeye alikuwepo katika eneo la tukio hilo ila alikuwa chumba cha kubadilishia nguo.

“Ni kweli mimi na Nelly tulikoseana ila hawezi kufanya tendo la ubakaji,” ameeleza mrembo huyo.

Monique Greene  ndiyo  mrembo anayedai kufanyiwa ubakaji na rapper huyo katika gari  la Tamasha maeno ya Washington, na sasa wanawake wengine wawili wameibuka na kudai kufanyiwa kitendo kama hicho na msanii huyo.

Maelezo ya mpenzi wa Nelly, Shantel Jackson:

Wanaume watatu waliokunywa dawa za kuongeza nguvu za kiume walazwa hospitali



Wanaume watatu waliokunywa dawa za kuongeza nguvu za kiume huko nchini Zambia  wamejikuta wakilazwa hospitali baada ya kuanza kutapika nakuharisha mfululizo baada ya kutumia dawa hizo.

Vyombo vya habari nchini Zambia vimeeleza kuwa wanaume hao walilazwa kwa makosa kwenye vituo vya zahanati za kuhudumia wagonjwa wa kipindu pindu wakidhaniwa kuwa wanaugua kipindu pindu hadi baadaye walipokuja kukiri kuwa walikunywa dawa za kuongeza nguvu za kiume na ndio zimepelekea waharishe na kutapika.

Kwa mujibu wa mtandao wa The Mast Online wa nchini humo umeeleza kuwa wanaume hao walikuja kubainika kuwa hawaugui kipindupindu wakati Kiongozi Mkuu wa Jimbo la Mashariki nchini Zambia, Chanda Kasolo alipotembelea kujua idadi ya wagonjwa juzi (Jumatano) katika Hospitali ya Katete jimboni humo..

“Mpaka kufikia jana kulikuwa na kesi mbili za wagojwa waliolazwa kutoka Lusaka, hivyo idadi ya wagonjwa imeongeka kutoka 24 hadi 26 jambo ambalo limeongeza hofu kwenye jamii yetu. Na kingine cha kushangaza jana tumepata wagonjwa wengine watatu kutoka Katete eneo ambalo halijawahi kupatwa kabisa na kipindu pindu lakini baada ya  uchunguzi wa madaktari tumebaini kuwa Wagonjwa hao hawakuwa wanaugua Kipindu Pindu,“amesema Kasolo na kuelezea kilichowakumba.

“Baada ya majibu ya vipimo kupatikana , inaonekana kuwa wanaume hao walikutwa na mchanganyiko wa pombe, vyakula na dawa za kienyeji ambazo zilisababisha mchafuko wa mfumo wa chakula na hivyo ikahusishwa na kipindupindu lakini baada ya kuwauliza maswali, baadaye walikiri kuwa walikunywa dawa ya kuongeza nguvu,”amesema Kasolo.

Hata hivyo tayari wanaume hao wamehamishwa kwenye hospitali hiyo inayolaza wagongonjwa wa kipindu pindu na kulazwa kwenye hospitali ya kawaida.

Mpaka sasa vifo vya watu wapatao 70 vimeripotiwa kutokea tangu mwaka jana kwa kesi za ugonjwa wa kipindu pindu .

Mwishoni mwa mwaka jana Rais wa Zambia, Edgar Lungu alitangaza kuwa ugonjwa huo ni janga la taifa huku akitaka kila mwananchi kuwajibika kwa usafi.

Nabii Tito ajikata na wembe tumboni


Nabii Tito ameibua mengine baada ya kujijeruhi kwa kujikata na wembe tumboni ambapo kumepelekea ashonwe nyuzi 25 katika zahanati ya polisi Dodoma.

Daktari wa hospitali hiyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na ameeleza kuwa Tito alifikishwa hospitali saa 9 mchana akiwa anavuja damu eneo la tumbo.

”Ni kweli Tito alifikishwa hapa majira ya saa 9 mchana, tulimfanyia matibabu kwa kumshona nyuzi 25 kutokana na ukubwa wa majeraha hayo” amesema Daktari.

Hata hivyo kamanda wa polisi Dodoma, Gilles Muroto hana taarifa kutokea kwa tukio hilo.

Nabii Tito sasa anashikiliwa na polisi kutokana na kauli zake zinazopingana na dini, amekuwa akihamasisha watu kunywa pombe, na wanaume kulala na wadada wa kazi akidai kuwa kufanya hivyo sio dhambi.

Hivyo baada ya matibabu hayo nabii Tito alirudishwa polisi kwa mahojianao zaidi.

Nafasi za kazi leo Jan 26

Bill Gates ampa onyo Trump kuhusu Afrika



Tajiri na Mfanyabiashara mkubwa duniani, Bill Gates amemuonya rais wa Marekani Donald Trump kwa misimamo ya sera yake ya “Marekani Kwanza” kuwa inaweza kuharibu uhusiano wa nchi hiyo na bara la Afrika.

Ameyasema hayo katika mkutano wa dunia wa uchumi World Economic Forum (WEF) unaofanyika huko Davos nchini Switzerland ambapo amesema kuwa kunatakiwa kuwepo kwa uwiano wa wenye nguvu kubwa na nguvu kidogo.

Amesema kuwa Marekani inaweza kupoteza ushawishi wake barani Afrika huku nchi kama China zinazidi kuimarisha uhusiano na bara hilo kwa kuwekeza katika sekta mbalimbali.

Bill Gates anamfuko wake barani Afrika unaoitwa Bill & Melinda Gates Foundation, ambao umekuwa ukijihusisha kwa kiasi kikubwa kutoa huduma za afya katika nchi kadhaa.

Hata hivyo, Rais Trump amesema kuwa atakata msaada wa bajeti ya afya kwa takribani dola bilioni 2.2 katika mfuko wa dunia, huku akiwakasirisha viongozi wa Afrika bada ya kuyaita mataifa ya Afrika machafu kupindukia.

Gwajima azuia watu kulia kwenye msiba wa Mama yake


ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dk. Josephat Gwajima ameacha gumzo na mshangao baada ya kuzuia watu kulia kwenye ibada ya kuaga mama yake mzazi, Bi. Ruth Paulo Gwajima iliyofanyika nyumbani kwa mchungaji huyo na kisha mwili wa marehemu kuzikwa kwenye shamba la familia, nje kidogo na nyumbani hapo, Salasala jijini Dar.