Saturday, 21 October 2017

VIDEO : Mwana FA Ft Ay & Fid Q _ Upo Hapo | Mp4 Download

https://cloudup.com/files/iKBl1xkibP8/download

AUDIO | Mwana FA Ft AY & Fid Q – Upo Hapo | Mp3 Download

AUDIO | Mwana FA Ft AY & Fid Q – Upo Hapo | Mp3 Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/283095/by/rsNQEQDqxY

Wanafunzi watishia kuchoma shule Geita

Geita. Vurugu kubwa zimeibuka katika Shule ya Sekondari Geita baada ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita kutishia kuchoma shule kushinikiza wenzao wanne wanaoshikiliwa na polisi waachiwe.
Polisi Geita inawashikilia wanafunzi wanne wa shule hiyo tangu Alhamisi baada ya kumpiga, kumjeruhi na kutishia kumuua mwenzao wa kidato cha tano.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Isaya Busagwe amesema mwanafunzi huyo alipigwa Jumamosi iliyopita na walimu waligundua tukio hilo baada ya aliyepigwa kuugua na kuomba ruhusa ya kwenda nyumbani kutibiwa.
Jana Ijumaa Oktoba 20, wanafunzi hao waligoma kuingia darsani, badala yake, waliandamana kwenda kituo cha polisi kushinikiza wenzao kuachiwa huru.
Baada ya juhudi zao kugonga mwamba kwa polisi kuendelea kuwashikilia wenzao, wanafunzi hao walirejea shuleni na kuanza kurusha mawe wakitishia kuchoma moto majengo wakishinikiza wajumbe wa bodi waliokua wakiendelea na kikao shuleni hapo kutatua suala hilo.
Leo Jumamosi asubuhi, wanafunzi hao walianzisha vurugu zingine, hali iliyolazimisha jeshi la polisi kuingilia kati na kufanikiwa kuzidhibiti.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita(OCD), Ally Kitumbo aliyeongoza kikosi cha kutuliza ghasia kudhibiti vurugu hizo hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo akisema yeye siyo msemaji na kazi yake ni kulinda amani na utulivu.
Katika vurugu hizo mwandishi wa habari hii naye amejikuta akiwekwa chini ya ulinzi na kunyang'anywa simu na askari polisi kabla ya kunusuriwa na OCD na kuruhusiwa kuendelea na kazi.

Friday, 20 October 2017

AUDIO | Come Dash _ Haitowezekana | Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/283017/by/vJHK6UaW3X

Breaking News: Matokeo ya darasa la saba yatangazwa


Bonyeza link hapo chini kuanaglia matokeo ya Darasa La Saba mwaka 2017

http://www.necta.go.tz/matokeo/2017/psle/psle.htm

Juma Nature Awafungukia Wasanii Wachanga

Msanii Juma Nature ambaye ni mkongwe kwenye game ya bongo fleva, amewataka wasanii wachanga kufuata sheria pale wanapotaka kutumia nyimbo za wasanii wakongwe jukwaani, ikiwemo kuomba kibali kwa muhusika na ikiwezekana amlipe fedha
Juma Nature ameyasema hayo alipokuwa akiongea na mwandishi wa East Africa Radio, na kueleza kwamba msanii mchanga kuimba nyimbo za msanii mkongwe jukwaani sio jambo baya na inaonyesha heshima, lakini ni vyema wakawa na makubalino maalum kabla hajafanya hivyo kuepusha migogoro.

Askofu Afariki Akiwa Safarini

Dar es Salaam. Jimbo Katoliki la Tunduru Masasi limempoteza askofu wake, Castory Msemwa aliyefariki jana Alhamisi Oktoba 19,2017 saa saba mchana nchini Oman.
Kwa mujibu wa Makamu wa Askofu wa Jimbo Katoliki Tunduru Masasi, Padri Jordan Liviga, Askofu Msemwa amefariki dunia mjini Muscat akiwa safarini kwenda nchini India kwa matibabu.
Taarifa ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) imesema Askofu Msemwa alikuwa na tatizo la kiafya kwa kipindi cha miaka miwili na amekuwa akipata tiba na kuendelea na utume kama kawaida.
TEC imesema Askofu Msemwa aliondoka nchini Jumatano Oktoba 18,2017 kuelekea nchini India kwa matibabu kabla hajafariki dunia.
Padri Liviga amebainisha kuwa utaratibu wa kuuleta nchini mwili wa marehemu Askofu Msemwa Jumapili Oktoba 22,2017 unafanyika. Amesema taarifa zaidi za utaratibu wa mazishi zitatolewa baadaye.
Askofu Msemwa amezaliwa mwaka 1955 katika Kijiji cha Kitulira, Parokia ya Matola Jimbo Katoliki Njombe.
Alipata elimu ya msingi katika shule ya Motola, kisha sekondari katika Seminari Kuu ya Peramiho ambako alisomea Falsafa na Teolojia kati ya mwaka 1981 na 1987. Alipata daraja ya upadri Juni 7,1987. Amekuwa Paroko Msaidizi, kiongozi wa vijana parokiani jimboni Njombe, mwalimu na amesoma katika Chuo cha Teresianum Pontifical College for Spirituality huko Roma na kuhitimu mwaka 1996.
Alipata Daraja ya Uaskofu Januari 30,2005 kisha kusimikwa kuliongoza Jimbo Katoliki Tunduru Masasi Agosti 25,2005.

Nassari ashangaa kuwaona viongozi ofisini


Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amesema kuwa bado anashangaa kuendelea kuwaona ofisini viongozi ambao aliowataja kwenye ushahidi wa kutumia rushwa kununua madiwani wa Chadema mkoani Arusha kwani watakuwa na nafasi kubwa ya kuharibu ushahidi huo. Mh. Nassari amesema kwamba hofu yake kwa viongozi hao ni kwamba watakuwa na nafasi kubwa ya kuuharibu ushahidi huo kwa kuwa bado wamekalia madaraka hivyo wanaweza kufanya lolote kuhakikisha ushahidi ulioneshwa unaharibika ikiwa ni pamoja na upelelezi kufanyika kwa mashaka. "Kinachonishikisha ni kuendelea kuwaona viongozi wale bado wapo ofisini. Huko nyuma tumeona watu wakiwajibika kisiasa pale wanapopata tuhuma kuhusu rushwa, huwa wanawajibika au kuwajibshwa. Hapa naona inakuwa ngumu kidogo kuhusu upelelezi wa kesi hii kufanyika . Mfano tunaona sehemu kwenye video Mkurugenzi anasikika akieleza ni namna gani ataelekeza wale madiwani waanze kulipwa kidogo kidogo lakini bado yupo ofisini hii inanisikitisha kwani upelelezi unakuwa na mashaka kidogo" Nassari Aidha Nassari amesema ameshangazwa na kauli ya Mkurugenzi wa Takukuru, Valentino Mlowola kwamba yeye anaingilia upelelezi wao na kudai kwamba anachoamini yeye ni kwamba hajavunja sheria wala hajaingilia upelelezi wao kwani anachokifanya ni kuutaarifu umma kila hatua anayokua anaifanya. Nassari ameongeza kwamba kauli zinazotolewa na Mlowola kama zina lengo la kumtia hofu basi kwake hofu hiyo anaamini haitafanya kazi kwake kwani kama ni kuzungumza na wanahabari wakati akiwa anapeleka ushahidi hataacha kwani huwa hazungumzii ushahidi alioubeba bali huwa anazungumzia hatua anazopiga. Pamoja na hayo Nassari amesema hawezi kuzungumza kama haki itapatikana au la bali anachoamini Takukuru ni taasisi inayojitegemea hivyo hawataona haya kutenda haki ili ijulikane wateule wa rais wana hatia au vinginevyo.

Mexime asema Kagera Sugar bado inatafuta ushindi

Kocha wa klabu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara Meck Mexime amesema timu yao bado inatafuta ushindi.
Meck ameyasema hayo leo kuelekea mchezo wa raundi ya 7 dhidi ya Mwadui FC utakaopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.
“Kikubwa sisi tunatafuta ushindi kwasababu hatujaupata tangu ligi ianze, hivyo tumejiandaa kutafuta ushindi na pointi tatu”, amesema Meck Mexime.
Mexime ambaye ni mchezaji na kocha wa zamani wa timu ya Mtibwa Sugar ameshindwa kuonesha makali ya msimu uliopita tangu ligi ya msimu wa 2017/18 ianze ambapo hajafanikiwa kupata ushindi kwenye mechi Sita za mwanzo.
Hadi sasa Kagera Sugar inaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 2. Wakata Miwa hao wa Kaitaba wamepoteza mechi 4 na kutoa sare mechi mbili. Wakati Mwadui wanashika nafasi ya 12 ikiwa na alama 6 baada ya michezo Sita.

Umoja wa Mataifa Umesitisha Shughuli Zake Zote Nchini Kenya Kuhofia Uchaguzi

Umoja wa Mataifa (UN) umesitisha shughuli zake zote nchini Kenya katika kipindi cha kuelekea uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26.
Taarifa iliyotolewa Ijumaa na Msaidizi wa Katibu mkuu kanda ya Afrika Mashariki, Peter Drennan imesema umoja huo utasitisha kwa muda programu zake zote ambazo hazikuwa muhimu sana.
“Baada ya kufanya tathmini ya hali ya usalama nchini Kenya, ofisa mteule (DO) kwa ushauri kutoka Timu ya Usimamizi wa Usalama, ameshauri kusitishwa kwa warsha, mikutano, semina na makongamano na jumbe mbalimbali zisizo za lazima nchini Kenya walau kwa wiki moja kabla na wiki moja baada ya uchaguzi wa marudio kwa kura ya urais,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
“Ninakubaliana na ushauri wa DO na mamlaka husika kusitishwa kwa programu hizo ambazo hazina ulazima kuanzia leo Oktoba 19 hadi Novemba 2.”
Jana Alhamisi serikali ilitangaza kwamba Alhamisi ya Oktoba 26 itakuwa siku ya mapumziko kwa ajili ya kuruhusu wananchi kushiriki uchaguzi wa marudio.
Kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani, Fred Matiang’i alitangaza kwamba siku hiyo imeandikwa katika Gazeti la Serikali kwamba itakuwa siku ya mapumziko kuwezesha Wakenya kushiriki kwa uhuru uchaguzi huo.
Tangazo hilo limekuja katikati ya mnyukano wa kisiasa na kuiweka uchaguzi huo katika hatihati ya kufanyika.
Jumatano, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati alielezea kukerwa kwake katika maandalizi ya uchaguzi wa marudio na akatangaza wazi kuwa hawezi kuhakikisha uchaguzi wa kuaminika.
Chekubati alisema kutokana na kupanda sana kwa hofu ya kisiasa nchini, alipendekeza Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wakutane kwa mazungumzo kabla ya uchaguzi huo

BAD NEWS ! Ajali ya Hiace na lori Yaua Watu watano

Muleba. Watu watano wamefariki dunia baada ya gari aina ya Toyota Hiace kugongana na lori kisha kuwaka moto.
Ajali hiyo imetokea katika Kijiji cha Kyamyorwa wilayani Muleba mkoani Kagera.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Olomi amesema ajali hiyo imetokea leo Ijumaa Oktoba 20, saa 12:00 asubuhi.
Amesema mwendo kasi wa dereva wa gari dogo la abiria ni chanzo cha ajali hiyo.
Ingawa Kamanda Olomi hakuwataja waliokufa, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Richard Ruyango amesema miongoni mwao ni dereva wa gari dogo, kondakta na abiria watatu.
Amesema watu hao walishindwa kujiokoa kutokana na mlango wa gari kubanwa hivyo kushindwa kufunguka.

UN yatoa Dola160 milioni nchini

Mratibu mkazi wa UN, Alvaro Rodriguez
Dar es Salaam. Umoja wa Mataifa (UN) umetoa Dola 160 milioni za Marekani kati ya Dola 200 milioni zinazitakiwa kutolewa mwaka huu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwamo kuwahudumia wakimbizi waliopo kambi mbalimbali Kigoma.
Nusu ya fedha hizo zimeelekezwa kwenye mradi wa Kigoma wa kuwahudumia wakimbizi na kiasi kingine kimeelekezwa kwenye miradi mingine ya maendeleo inayofadhiliwa na mashirika mbalimbali ya UN.
Oktoba 24, UN itaadhimisha miaka 72 tangu kuanzishwa kwake na sherehe za maadhimisho hayo kitaifa zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wageni zaidi ya 500 wakiwamo na mabalozi, wanafunzi na vyombo vya ulinzi na usalama.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ‘Maendeleo ya Viwanda na Utunzaji Mazingira kwa Maendeleo Endelevu.’
Akizungumzia maadhimisho hayo jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kimataifa na kikanda, Dk Susan Kolimba alisema wameamua kuunganisha kauli mbiu ya Serikali ya kuendeleza viwanda na mpango wa UN wa kutekeleza Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
Mratibu mkazi wa UN, Alvaro Rodriguez alisema programu ya Kigoma imebuniwa ili kukidhi vipaumbele vya maendeleo ya mkoa huo na hasa kuzilenga jamii katika wilaya za Kasulu, Kibondo na Kakonko.

Yanga yaipiga mkwala stand UTD

KOCHA MSAIDIZI WA KLABU YA YANGA, SHADRACK NSAJIGWA.
KOCHA msaidizi wa klabu ya Yanga, Shadrack Nsajigwa, amesema maandalizi waliyoyafanya kuelekea mchezo wao dhidi ya Stand United ni ya kiwango cha juu na wenyeji hao wasitegemee urahisi.
Yanga itashuka kwenye Uwanja wa Kambarage, ulioko Shinyanga keshokutwa ili kusaka pointi nyingine muhimu za kutetea ubingwa wanaoushikilia.
Akizungumza na gazeti hili jana kutoka Tabora walipokuwa wameweka kambi ya muda kujiandaa na mchezo huo, Nsajigwa, alisema kuwa, wamejiandaa vizuri na mchezo wao wa kirafiki waliocheza juzi dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora umewaongezea nguvu.
“Tulijiwekea mikakati katika michezo miwili ule wa Bukoba na huu tunaokwenda kucheza Shinyanga, tuondoke na pointi zote sita, tumefanikiwa mchezo wa kwanza, tunaenda Shinyanga kukamilisha kile tulichokianza Bukoba,” alisema Nsajigwa.
Aliongeza kuwa wanajua watakutana na ushindani kutoka kwa wenyeji wao, ambao watataka kutumia vyema uwanja wa nyumbani, lakini wamejipanga kuondoka na ushindi.
Kuhusu wachezaji watakaoanza kwenye mchezo huo hasa kuepuka wale wenye kadi mbili za njano ambao wanaweza wakapelekea kuukosa mchezo dhidi ya Simba, Nsajigwa alisema suala lipo chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina.
“Tuna siku ya leo (jana) kesho (leo) na Jumamosi kuangalia nani ataanza kwenye mchezo wa Shinyanga, tunafahamu tunatakiwa kuwa na tahadhari, si tu kwa kadi lakini pia kuepuka wachezaji wetu wasiumie kwa sababu ya mchezo wa Oktoba 28, hilo suala linafanyiwa kazi,” alisema Nsajigwa.
Wachezaji wa Yanga ambao wana kadi mbili za njano na wako katika hatari ya kuikosa Simba kama wataonyeshwa kadi yoyote Jumapili ni Kelvin Yondani na Juma Abdul.

Uongozi wa Trump wakosolewa na Marais hawa

Marais wa zamani George Bush na Barrack Obama
Marais wawili wa zamani nchini Marekani wameonyesha wasiwasi wao kuhusu hali ya kisiasa nchini humo bila kumtaja rais Donald Trump kwa jina.
Barrack Obama aliwataka wapiga kura kukataa kile alichokitaja kuwa siasa za kuwagawanya watu mbali na siasa za hofu.
Alikuwa akimfanyia kampeni mgombea wa chama cha Democrat anayewania wadhfa wa gavana wa jimbo la New Jersey.
Matamshi yake yanajiri saa chache baada ya mtangulizi wake George W. Bush kukosoa unyanyasaji na chuki katika maisha ya kawaida ya raia Marekani.
Katika hotuba, alisema chuki dhidi ya wale wanaokupinga zimeongezwa nguvu huku maadili ya kiraia yakisahaulika.
Bwana Trump ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa mtangulizi wake bado hajatoa tamko lolote.
Marais wa zamani nchini Marekani kwa kawaida huwa nadra kutoa maoni yao kuhusu hali ya kisiasa na ilionekana kuwa makosa makubwa kwa rais aliyetangulia kumkosoa mrithi wake katika ikulu ya Whitehouse.
lakini maadili na viwango vya tabia ambazo awali zilikuwa zikifuatwa sasa zimesahaulika katika mazingira ya kisiasa ya wakati huu.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni za chama cha Democrat , mjini New Jersy, Obama alisema kuwa Wamarekani wanapaswa kutuma ujumbe kwa ulimwengu kwamba tunakataa siasa za kugawanywa na siasa za hofu.
Aliongezea: Kile ambacho hatufai kuendelea nacho ni kuwa na siasa za zamani za kugawanyana ambazo zimekuwepo nyakati za wali.
Siasa tunazoziona sasa tulidhani zimepitwa na wakati, hiyo ni kurudi miaka 50 nyuma.Ni karne ya 21 sio 19. jamani!.

Korea Kaskazini yaionya Australia

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Serikali ya Australia imesema kuwa imepokea stakhabadhi kutoka Korea Kaskazini ikiitaka Canbera kutojihusisha na utawala wa rais Trump.
Barua hiyo imeshutumu onyo la Marekani kwamba itaiangamiza Korea Kaskazini iwapo italazimika kujilinda.
Waziri mkuu wa Australia PM Malcolm Turnbull amesema kuwa barua hiyo pia ilitumwa kwa mataifa mengine.
Amesema inaonyesha kuwa shinikizo za kidiplomasia dhidi ya Korea Kaskzini zimeanza kufanya kazi, licha ya barua hiyo kuwa na ufyozi na malalamishi ya kawaida ya taifa hilo.
Barua hiyo yenye ukurasa mmoja ilitumwa kupitia ubalozi wa Korea Kaskazini nchini Indonesia na inadaiwa kutoka kwa kamati ya maswala ya kigeni ya Korea Kaskazini.
Imezitaka serikali nyengine kujitenga na hatua zisizokuwa na heshima za rais Trump ikisisitiza kuwa Marekani inaweza kusababisha janga kubwa la kinyuklia.
Bwana Turnbull amesema kuwa Korea Kaskazini ndio inayosababisha wasiwasi kwa kutishia kuyashambulia mataifa ya Japan, Korea Kusini na Marekani kwa kutumia silaha za kinyuklia.
''Wametuma barua hizi kwa mataifa mengi , kama barua iliosambazwa'', alisema Bwana Turnbull kwa kituo kimoja cha redio 3AW.
Waziri wa maswala ya kigeni Julie Bishop aliitaja barua hiyo kuwa hatua isiokuwa ya kawaida ya Korea Kaskazini.
Baadaye bwana Turnbull alionekana kutojali umuhimu wake akiifananisha na ufyozi na malalamishi kuhusu Donald Trump unaotolewa na Korea Kaskazini.
Hatahivyo wote wanakubaliana kwamba huenda ni ishara kwamba shinikizo za kimataifa dhidi ya taifa hilo zimeanza kuzaa matunda na kuwa na matumaini kwamba kutakuwa na majadiliana ya kimataifa.
Siku ya Jumamosi Pyonyang iliionya Australia kwamba haitaweza kuzuia janga iwapo itashirikiana na sera za Marekani dhidi ya utawala wa Kim Jong Un.
Korea Kaskazini imekiuka makubaliano ya kimataifa katika miezi ya hivi karibuni kupitia kufanyia majaribio kombora lake la kinyuklia mbali na kurusha makombora mawili juu ya anga ya taifa la Japan.
Marekani imejibu kwa vitisho vya kijeshi , lakini waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani Rex Tillerson anasisitiza kuwa bwana Trump yuko tayari kuutatua mgogoro huo kupitia diplomasia.

Chris Brown kurudiana na Rihanna?

Mkali wa Muziki wa Pop, Christopher Maurice ‘Chris Brown’ akiwa na Rihanna.
TAARIFA kutoka chini ya kapeti zinaeleza kuwa, miezi michache baada ya kutengeneza filamu fupi ya maisha yake, mkali wa Muziki wa Pop, Christopher Maurice ‘Chris Brown’ huenda akarudiana na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Rihanna.
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na Chris, baada ya filamu hiyo kutoka inayoitwa Welcome To My Life, Chris anaamini kwa asilimia kubwa Rihanna ameiona yote na atakuwa tayari kurudiana naye. “Chris anaamini Rihanna ameshamsamehe baada ya kuangalia filamu.
Chris alishawahi kumwambia rafiki yake anataka kuwa anamchukua Rihanna na kwenda naye kwenye filamu,” kilisema chanzo.

Moto wateketeza Hoteli ya Kifahari

Moto mkubwa imeteketeza hoteli kubwa ya kifahari katika mji wa Yangon nchini Myanmar na kumuua mtu mmoja.
Watu wengine walijeruhiwa kwenye moto huo ambao ulianza mwendo wa saa 20:30 GMT siku ya Jumatano katika hoteli ya Kandawgyi Palace.
Iliwachukua mamia ya wazima moto saa kadha kuuzima moto huo. Zaidi ya wageni 140 waliondolewa.
Haijuliana moto huo ulinza kwa njia gani huku ripoti za kukanganya zikisema kuwa kulikuwa na mlipuko wa mtungi wa gesi au hutilafu ya umeme.
"Hakukuwa na king'ora na vurugu zilikuwa ni kama kulikuwa na walevi hotelini," mtalii mmoja alisema, akiongeza kuwa ni mfanyakazi mmoja ambaye alimuelekzea eneo salama.
Wageni wamehamishwa kweda kwa hoteli zingine mjiji Yangon.
Hoteli hiyo ili kando ya ziwa Kandawgyi, ilijengwa miaka ya 1990 lakini huenda uwepo wake uliazia miaka ya 1930 wakati eneo hilo lilikuwa likitumia kama klabu ya wanajeshi wa Uingereza.
Hoteli ya kifahari kabla ya kuteket

AUDIO | Timmy Tdat Ft Dela _ We'll Be Ok | Download

AUDIO | Timmy Tdat Ft Dela – We’ll Be OK | Mp3 Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/282765/by/DM19joF3B~

VIDEO : Harmonize _ Nishachoka | Download

https://cloudup.com/files/iuRG9ODfNAv/download

Thursday, 19 October 2017

Nyalandu Akomalia katiba

Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM) amefunguka na kusema katika kikao cha Tisa cha Bunge kinachotarajiwa kuanza Novemba 7, 2017 Dodoma anakusudia kuwasilisha azma yake ya kupeleka muswada binafsi utakao weka sharti la kurejea mjadala wa Katiba Mpya.
Nyalandu amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya kijamii na kusema amekusudia kufikisha jambo hilo mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai.
"Nakusudia kuwasilisha kwa spika wa Bunge Mh. Job Ndugai. Azma yangu ya kuleta muswada binafsi wa sheria katika kikao kijacho cha Bunge itakayoweka sharti la kurejea upya mjadala wa Katiba Mpya ya Tanzania, kwa kuzingatia rasimu ya Katiba kama ilivyowasilishwa na Tume ya Jaji Warioba" alisema Lazaro Nyalandu
Suala la Katiba Mpya licha ya kuwa siyo kipaumbele cha Rais John Pombe Magufuli lakini wadau mbalimbali wamekuwa wakilizungumzia wakisema kuna haja kubwa ya mchakato huo wa Katiba mpya kuendelea sasa wakidai kuwa huu ni wakati sahihi zaidi mchakato wa Katiba Mpya kuendele

Chadema yajilipua kuhusu lowassa

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu amefunguka na kusema kwamba wanawaruhusu Chama cha Mapinduzi watumie nafasi ya Lowassa kuwepo Chadema kuwaita wao mafisadi kama jinsi wao walivyofanya kwa miaka mingi.
Salumu amesema kwamba kuwataja watu ambao waliwaita vinara wa ufisadi na leo wapo nao kwenye chama chao ulikuwa ni wajibu wao kama chama cha upinzani kutumia upenyo wa udhaidfu wa chama cha mapinduzi kuonyesha wananchi madhaifu ya serikali.
"Lazima ukubali kwamba ni wajibu wetu kuonyesha madhaifu ya serikali, Kama tulikuwa tunampinga Lowassa kwamba ni fisadi ulikuwa ni wajibu wetu Chadema. Sasa kama leo hii Lowassa yupo kwetu ni wajibu wao CCM kuwaambia watanzania kuwa Chadema kina mafisadi. Kwa sababu Lowassa amekuja Chadema ni yule yule wala hajawa malaika kama jinsi ambavyo kelele zinavyopigwa," Mwalimu amefunguka
Akizungumzia kuhusu chama kupwaya na kumtegemea mtu mmoja kuwa mkosoaji wa serikali iliyopo Madarakani, Mwalimu amesema kupanga ni kuchagua hivyo wao kama Chadema wanauwezo mkubwa wa kukosoa lakini huamua kuchagua nani atoe hoja kwa wakati gani na siyo kwamba wameishiwa.
"Hata kwenye timu ya mpira wapo mastaa wengi wanaofanya vizuri lakini huangaliwa ni nani wa kuibeba timu, ndivyo hata Chadema ilivyo, mnaweza kuwa wengi lakini kupanga ni kuchagua, Tundu ni Mwanasheria Mkuu wa chama hivyo chama kinaanda ajenda lakini atachaguliiwa mmoja wa kuifikisha ajenda hiyo huku wengine tukitoa sapoti, inategemea ajenda hiyo pia inatolewa wakati gani, mbona hapa katikati mengine yametokea kwani tumemuinua Lissu kitandani atusaidie kusema. si tulisema wenyewe. ? hivyo hakuna mtu mmoja anayeibeba Chadema bali tunashirikiana pamoja", Mwalimu ameoneza.
Huu ni utaratibu wetu hata kipindi cha kina Mh. Zitto Kabwe pamoja na Dkt. Slaa wote agenda zilikuwa ikitengenezwa na watu ndani ya chama na wanaozipeleka mbele huwa ni wachache siyo kwamba eti chama kimepwaya.
Katika hatua nyingine Mwalimu amesema lengo la chama cha upinzani ni kushika dola na siyo kusikiliza jinsi ambavyo watu wengine wanavyokosoa na kusisitiza kwamba Chama chao kilianzishwa kwa malengo ya kuja kushika dola.

Wema Sepetu na wasanii wengine wamfaliji Lulu

Dar es Salaam . Msanii wa fani ya uigizaji filamu nchini, Wema Sepetu ni miongoni mwa watu waliomfariji Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayekabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia iliyoanza kusikilizwa leo katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Wasanii wametumia mtandao wa Instagram kumfariji mwigizaji Lulu ambaye ni mshindi wa tuzo za filamu za AMVCA.
Jackline Wopler, Katarina Karatu, Nisha, Aunt Ezekiel na wengine wametuma picha za mwigizaji huyo zikiambatana na maneno ya kumfariji wakimweleza kuwa atavuka salama katika mtihani huo.
Kupitia ukura wake wa Instagram, Wema ameweka picha ya Lulu na kuandika, “This Too Shall Pass Baby… God is Great u know… so have faith… ur in my prayers,” akiwa na maana hata hili litapita, Mungu ni mkubwa hivyo anatakiwa kuwa na imani na atamwombea.
Lulu anadaiwa Aprili 7,2012 alimuua bila ya kukusudia mwigizaji mwenzake Steven Kanumba, eneo la Sinza Vatican jijini Dar es Salaam. Kesi inasikilizwa na Jaji Sam Rumanyika.

Harmonize afurahia support anayopata toka kwa Wolper

Msanii wa Bongo Flava kutoka label ya WCB, Harmonize amefunguka mambo kadhaa kuhusu aliyekuwa mpenzi wake, Jacqueline Wolper.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Shulala’ ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa anafurahi kuona anapata support ya Wolper katika muziki wake.
“Nadhani mwanzo ilikuwa hasira tu, nashukuru kuona support ya Wolper, namchukulia kama shabiki yangu tu” amesema Harmonize.
Hiyo juzi katika mtandao wa Instagram Jacqueline Wolper aliposti video mbili zikimuonyesha akifurahia kusikiliza ngoma hiyo ambayo Harmonize amemshirikisha Korede Bello.

Waziri kigwangalla atoa siku 7

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Hamisi Kigwangalla amefunguka na kuwapa siku saba wavamizi ambao wapo kwenye pori tengefu la Loliondo kuondoka mara moja ndani ya siku hizo kwani wasipofanya hivyo baada ya hapo mali zao zitataifishwa na serikali.
Kigwangalla amesema uwepo wa wavamizi hao ambao wana ng'ombe zaidi ya 6,000 na matrekta zaidi ya 200 kutoka nchi ya jirani imekuwa sababu kubwa ya chanzo cha mgogoro wa ardhi baina ya vijiji na hifadhi hiyo.
"Kuna taarifa kwenye eneo lenye mgogoro la Pori Tengefu la Loliondo, kuna ng'ombe zaidi ya 6,000 na trekta zaidi ya 200 toka nchi jirani, yote kinyume cha sheria! Uwepo wao siyo tu unahatarisha uhai wa mfumo wa ikolojia ya Serengeti-Mara, bali pia unapunguza eneo la kuchungia kwa wenyeji wa Loliondo. Hivyo kuleta kiu ya wananchi wa Loliondo kuingia ndani zaidi ya eneo la hifadhi kutafuta malisho na hatma yake kuhatarisha uhai wa Serengeti. Uvamizi huu wa wenzetu kutoka nchi jirani ni moja ya sababu kubwa (zilizojificha) za mgogoro wa ardhi baina ya vijijj na hifadhi kukolea moto" alisema Waziri Kigwangalla
Aidha Waziri huyo amesema wakati wanaendelea kutafuta ufumbuzi wa kudumu wamewataka wavamizi hao kuondoka katika maeneo hayo
"Wakati tukiendelea kutafuta suluhisho la kudumu, tutaondoa makando kando kama haya haraka. Leo tumetoa siku saba kwa wavamizi wote toka nchi jirani waliopo eneo la Loliondo bila kufuata taratibu za kisheria waondoke na mali zao la sivyo tutazitaifisha" alisisitiza Kigwangalla.

Wahamiaji Haramu 21 kutoka DRC wamekamatwa

JESHI la Polisi Mkoani Tabora linawashikilia wahamiaji haramu 21 raia wa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa tuhuma za kuingia nchini bila kufuata utaratibu. Taarifa hiyo imetolewa leo na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora (RPC) Wilbrod Mutafungwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari Ofisini kwake.
Alisema kuwa watuhumiwa hao wa uhamiaji haramu walikamatwa tarehe 17 mwezi huu wilayani Urambo baada ya Polisi kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema. Kamanda huyo wa Mkoa alisema kuwa baada ya wasamaria wema kutoa taarifa kwa Polisi ndipo waliweka mtego na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao ambao ni wa familia tano tofauti za kutoka DRC.
Alisema kuwa katika orodha hiyo wapo wanaume wawili, wanawake watano na watoto 14 ambao walikamatiwa Urambo baada ya kushuka katika gari la abiria la Saratoga linalofanya safari zake kutoka Kigoma hadi Tabora. Kamanda Mutafungwa aliongeza kuwa watuhumiwa hao walikuwa wakitatafuta usafiri wa kwenda Tabora mjini kutoka Urambo na ndipo Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata.
Alisema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kushirikiana na Uhamiaji na vyombo vingine kuwahoji sababu ya kuja nchini bila kufuata taratibu inagwa wao wanadai kuwa walikuja kutafuta Kambi ya Wakimbizi kufuatia machafuko yanayoendelea nchini mwao. Kamanda Mutafungwa alisema watuhumiwa kutoka familia ya kwanza ni Dieudonne Buloze (32), Kigwasa Mariya(20), Medianne Buloze(3) na Alber Buloze(1). Wengine ni Byamungu Mateus(38), Mulasi Nabunane(33), Busime Mateusi(13), Faida Mateusi(8), Mbamba Mateusi(6), Hadija Mateusi(3) ,Bereke Mateusi(2) na Lebinde Omary(60).
Aliwataja wengine walikamatwa kuwa ni Betie Kasongo(24) , Yoshuwa Ekombe(3) , Yosia Ekombe(miezi 10), Aline Chekanabo (28), Francoise Heva (9), Jistin Faiba (7) , Amida Faiba (6), Kikombe Sumaili(4) na Gulenne(miezi 10). Mmoja wa wahamiaji haramu hao Dieudonne Buloze alikiri kuwa walikimbia DRC kukimbia mapigano yanayoendelea , wakiwa wanatokea Kivu ambapo wavuka mpaka kupitia ziwa Tanganyika na kujikuta wako upande wa Tanzania.
Alisema wamekuja Tanzania kutafuta hifadhi ili kuokoa maisha yao kutokana na mapigano yanayoendelea baina ya vikosi vya Serikali na Waaasi. Katika hatua nyingine Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora alisema kuwa watoto wawili wa shule ya Ncheli katika Kata ya Sungwizi wilayani Simbo wamefariki dunia baada ya kutumbukia katika kisima kilikuwa hakina uzito.
Alisema kuwa chanzo cha vifo hivyo ni wakati mtoto wa kwanza Mwashi Yohana alipoteleza na kuanguka kisimani wakati akijaribu kutaka kunywa maji na ndipo wa pili ajulikanaye kama Wande Shija alifariki baada ya kutumbukia katika kisima wakati akijaribu kumwokoa mwezie.
Kufuatia vifo hivyo Kamanda Mutafungwa alitoa wito kwa wakazi wote Mkoani hapa kuweka uzio katika visima vyote walivyovichimba wakati wa kiangazi na kuhakikisha wazazi wanawasindikiza watoto wao wakati wa kwenda na kutoka shule hasa kwa wale wa shule za awali.

TANGAZO: FAMOUS FURNITURE, WASAMBAZAJI WA MAGODORO YA SEALY POSTURPEDIC NA MASOFA YA LA-Z-BOY WAFUNGUA DUKA DAR ES SALAAM

Famous Furniture, wasambazaji wa magodoro ya Sealy Posturpedic na masofa ya La-Z-Boy wafungua duka Dar es salaam, Tanzania.
Oktoba 18, 2017 Dar es salaam, Famous Furniture wamefungua duka lao Mlimani City, Dar es salaam , Tanzania kwa ajili ya wanaopenda kuishi maisha yasiyo na karaha. Famous Furniture watakuwa ni wasambazaji rasmi magodoro na vitanda vya Sealy Posturepedic pamoja na sofa na viti vya La-Z-Boy nchini.
Magodoro ya Sealy Posturepedic
Sealy ina uzoefu wa utengenezaji wa magodoro na vitanda kwa zaidi ya miaka 100, na kwa sasa ndiyo chapa inayoongoza kwa kutengeneza vitanda na magodoro bora kabisa duniani kote. Vitanda vya Sealy vimetengenezwa na wabobeaji wa afya ya mfupa ili kukupatia starehe, mfumo bora wa egemezi yote haya yakiwa kuhakikisha unapata usingizi mzuri na wenye afya.
Sealy wana vitanda na magodoro ya aina mbalimbali yanayokidhi mahitaji ya kiafya na starehe na yanayodumu kwa muda mrefu.
Zaidi ya watu milioni 40 duniani wanapata usingizi mzuri na kuamka wenye afya kwa sababu ya kutumia bidhaa za Sealy. Tunahakikisha usiku wako unakuwa wenye pumziko na amani. Usingizi mzuri hupoza mwili, unakupa nguvu, unahakikisha unakua vyema na afya nzuri huku akili yako ikizidi kujijenga vizuri. Kumbuka, unatumia theluthi ya maisha yako yote kwenye usingizi.
Leo hii, kuna bidhaa mbalimbali za Sealy unazoweza kuchagua lakini lengo letu ni moja; kuhakikisha tunakuwa sababu ya wewe kuwa na maisha yenye starehe.
Masofa na viti vya La-Z-Boy
Fenicha za La-Z-Boy zinatengenezwa na kusambazwa kwa leseni katika nchi nyingi duniani. La-Z-Boy ina haki miliki za US na kimataifa kwenye miundo zaidi ya 200. Dizaini ya kwanza ilitengenezwa mwaka 1928 na tangia hapo, wamekuwa ni mabalozi “maisha ya starehe” wanaoongoza duniani.
Kupumzika ni starehe
Binadamu hutumia muda mwingi wakiwa wamekaa chini, hii ndio ya sababu ya wabunifu, watafiti na wataalamu wa afya kuumiza vichwa kutoa bidhaa zitakazoleta starehe katika mikao. Unahitaji kukaa kwenye viti bora na vizuri vinavyokujenga kiafya. Ryan Beattie kutoka Bravo Group, wasambazaji wa La-Z-Boy kutoka Famous Furniture anasema “Starehe ya mkao sio katika muonekano t
u – baliile inayokupa starehe ya mwili na mfumo bora wa egemezi, hasa kama unakaa kwa muda mrefu”.
Kuhusu Famous Furniture Ltd
Famous Furniture Limited (iliyosajiliwa na namba 135127) iliona umuhimu wa kutambulisha bidhaa bora za nyumbani ili kukidhi soko linalokuwa la Tanzania. Bidhaa bora za La-Z-Boy zitaboresha mwonekano wa nyumba yako na starehe yako ya mkao wakati magodoro ya Sealy posturepedic yatahakikisha usingizi wenye afya. Na sasa vyote hivi vinapatikana katika duka namba 47, Mlimani City. Wataalamu wetu wapo tayari kusikia mahitaji yako na kuyafanyia kazi. Famous Furniture inatarajia kufungua maduka mengine matano (5) nchini kote kabla ya mwisho wa mwaka 2018.
Famous Furniture ni kampuni iliyo chini ya Bravo Group Manufacturing (Pty) Ltd yenye viwanda 7 Afrika Kusini na inayoongeza kwa kuwa na bidhaa bora za chumbani na sebuleni.
UKWELI
Anuani: Mlimani City Mall, duka namba 47, Barabara ya Sam Nujoma, Dar es salaam, Tanzania
Simu: Nabeel Dharsee - +255713722911
Kwa maelezo na msaada zaidi, wasiliana na:
Nabeel A Dharsee, Meneja Mkuu
+255713722911
nabeel@bravogroup.co.za

Kifo Cha kanumba : Ushahidi Wa kwanza umetolewa Leo 19 October

Leo Oktoba 19, 2017 mahakama kuu chini ya Jaji Sam Rumanyika imeanza kuisikiliza shauri la kesi ya jinai namba 125 ya mwaka 2012, Inayomkabili Msanii Elizabethi Michael ya kumua msanii mwenzie Steven Kanumba bila kukusudia mbapo leo upande wa jamhuri ulikuwa na Mashahidi 2 na shahidi namba moja alikuwa ni Mdogo wake Steven Kanumba Aliyejimabulisha kama Seth Bosco, lakini shahidi wa pili aliomba udhuru wa kutofika leo.
Katika maelezo ya Shahidi Seth Bosco akiongozwa na wakili wa Jamhuri Faraja George ameieleza mahakama kuwa Kanumba ndiye aliye mfungulia mlango Lulu, na alipofika ndani baada ya muda kidogo yeye akiwa chumbani kwake alianza kusikia mvutano wa sauti ya Kanumba ikimwambia Lulu
"kwanini Unaongea na 'Boyfriend' wako mbele yangu?" Mabishano yalianzia kwenye korido, na baada ya kuingia chumbani zilianza kusikika kelele
Baada ya muda mfupi Lulu aliinita na kuniambia Kanumba ameanguka najaribu kumwagia maji naona haamki, nilipoingia chumbani nikweli nilikuta yuko chini akiwa ameegemea ukuta, nikamchukua nikamlaza chali na ndipo nilipoanza kumtafuta Daktari wake anayeitwa Paplas Kageiya, daktari alipofika alimfanyia 'Chek up' akasema ameshafariki, akashauri tumpeleke Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, niliendesha gari mpaka muhimbili, tulipofika muhimbili kwenye kitengo cha dharura walituambia tukatafute utaratibu wa kipolisi, wakati wao wanaandaa vibali vya kuruhusiwa apelekwe mochwari, Baada ya mahojiano ya Polisi katika kituo cha urafiki Ubungo, niliondoka na Askari kurudi nyumbani kwaajili ya uchunguzi, baada ya polisi kufika pale wakiwa chumbani wanaendelea na uchunguzi walikuta Panga chini ya kitanda" Alisema shahidi Seth Bosco
Baada ya ushahidi huo, mahakama imeahirisha shauri hilo hadi kesho Oktoba 20, 2017 kwaajili ya kuendelea kusikiliza mashidi wengine Wanne kutoka upande wa Jamhuri.
Upande wa mstakiwa unaongozwa na Wakili Msomi Peter Kibatala.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa kwa siku tatu mfulilizo, ingawa Jaji Rumanyika ameelekeza upande wa mstakiwa na Jamhuri kuona kama wnaweza kutumia hata siku mbili kuisikiliza na siku ya tatu ikatumika kuandika hukumu.

Mke Wa Mugabe Amshtaki Mfanyabiashara kwa kutomuuzia Pete ya $1.35m

Zimbabwe na mkewe Grace MUgabe
Mke wa rais nchini Zimbabwe Grace Mugabe amemshtaki mfanyibiashara mmoja kwa kushindwa kumpatia pete ya almasi yenye thamani ya $1.35m kulingana na chmbo cha habari cha Herald.
Jamal Ahmed alidaiwa kumpatia pete yenye thamni ya $30,000 badala ya ile aliyoagiza.
Ni mgogoro wa hivi karibuni kuhusu pete hiyo yenye Carat 100 iliotarajiwa kuwa zawadi ya rais Mugabe kwa mkewe wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ndoa yao.
Mwaka uliopita, bwana Ahmed aliwashtaki Bi Grace Mugabe na mwanawe wa ndoa yake ya kwanza mahakamani baada ya kuchukua mali zake katika mgogoro wa pete hiyo.
Alisema katika nakala za mahakamani kwamba bi Mugabe alitaka kurudishiwa fedha zake baada ya pete hiyo ya almasi ilionunuliwa Dubai kukabidhiwa yeye baada ya kusafishwa na mtu mwengine.
Wakati aliposhindwa kulipa fedha hizo kwa akaunti moja huko Dubai, licha ya kusema kuwa fedha hizo zilitumwa kupitia benki moja ya Zimbabwe mke huyo wa rais alichukua kwa lazima nyumba zake.
Bwana Ahmed alisema kuwa alinyanyaswa, kutukanwa na kutishiwa na kuambia hawezi kuchukua hatua yoyote kwa kuwa walioshtakiwa ndio 'Zimbabwe'.
Disemba iliopita jaji mmoja alimuagiza bi Mugabe kurudisha mali hiyo.
Na sasa anamshtaki bwana Ahmed , ambaye ana kibali cha kuishi nchini Zimbabwe na biashara katika taifa hilo kwa $1.23m ili kulipa deni hilo.

Shehena ya bangi yaibuka kwenye ajali

Kibaha. Majeruhi wawili wa ajali ya gari wanashikiliwa na polisi mkoani Pwani wakituhumiwa kuhusika na usafirishaji na biashara ya bangi kilo 7,500.
Majeruhi hao ni Gudluck Kundaeli maarufu Mbowe (24) mkazi wa Kiwalani na Ally Gebra maarufu Mtena (28) wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jonathan Shanna amesema leo Alhamisi Oktoba 19,2017 kuwa watuhumiwa walikamatwa jana eneo la Kwa Mathias mjini Kibaha baada ya upekuzi kufanyika kwenye gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota IST lililopata ajali.
Amesema gari hilo lilipata ajali eneo hilo saa tatu usiku na askari walifika kutoa msaada ikiwemo kuwaokoa majeruhi ambao walipelekwa Hospitali ya Tumbi kwa matibabu.
Kamanda Shanna amesema baada ya kuwaokoa majeruhi na askari kufanya upekuzi kwenye gari walikuta magunia saba yenye bangi.
"Tulipata taarifa ya ajali kutokea eneo la Kwa Mathias, askari wakaenda kwa ajili ya uokoaji na waliwaokoa vijana hawa. Baadaye walifanya upekuzi kwenye gari na kukuta bangi hiyo. Tumepima ina kilogramu 7,500 kwa hiyo tunawashikilia watusaidie katika uchunguzi," amesema Kamanda Shanna.

Kauli ya Ridhiwani kikwete kuhusu Tundu Lissu,,,,

Mbunge mpya wa Jimbo la Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete amefunguka na kusema kuwa amefurahi kumuona Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akiwa mwenye tabasamu na furaha na kuzidi kumuombea apone kabisa na kurudi kupambana.
Ridhiwani Kikwete amesema hayo kupitia mtandao wake wa Instagram na kusema Mungu siku zote anatenda wema kwa watu kufuata kushambuliwa kwa risasi nyingi Tundu Lissu na hatimaye kuweza kupona na sasa furaha yake kuanza kurejea.
"Mungu utenda wema siku zote. Ashukuliwe yeye kwa kazi ya kurejesha tabasamu katika sura yako na afya kwa wanaokuuguza. Nimefurahi kukuona tena msomi, Kiongozi wangu na mwana kamati mwenzangu wa Bunge ukitabasamu na mwenye Afya njema. Mungu akulinde na akusimamie katika matibabu yako .Looking forward to see you back into your good shape" aliandika Ridhiwani Kikwete
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mnamo Septemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma na kisha baadaye kusafirishwa na kupelekwa jijini Nairobi Kenya kwa matibabu ambapo mpaka sasa yupo nchini Kenya akiendelea kupatiwa matibabu

CHADEMA Waliamsha Dude

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeweka wazi kwamba hakimuhitaji Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Bw. Christopher Kazeri kuwa msimamizi wa uchaguzi mdogo kwa madai hawana imani naye pia hana sifa kwani anaweza kusababisha umwagikaji wa damu.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeweka wazi kwamba hakimuhitaji Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Bwana Christopher Kazeri kuwa msimamizi wa uchaguzi mdogo kwa madai kwamba hawana imani naye pia hana sifa kwani anaweza kusababisha umwagikaji wa damu.
Akiitoa taarifa hiyo Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini Amani Golugwa amesema kwamba Mkurugenzi huyo alipoteza sifa za kusimamia uchaguzi tangu Juni, 24 walipokuwa kwenye uchaguzi wa vitongoji na vijiji kwa kufoji matokeo katika vijiji kadhaa na kuwalazimisha wasimamizi wabadilishe namba kwenye fomu.
Golugwa amesema kwamba vitendo ambavyo Mkurugenzi huyo alivifanya anavitafsiri kama mambo ya kihuni kwani yalipelekea kugombanisha watu ambao ni ndugu hivyo hofu yao ni kwamba anaweza kusababisha umwagikaji damu katika uchaguzi mdogo wa marudiano Arumeru Mashariki.
"Tumeishauri Tume iweze kuwasiliana na mamlaka ya uteuzi kwamba hatumtaki ndg Kazeri awe msimamizi wa uchaguzi huu mdogo Arumeru Mashariki, kwanza aliingilia uchaguzi wa vitongoji na vijiji na kulazimisha kubadilishwa matokeo ambayo yalionyesha Chadema wameshinda, jambo ambalo lilileta ugombanishi kwa wagombea, na hata wagombea wa CCM walikataa matokeo kwa kukubali kwamba walishindwa na hata wasimamizi na askari waliokuwepo hapo walithibitisha kwamba Chadema walikuwa wameshindwa" Golugwa
Ameongeza "Kama uchaguzi wa vitongoji Mkurugenzi ametumia mabavu na kufanya uhuni ambao tumeumbatanisha kwa Tume, kwenye uchaguzi huu wa madiwani si ataleta hata vifaru au kusababisha umwagaji wa damu? Kwa busara na hekima ya kawaida matendo aliyoyafanya Kazeri hayampi sifa ya kuwa msimamizi.
Hata hivyo Golugwa amefafanua na kusema kwamba wamewasilisha ushahidi wa wagombea wa CCM wakikataa kupokea ushindi huo wa vitongoji kwa madai kwamba hawawez kupokea ushindi wa mtutu wa bunduki.

Mwigamba avuta 'jeshi' kujiunga CCM

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Samsoni Mwigamba na wanachama wengine 10 wametangaza kujiunga na chama cha CCM baada ya kujivua uanachama wa ACT Wazalendo leo.
Taarifa za Mwigamba kujiunga na CCM zimetolewa leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, na kusema kwamba wameamua kufanya hivyo ili kujitenga na upinzani unaokerwa na maendeleo ya nchi, na pia kuunga mkono juhudi za serikali za mapambano dhidi ya rushwa.
“CCM ya sasa ndicho chama kinachotekeleza kwa karibu itikadi, falsafa na sera za ACT Wazalendo ambazo mimi na wenzangu tulishiriki kukiasisi, nchi yetu ndio kinara wa mapambano dhidi ya rus
hwa sasa hivi, sera ambazo ndio misingi ya ACT Wazalendo, tumeamua kujitenga na upinzani unaokerwa na mafanikio ya nchi ili tuendelee kuwa sehemu ya mapambano katika kurejesha nchi kwenye misingi yake”, amesema Mwigamba.
Samson Mwigamba atakuwa kiongozi wa pili ACT Wazalendo kujivua uanachama wa ACT Wazalendo kwa mwaka huu baada ya Prof. Kitila Mkumbo ambaye naye alifanya hivyo wiki kadhaa zilizopita.

Nafasi za kazi Leo 19

Bonyeza Links Zifuatazo Kusoma zaidi na Kuapply
Nafasi zingine ingia Nafasi za kazi leo October 19
2 Job Opportunities at Vodacom Tanzania
Job Opportunity at Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA)
Job Opportunity at Alliance for a Green Revolution in (AGRA), Finance & Administration Officer
Job Opportunity at Multinational
Bank, Branch Manager
Job Opportunity at TAPBDS CO LTD, Accountant
Job Opportunity at The Belgian Red Cross, Regional Cash Delegate, Tanzania
Job Opportunity at EngenderHealth Tanzania, Research Coordination Advisor
Job Opportunity at NMB Tanzania, Senior Manager Branch Technology Support
Job Opportunity at ILO, Technical Officer
www.ajirayako.co.tz

Picha ya faru aliyeuawa yashinda tuzo ya picha bora

Picha ya kutisha ya uhalifu wa mazingira imetangazwa kuwa mshindi katika tuzo za shindano la wapiga picha la mwaka huu
Picha ya kutisha ya uhalifu wa mazingira imetangazwa kuwa mshindi katika tuzo za shindano la wapiga picha la mwaka huu.
Picha hiyo iliopigwa na mpiga picha wa Afrika Kusini Brent Stirton inaoyesha hali ya faru mweusi katika mbuga ya wanyama pori ya Hluhluwe Imfolozi.
Wawindaji haramu walimuua mnyama huyo usiku kabla ya kumtoa pembe zake.
Stirton alipiga picha hiyo ikiwa miongoni mwa uchunguzi kuhusu biashara haramu ya bidhaa za faru.
Mpiga picha huyo alizuru zaidi ya maeneo 30 uliofanyika uhalifu huo wakati wa uchunguzi wake ambao aliutaja kuwa wa kuogofya.
Mwanangu wa kwanza atazaliwa mnamo mwezi Februari ; nina umri wa miaka 48. Unaweza kupoteza utu mara nyengine.
Stirton, ambaye alipokea tuzo hiyo katika tamasha la chakula cha jioni lililofanyika katika jumba la kumbukumbu mjini London , anaamini kwamba unyama huo aliofanyiwa faru huyo ulitekelezwa na wakaazi wa eneo hilo.
Lengo kubwa la uwindaji huo ni kuuza pembe mbili za faru huyo kwa wafanyibiashara.
Wafanyibiashara hao baadaye huzipeleka pembe hizo hadi Afrika Kusini kupitia Msumbiji hadi China ama hata Vietnam.
Katika mataifa hayo ya bara Asia, pembe za faru zina thamani ya juu ikilinganishwa na dhahabu ama dawa ya kulevya ya Cocaine.
Biashara hiyo hupata msukumo wa imani kwamba sawa na kucha za vidole vya mguuni, zinaweza kutibu ugonjwa wowote kutoka saratani hadi mawe ya figo.
Brent Stirton aliambia BBC : Kwa mimi kushinda tuzo hii, kwa majaii kuweza kutambua kazi yangu ni wazi kwamba tunaishi katika muda tofauti na kwamba hili ni swala nyeti.
''Swala la kuangamia kwa baadhi ya wanyama ni la kweli na faru ni mojawapo ya aina ya wanyama wanaoendelea kuangamia kwa kiwango kikubwa na ninashukuru kwamba majaji waliweza kutambua picha yangu kwa kuwa inaliangazia swala hili kwa hatua nyengine''.
Lewis Blackwell, mwenyekiti wa jopo la majaji hao wa WPY, alisema kuwa picha hiyo ya faru ilikuwa na athari kubwa katika jopo lake.
''Watu wanaweza kusinywa ama kushtushwa lakini ukweli ni kwamba picha hiyo inakuvutia na kukufanya kuhisi kana kwamba unataka kujifunza mengi.Unataka kujua habari kuihusu. Na huwezi kuitoroka kwa sababu inakuangazia yale yanayoendelea duniani''.

MAGAZETI YA LEO 19/10/2017














AUDIO | Rayvanny _ Tabia | Np3 Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/282350/by/nUXzBDbVsZ

Msami afunguka ishu ya kutoka na Nandy Kimapenzi

Msanii wa Bongo Flava, Msamii amesema si kweli kwamba ameshawahi kutoka kimapenzi na Nandy.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma katika mahojiano na Bongo5 amesema Nandy ni kama dada yake hivyo hawezi kufanya hivyo.
“Nandy sijawahi kupita naye ni kama mdogo wangu, dada yangu, kwa hiyo kwa sasa hivi mimi na Nandy ni kaka na dada, let say mimi ni mtu ambaye nimetoka kwenye familia ya THT Nandy pia kwenye familia hiyo hiyo, tupo familia moja” amesema Msami.
Msami anaungana na rapper Bill Nass ambaye amekuwa akidaiwa kuwa na mahusiano na Nandy kitu ambacho amekuwa akikikanusha kila mara.