Thursday, 23 November 2017

Usajili wa Yanga imebaki siku Tatu



IKIWA Dirisha Dogo la Usajili limefunguliwa Novemba 15 mwaka huu na litafungwa Disemba 15, klabu hutumia kipindi hiki kidogo cha usajili kuongeza wachezaji katika kuimarisha vikosi vyao katika kuelekea Raundi ya 11, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema baada ya siku tatu mambo yatakuwa hadharani.

Mkwasa amesema kwa kipindi hiki bado wapo katika mikakati ya kuangalia wapi panahitaji mtu wa kuziba pengo baada ya hapo watatoa taarifa kamili baada ya kukaa na kamati ya usajili na kutangaza rasmi ni mchezaji gani ameongezwa kwa kusikiliza mahesabu ya Kocha Mkuu George Lwandamina.

Tukiangazia klabu mbalimbali, kwa upande wa Klabu ya Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo, wakifanya hivyo msimu wa 2014-15, 2015-16, 2016-17, lakini pia wakisimama kama mabingwa wa kihistoria wa ligi hiyo kwa mara 27 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1965, inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 20.

Kwa misimu wa mwaka 2017/18, Yanga wamekuwa wakiweka mikakati katika usajili kwa maana ya kuandaa timu nzuri katika mapambano ligi hii, ndiyo maana kwa sehemu kubwa wameweza kupambana ili kupata pointi na kutaka kuongoza ligi ingawa changamoto kubwa ni michuano ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment