Saturday 16 December 2017

Zaidi Ya kaya 100 zakosa makazi Songea



Zaidi ya Familia 100 hazina mahali pa kuishi kufuatia nyumba zao kubomoka na kuezuliwa kwa upepo uliuoambatana na mvua kali iliyonyesha usiku wa kuamkia leo ambapo nyumba zaidi ya 60 na vyumba vitano vya madarasa ya shule ya msingi Chandamali kata ya Bombambili manispaa ya Songea vimeezuliwa.
Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Songea chini ya mwenyekiti wake mkuu wa wilaya Pololeti Mgema wamewatembelea wananchi waliokumbwa na kadhia hiyo kwa lengo la kutoa pole kwa wahanga.
Serikali imewataka wananchi kuzingatia kanuni bora za ujenzi kwani nyumba nyingi zilizoezuka zimejengwa bila kuzingatia kanuni za ujenzi, aidha serikali itaelekeza nguvu zake kukarabati vyumba vitano vya shule ya msingi Chandamali hivyo wananchi waanze kukarabati nyumba zao bila kusubiri msaada.
Wakati huo miundo mbinu ya Tanesco nguzo zimedondoka na nyaya za umeme kusambaa hovyo, aidha huko Matimila halmashauri ya wilaya ya Songea nyuma 15 zimeezuka na jengo la utawala la sekondari ya Matimila gharama za hasara iliyotokana na maafa hayo bado haijafahamika serikali inaendelea kukusanya taarifa sahihi.

Simba yafanya Maamuzi Magumu



SIMBA SC imesajili wachezaji watatu wapya wa kigeni, beki Mghana Asante Kwasi, kiungo mshambuliaji Mzambia Jonas Sakuwaha na mshambuliaji Antonio Dayo Domingues kutoka Msumbiji.
Wakati dirisha dogo la usajili linakaribia kufungwa jana, viongozi wa Simba walikuwa wanahaha kukamilisha usajili huo, hususan wa mchezaji Kwasi, ambaye bado ana mkataba na klabu yake ya sasa, Lipuli ya Iringa.
Lakini kwa Sakuwaha na Domingues hakukuwa na tatizo na habari zinasema wachezaji hao watachukua nafasi za beki Mzimbabwe, Method Mwanjali na washambuliaji, Mghana Nicholas Gyan na Mrundi Laudit Mavugo.
Wapinzani wao, Yanga wamesajili wachezaji wawili tu wapya, beki Fiston 'Festo' Kayembe Kanku kutoka Balende FC ya kwao, DRC na mshambuliaji kinda, Yohanna Nkomola ambaye ni mchezaji huru, aliyekuwamo kwenye kikosi cha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys.
Azam FC imeingiza mmoja tu mpya, mshambuliaji Bernard Arthur kutoa Liberty Professional ya Ghana, baada ya kumuacha Mghana mwenzake, Yahya Mohammed na Singida United imesajili saba wapya; Lubinda Mundia kwa mkopo kutoka Res Arrows ya Zambia, Daniel Lyanga kutoka Fanja ya Oman, Kambale Salita 'Papy Kambale' kutoka Etincelles ya Rwanda, Issa Makamba, Assad Juma, Ally Ng’azi na Mohamed Abdallah wote huru waliokuwa Sereneti Boys.
Singida imewaacha wawili, Atupele Green na Pastory Athanas waliovunjiwa mikataba wakati Mohamed Titi na Frank Zakaria wametolewa kwa mkopo Stand United na Mbeya City imewasajili George Mpole kutoka Maji Maji na Abubakar Shaaban huru, baada ya kuwaacha Emmanuel Kakuti na mkongwe Mrisho Ngassa anayehamia Ndanda FC.

Ronaldo Atimiza ndoto yake



Nyota wa klabu ya soka ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo,
amesema anajisikia vyema kutimiza malengo yake kwenye ulimwengu wa soka na anafuraha kushindana na Lionel Messi kwa muda mrefu.
Akifanya mahojiano na tovuti rasmi ya FIFA, Ronaldo amesema ndoto yake ilikuwa kuweka historia na kuacha kumbukumbu kwenye ramani ya soka na hicho kitu kimetimia akiwa ametwaa mataji mengi pamoja na mafanikio binafsi ikiwemo tuzo tano za Ballon d’Or.
“Najisikia vizuri kutimiza malengo yangu, nilitamani sana kuweka historia kuacha jina langu kwenye vitabu vya soka, nimepata mafanikio mengi sana ngazi ya klabu na taifa, nafurahia kuwa mmoja wa wachezaji waliofanikiwa zaidi kama kuchukua tuzo tano sawa na Messi”, amesema Ronaldo.
Ronaldo ameongeza kuwa katika maisha yake amefanya kitu anachokipenda zaidi ambacho ni kucheza soka na amefanikiwa sana na hiyo inamuhamisha kuendelea kufanya vizuri akiwa bado anapenda soka kwasababu utafika wakati hawezi tena kufanya hivyo.
Ronaldo ameshinda taji la Ligi Kuu ya England EPL mara tatu akiwa na Manchester United kabla ya kutua Real Madrid na kushinda ubingwa wa La Liga mara mbili. Pia ameshinda taji la ligi ya mabingwa barani Ulaya UEFA mara nne.

BREAKING NEWS : Mkurugenzi Mkuu NHC Asimamishwwa kazi



Zitto Kabwe ahoji kuhama kwa makada Wa ACT



Kiongozi wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe ametumia hotuba yake ya ufunguzi wa kikao cha Kamati Kuu kuzungumzia wimbi la kuhama kwa makada wa chama hicho, akihoji iwapo kimeanza kupoteza mwelekeo.
Katika hotuba yake leo Jumamosi Desemba 16,2017, Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Mjini amewataka wajumbe wa kamati hiyo kujiuliza maswali magumu, likiwemo la kwa nini hali hiyo inakikumba chama chao.
Makada wa chama hicho waliojiunga na CCM ni Profesa Kitila Mkumbo aliyeachia nafasi ya ushauri wa ACT –Wazalendo baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho; wakili Albert Msando, Samson Mwigamba na Edna Sunga.
Katika hotuba hiyo, Zitto amesema hamahama hiyo imezua taharuki kwenye chama hicho na kuacha maswali juu ya kinachoendelea katika siasa za Tanzania.
“Ni lazima tujiulize maswali magumu sisi wenyewe na kuzungumza tukitazamana machoni, je hakuna sababu za ndani sisi wenyewe zinazokimbiza wanachama wetu? Kama zipo ni zipi? Je ni sababu ambazo tunaweza kurekebisha na kukiimarisha chama," amehoji Zitto.
Amesema, "Kama ni sababu zilizo nje ya uwezo wetu tunafanya nini ili kuzikabili, je bado sisi tunaamini katika misingi ya chama kwa mujibu wa Azimio la Tabora? Tulikuwa kundi tu tulioumizwa na vyama tulivyokuwamo na tukaamua kuunda chama kupoza hasira zetu tu na sasa hasira zimeisha hakuna sababu ya chama kuwapo."
Amesema kati ya waanzilishi watatu wa ACT, wawili wamekikimbia na kujiunga na CCM na kwamba, jambo hilo huenda likarutubisha hoja kuwa chama hicho kilikuwa mradi wa chama tawala, kwamba sasa hauna maana tena.

Wabakaji Watoto Kuuwawa India



Wabakaji wa watoto wanapaswa kuuawa katika muda wa miezi sita tangu watekeleza uovu huo, mteteaji mkuu wa haki za wanawake India amependekeza.
Swati Maliwal ametoa ombi hilo katika barua aliyomuandikia waziri mkuu Narendra Modi.
Iliandikwa kuendana na kumbukumbu ya mwaka wa tano tangu mwanafunzi Jyoti Singh mwenye umri wa miaka 23 alipobakwa na gengi la wanaume, kifo chake kilichozusha maandamano ya kitaifa.
"Hakuna kilichobadilika kaika miaka mitano iliyopita," Bi Maliwal, ameiambia BBC.
"Delhi bado ndio mji mkuu wa ubakaji. Mwezi uliopita, mtoto wa kike wa mwaka mmoja na nusu alibakwa na gengi la wanaume, na ubakaji wa mtoto wa miaka saba,na mwingine wa kike wa mwaka mmoja na nusu alibakwa."
Kwa wastani, alisema, watoto watatu wa kike na wanawake wasita wanabakwa katika mji mkuu huo kila siku.
India ilifanyia mageuzi sheria zake kuhusu ubakaji kutokana na shutuma miaka mitano iliopita, na ilichukua hatua kuharakisha kusikilizwa kesi na kuwashinikiza maafisa wa polisi kutilia uzito tuhuma za ubakaji na unyanyasaji wa kingono.

Rais Mstaafu CWT anaswa na TAKUKURU



Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU inamshikilia Rais mstaafu wa Chama Cha walimu Tanzania (CWT) Gracian Mkoba kwa tuhuma za rushwa.
Hilo limethibitishwa na Afisa Uhusiano wa TAKUKURU Makao Makuu, Mussa Misalaba, ambaye amesema wanamshikilia Mkoba kwa tuhuma za kugawa fedha kwa baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho ili kuwashawishi wamchague mgombea anayemtaka.
"Mukoba ameshastaafu, lakini kuna mgombea mmoja alikuwa anataka achaguliwe, tumemkamata leo asubuhi akigawa rushwa kuwashawishi wapiga kura kwenye ukumbi wa Chimwaga wamchague huyo mgombea wake," amesema Misalaba.
Misalaba ameongeza kuwa TAKUKURU inaendelea kufanya uchunguzi zaidi dhidi ya Mukoba kabla ya kumfikisha mahakamani.
Mukoba anakuwa mtu wa tatu kukamatwa na TAKUKURU kwa tuhuma za rushwa kwenye uchaguzi ndani ya wiki moja, wengine ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Sadifa Juma Khamis na mfanyabiashara Haider Gulamali.

Waziri azindua mfumo Wa kieletroniki utambuzi wanamuziki



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe leo December 16, 2017 amezindua mfumo mpya wa Kieletroniki wa Utambuzi wa Wanamuziki ambao utaanza kutumika nchini kwa ajili ya kulinda maslahi ya wasanii.
Moja ya vitu ambavyo Dr. Mwakyembe amevizungumza ni kuhusu kuibiwa na kutumiwa kwa kazi za wasanii na watu wachache bila ridhaa yao “tulipotoka ni kubaya, mimi nilikuwa DRC nilichoshangaa sana nilipita sehemu nikakuta picha kubwa ya Kanumba kule ni Star, ukija hapa mi nlifikiri kaacha mali za ajabu sana,”
“Vijana wetu wana majina makubwa, mifukoni hawana kitu, mambo mengi yanaudhi ni kwenye sanaa, tutakwenda Mahakamani haiwezekani huu unyonyaji, ngoja tuondoe hii njaa ya mwanzo afu nianze kupambania mambo mengine,” – Dr. Mwakyembe

Waziri Jafo Azuia shule ya Ihunge kuwa Chuo Kikuu



Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo amewasisitiza viongozi wa mkoa wa Kagera kutokubadilisha malengo ya shule ya Ihungo kwa kuigeuza kuwa chuo kikuu baada ya kukamilika kwa ujenzi.
Jafo ameyasema hayo alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo inayojengwa upya baada ya hapo awali kukumbwa na tetemeko la ardhi.
Shule ya Ihungo inajengwa kisasa na itakapokamilika itakuwa shule ya kipekee kwa kuwa na miundombinu ya kisasa hapa nchini.
Amesema Majengo ya shule hiyo kwasasa yanaweza kuwatamanisha baadhi ya viongozi kutaka kubadilisha shule hiyo hapo baadae kuwa chuo kikuu kitu ambacho amezuia jambo hilo.
Amesema amezuia ili vijana wa kidato cha tano na sita ili waweze kupata nafasi kusoma katika shule hiyo yenye mazingira mazuri.
Baada ya ukaguzi wa shule hiyo,Waziri Jafo alielekea na ukaguzi wa shule nyingine ya Nyakato inayojengwa na Suma JKT na kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi.

Tani 9 za dawa ya meno Aloe zaangamizwa Zanzibar



Wafanyakazi kutoka Bodi ya Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar wameangamiza Tani tisa za Dawa ya meno aina ya Aloe zilizoharibika katika jaa la Kibele Wilaya ya Kati Unguja
Dawa hizo ziliingizwa nchini na Kampuni ya Bacelona Interprises Limited zikiwa zimeharibika baada ya kontena lilikuwa na dawa hizo kuinga maji wakati wa kusafirishwa kuja Zanzibar .
Mkaguzi Mkuu wa Wakala wa Chakula Dawa Zanzibar Mwadini Ahmadi Mwadini alisema walibaini kuwa dawa hizo zimeharibika wakati wa kuzitoa bandarini na kumshauri mmiliki wa dawa hizo kuzirejesha zilikotoka au kuziangamiza na alikubali ziangamizwe ili kujiepusha na gharama nyengine.
Mwadini alisema Bodi inaendelea kufanya ukaguzi kwa bidhaa zinazoingizwa bandarini na maduka mbali mbali ili kuhakikisha zinakuwa salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
Aliwataka wafanyabiashara kuwa waangalifu wanapoagiza Bidhaa na kujenga ushirikiano wa karibu na Bodi yake kwa kutowa taarifa wanapoona bidhaa zao zinamashaka kuuzwa kutokana na kuharibika au kupitwa na muda wake wa matumizi.
Aidha aliwaomba wananchi wanaponunua bidhaa madukani na kuzigundua kuwa hitilafu watowe taarifa katika Bodi ili hatua zinazofaa ziweze kuchukuliwa kwa usala wao.
“Kama mukigundua kunafanyika udanganyifu kwa bidhaa mnazonunua kama kuharibika au kupitwa na wakati musisite kutoa taarifa kwetu, tupo kwa ajili ya kulinda usalama wa wananchi.” alisema Mkaguzi Mkuu.
Nae mtoa mzigo Bandarini aliesimamia kontena hilo Omar Kombo Sharif alisema mzigo huo uliingia Zanzibar mnamo mwezi wa nane na baada ya kubainika umeharibika walitoa taarifa kwa mmiliki na walikubaliana uzuiliwe kwa ajili ya kuuangamiza.
Wakati huo huo Mkuu wa Uchunguzi wa Chakula na Dawa Zanzibar Mohamed Shadhil alisema wamekamata Nyama ya ngombe kilo 180 iliyokuwa inasafirishwa kinyume na taratibu zilizowekwa na Bodi hiyo.
Alisema bidhaa hiyo imekamatwa wakati inasafirishwa kutoka machinjioni kwa kutumia Baskeli pamoja na vespa bila ya kuwa na kibali cha daktari na nikinyume cha utaratibu. Bidhaa za nyama zinatakiwa kusafirishwa kwa kutumia gari kwa ajili ya usalama wa watumiaji.
Nyama hiyo wameamua kuifukia baada ya kufanyika uchunguzi na kuwaita wamiliki ambao walikubali kuwa wamefanya kosa licha ya kulalamika kuwa utaratibu wa kusafiri bidhaa hiyo kwa kutumia baskeli na vespa umekuwapo kwa muda mrefu.
Mkuu huyo wa uchunguzi aliwataka wananchi wanaochinja nyama kufuata taratibu zilizowekwa ikiwemo kutumia vyombo vinavyotakiwa vyakuchukulia bidhaa hiyo ili kuepuka usumbufu na hasara katika biashara zao.

Waziri Lukuvi ampiga STOP mkurugenzi mkuu NHC



Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu amesimamishwa kazi.
Taarifa ya kusimamishwa kazi kiongozi huyo imetolewa leo Jumamosi Desemba 16,2017 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi akieleza uamuzi huo umetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.
Mchechu aliteuliwa kuliongoza shirika hilo Machi Mosi, 2010. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA.
Taarifa ya Dk Abbasi imesema Lukuvi amechukua uamuzi huo kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu F. 35 (1) cha Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2009.
Mbali na Mchechu, Lukuvi ameitaka bodi ya shirika hilo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Huduma za Mikoa na Utawala, Raymond Mndolwa.
"Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Dorothy Mwanyika imesisitiza kuwa uamuzi huo unapaswa kutekelezwa kuanzia leo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili watendaji hao," amesema.
Desemba 13, wakati Rais John Magufuli akizindua nyumba 300 za shirika hilo alieleza hujuma zinazofanywa na viongozi wa NHC, akiwemo Mchechu na Bodi ya wakurugenzi.
"Visumu sumu ambavyo vinaleta mawazo mengi vipo, unakuwa na shirika la kujenga nyumba wakati wewe ni mkurugenzi na ni shirika lako. Unanunua viwanja kule na wewe unakwenda unanunua maeneo unayaandikia kwa majina fulani, tukichunguza tunakuta vyako, mengine nimeyamezea kwa sababu ya kazi nzuri unayofanya," alisema Rais Magufuli.
Katika hotuba yake, Rais alimtaka Mchechu kuwa makini na watu anaofanya nao kazi kwa maelezo kuwa wapo wanaotaka nafasi yake na kutumia wajumbe wa bodi na wanasiasa kumchafua.
"Wako wanaokupiga vita kwa wivu wao, lakini na wewe saa zingine matumizi yanakuwa ya ajabu," alisema Rais.

Salam Za JK Kikwete baada ya Zanzibar Heroes kufuzu Fainali challenge cup



Baada ya timu ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ kufuzu kucheza fainali ya michuano ya CECAFA Senior Challenge Cup 2017, Rais mstaafu wa serikali ya awamu ya nne Dr. Jakaya Kikwete ‘JK’ ametuma salam za pongezi kwa timu hiyo.
Kupitia ukurasa wake wa twitter JK ameandika: “Nawapongeza Zanzibar Heroes kwa kututoa kimasomaso na kutinga fainali. Nawatakia kila la kheri katika mechi ya fainali waibuke na kombe na watupe raha ambayo Watanzania tumeikosa kwa muda mrefu.”
Zanzibar waliifunga 2-1 timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ kwenye mchezo wa nufu fainali, ikumbukwe Uganda ndio walikuwa mabingwa watetezi wa kombe hilo walilolitwaa mwaka 2015. Mwaka huohuo Uganda waliifunga Zanzibar 4-0 katika mchezo wa hatua ya makundi.
Mchezo wa fainali utachezwa Jumapili December 17, 2017 kati ya wenyeji Kenya dhidi ya Zanzibar.

Zitto Kabwe aiombea uanachama Zanzibar heroes



Mbunge wa Kigoma mjini Mh. Zitto Kabwe ambaye ni mdau mkubwa wa michezo hususani soka amekiombea aunachama wa FIFA chama cha soka cha Zanzibar ZFA.
Hatua hiyo imekuja baaada ya timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kutinga hatua ya fainali ya michuano ya CECAFA Senior Challenge 2017 inayoendelea nchini Kenya.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook Zitto amefunguka ya moyoni akitaka ZFA iwe mwanachama wa shirikisho la soka la kimataifa FIFA pamoja na lile la Africa CAF angalau kwa miaka mitano na inaweza kupiga hatua ambazo TFF imeshindwa.
“Kama hatutaki Zanzibar kuwa Mwanachama wa FIFA kama ilivyo Scotland. Tuseme kwa miaka 5 ijayo kuanzia mwaka huu ZFA ndio mwanachama FIFA na CAF ili TFF ipate muda wa kujipanga. Ndani ya hiyo miaka 5 nawaambia Zanzibar itakwenda AFCON na hata Kombe la Dunia. #MsemaKweliMpenziWaMungu”, ameandika Zitto Kabwe.
Zitto ametoa mfano kuwa Zanzibar ingepata uanachama kamili wa FIFA kama ilivyo kwa nchi za Scotland pamoja na Wales ambazo pia ni nchi dada za taifa la Uingereza lakini zinatambuliwa na FIFA kama mataifa wanachama huku Uingereza ikitambulika kama England

Mwaijage Ameitaka kampuni ya mbolea kubadili mfumo



WAZIRI wa Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage, ameitaka Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC) kubadilisha mfumo wa utendaji ikiwa ni pamoja na kutoingia mikataba inayoweza kuisababishia serikali hasara, badala yake kuangalia wabia wanaoweza kuisaidia kujipanua na kupata faida kubwa zaidi.
Waziri Mwijage, aliyasema hayo juzi wakati akiizindua bodi mpya ya Wakurugenzi ya TFC, na kuongeza kwamba serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli, haiko tayari kuona taasisi zake za umma zikiingizwa katika mikataba mibovu na isiyokuwa na tija.
Pia aliagiza kwamba, baada ya kuizindua bodi hiyo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Egid Mbofu na wajumbe wake, waanze kazi mara moja na moja ya majukumu yao ya awali ni kuangalia ama kuipitia upya miokataba ambayo awalo iliingiwa na TFC.
Alisema TFC ikifanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kujielekeza kwenye kazi zenye faida kubwa, itaweza kusaidia kasi ya kuendeleza sekta ya kilimo nchini, na kufikia malengo ya serikali ya awamu ya tano ya Taifa la uchumi wa kati na wa Viwanda.
"Tunatambua sekta ya kilimo ni nguzo muhimu kwa ajili ya uchumi wa TANZANIA, lakini haiwezi kuleta mafanikio makubwa kwa jamii, ikiwa TFC haitaweza kupewa uwezo na kuwafikia wakulima wengi zaidi", alisema Waziri Mwijage

Ramsey Noah asema pengo la kanumba haliwezi kuzibikka



NGULI wa filamu za Nigeria, Ramsey Noah amesema japokuwa miaka mingi imepita tangu kufariki dunia kwa aliyekuwa msanii mahiri wa filamu za Kibongo, Steven Kanumba, bado pengo lake haliwezi kuzibika katika ulimwengu wa tasnia ya filamu.
Akizungumza katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam alikoenda kuzuru kaburi la marehemu Steven Kanumba leo Jumamosi, Desemba 16, 2017, Ramsey, alisema Kanumba aliondoka kipindi ambacho nyota yake ya mafanikio ndiyo kwanza ilikuwa imeanza kung’ara na kwamba, kila anapomkumbuka na mambo waliyoyafanya pamoja, huwa haamini kama hatamuona tena maishani mwake.
Ramsey alizuru hapa nchini kuhudhuria Tamasha la Kutambua Fursa kwa vijana lilioandaliwa chini ya Kampuni ya Sahara, tamasha hilo lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), juzi Alhamisi.
Katika kuzuru kaburi hilo aliongozana na mama mzazi wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa, mdogo wa marehemu, Seth Bosco, wasanii wa filamu na mashabiki wa marehemu Kanumba.
Ramsey ndiye msanii wa kwanza mkubwa nchini Nigeria kufanya filamu na Mtanzania ambapo walifanya Moses na Devil’s Kingdom jambo ambalo liliunganisha Bongo Movie na Nollywood hivyo kutengeneza uhusiano imara kati ya nchi hizi mbili katika tasnia ya filamu.
Kanumba alifariki dunia Aprili 7, 2012 baada ya kutokea mzozo kati yake na aliyekuwa mpenzi wake, muigizazi Elizabeth Michael ‘Lulu’. Mwanadada huyo kwa sasa anatumiankifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na ya kumuua Kanumba bila kukusudia.

Kituo kimetakiwa kuwa kitovu Cha kuwaandaa na kuwanoa viongozi na taasisi nyengine


Arusha. Kituo cha maendeleo na ushirikiano wa kimataifa kati ya Tanzania na Denmark (MS-TCDC) kilichopo Usa River wilayani Arumeru mkoani Arusha, kimetakiwa kuwa kitovu cha kuwaandaa na kuwanoa kikamilifu viongozi wa Serikali na taasisi nyingine barani Afrika.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema hayo kwenye kongamano la maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kituo hicho kinachotoa mafunzo ya uongozi, utawala bora, demokrasia na masuala ya kijamii.
Mghwira aliyewahi kuwa mwalimu na mjumbe wa bodi ya kituo hicho, amesema jana Ijumaa Desemba 15,2017 kuwa kituo kina manufaa mengi, utajiri wa maarifa, elimu na fursa pana ya kujifunza.
“Niwatie moyo watumishi kwa kadri inavyowezekana waje kusoma, binafsi baada ya kufundisha kisha nikaingia kwenye uongozi imenisaidia,” amesema.
Mghwira amesema, “Moja ya mambo ya kuangalia kwenye majadiliano ni kuhakikisha kituo kinafanya kazi na nini kifanyike miaka 50 ijayo, sekta hii ya uongozi ifanyiwe kazi kikamilifu watu waandaliwe na wanolewe kuwa viongozi.”
Amesema kituoni hapo alifundisha masomo ya uongozi na utawala, haki za binadamu katika uongozi, haki za mama na mtoto.
Mkuu huyo wa mkoa amesema baada ya Taifa kuingia kwenye mkataba mpya wa kimataifa wa mtoto mjadala uliokwenda kwenye asasi za kiraia na kusaidia kupatikana sheria ya mtoto ya mwaka 2009.
Katika kongamano hilo lililohudhuriwa na Balozi wa Denmark Tanzanua, Einar Hebogard Jensen wito umetolewa kwa Serikali kushirikiana na kituo hicho kuendelea kuwajengea uwezo viongozi.
Macrine Rumanyika, mratibu wa muungano wa utepe mweupe wa uzazi salama Mkoa wa Arusha amesema alijifunza mafunzo ya afya ya jamii na katika kufanya kazi alikabiliwa na changamoto zilizomsukuma kwenda kusoma MS-TCDC.
“Nilihitaji elimu ya maendeleo, hivyo tangu mwaka 1996 nimekuwa mwanafunzi hapa katika kozi fupi na ndefu na baadaye nikiwa hapa nilipata shahada ya maendeleo ya jamii,” amesema.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano cha MS TCDC, Emmanuel Munisi amesema wadau waliofanya kazi katika kituo hicho walikutakana kujadili na kutafakari miaka 50 iliyomalizika na mingine 50 ijayo.

Libya, badala ya kuwa mkimbizi unageuka kuwa ‘mtumwa’



Maelfu ya watu kutoka nchi kadhaa za Kiafrika, wengi vijana, wanazipa mgongo nchi zao na kutafuta bahati zao Ulaya. Hali ngumu za maisha katika nchi zao, umskini na migogoro na vita imewasukuma kutafuta hata njia za hatari na zisizokuwa za kisheria kufika Ulaya. Kuna waliofaulu na kutambuliwa rasmi kuwa wakimbizi walipofika Ulaya, lakini kuna wengi waliozama katika Bahari ya Mediterenia. Kuna wengi ambao wamepata masaibu makubwa hata kabla ya kutia mguu Ulaya.
Nchi ya Libya baada ya kupinduliwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011, imegeuka kuwa “mchafukoge”, haina serikali iliyo imara na makundi tafauti ya kijeshi yamekuwa yakikabana roho. Hali hiyo ya fujo imewarahisishia watu kutoka nchi kadhaa za Kifrika kukusanyika katika miji iliyo kwenye mwambao wa Libya katika Bahari ya Mediterenia wakitamani waivuke bahari hiyo ili wafike Ulaya. Sasa Libya imekuwa ni kituo kukubwa kinachotumiwa na walanguzi wa biashara ya wanadamu kuwakusanya wateja wao wanaowaahidi kwamba watawafikisha “Mtoni” (yaani Ulaya). Makundi ya kijeshi katika nchi hiyo hushirikiana na walanguzi hao kuwakabidhi wakimbizi wa kutoka nchi mbalimbali za Afrika chini ya Jangwa la Sahara katika masoko na watu hao kuuzwa kama “watumwa”.
Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa ni kwamba hivi sasa wanaishi Libya hadi Waafrika milioni moja wakitokea nchi zilizo chini ya jangwa la Sahara, zile za Ukanda wa Sahel, Somalia, Eritrea na Sudan. Maelfu yao wamezuiliwa katika kambi, tena chini ya hali ya kutisha isiyokuwa ya kiutu. Libya ilisaidiwa na Umoja wa Ulaya kwa kupatiwa boti za doria kulinda mipaka yake ya bahari na pia kuziokoa boti zinazobeba wakimbizi na ambazo ziko katika hatari ya kuzama. Msaada huo umewezesha kupungua idadi ya watu wa kutoka nchi chini ya Jangwa la Sahara kuivuka bahari kutoka watu 11,500 Julai na kufikia 6,300 Septemba mwaka huu. Hiyo ina maana kwamba idadi ya watu wanaoshikiliwa kwa nguvu katika makambi ya Libya imeongezeka.
Malalamiko ya serikali za nchi za Afrika na pia mashirika ya kutetea hali za binadamu yalizidi pale televisheni ya Kimarekani, CNN, ilipotangaza na kuthibitisha hapo Novemba 14 kuweko Libya kambi za minada ambapo wakimbizi kutoka nchi za Kiafrika huuzwa kama watumwa. Jambo hilo, licha ya kwamba limeiaibisha Libya, lakini limetoa sura kwamba kuna serikali za nchi nyingine za Kiafrika zisizojali nini kinawasibu Waafrika wenzio huko Libya. Lakini, ilipojulikana kashfa hiyo, angalau serikali ya Rwanda ilitangaza kwamba itakuwa tayari kuwachukua Waafrika 30,000 wanaoshikiliwa katika kambi hizo.
Wizara ya mambo ya kigeni ya Rwanda ilisema mwezi uliopita: “ Kama ilivyo dunia iliyobaki, Rwanda nayo pia imeshtushwa na picha zilizochapishwa na zinazoonyesha maafa yaliyoko huko ambapo Waafrika- wakiwamo wanawake na watoto- waliokamatwa walipokua njiani kwenda kutafuta himaya ya ukimbizi Ulaya wanashikiliwa. Kutokana na falsafa ya kisiasa ya Rwanda na kutokana na historia yetu wenyewe, sisi hatuwezi kunyamaza kimya wakati watu wanafanyiwa uovu wa kinyama wa kuuzwa kwa mnada kama vile wao ni wanyama wa mifugo.” Tangazo hilo la serikali ya Kigali liliendelea kusema: “Huenda Rwanda haiwezi kusema kwamba kila mtu anakaribishwa, lakini mlango wetu uko wazi.”
Gazeti la New Times la huko Kigali liliripoti baadaye kwamba serikali ya Rwanda na Umoja wa Afrika (AU) zimekubaliana kwamba nchi hiyo itachukuwa wakimbizi 30,000 na waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo, Louise Mushukiwabo, aliandika katika mtandao wa Twitter kuhusu Waafrika wanaouzwa huko Libya: ” Rwanda ni nchi ndogo, lakini tutatafuta nafasi kwa ajili yenu.” Inasemakana Rwanda pia inafanya mazungumzo na Israel ili kuwachukua Wasudan na Waeritrea waliokwama huko Israel walipokuwa njiani kwenda Ulaya kutafuta ukimbizi. Moussa Faki Mahamat, mkuu wa Kamisheni ya AU, ameipongeza hatua ya Rwanda na akazitaka nchi wanachama wa AU, sekta ya kibinafsi na raia wa Kiafrika kuwaunga mkono ndugu zao wanaosononeka na kuteseka huko Libya.
Mwezi uliopita huko Abidjan, Ivory Coast, ulifanyika mkutano wa kilele wa kawaida baina ya Umoja wa Ulaya na Afrika ambao ulijishughulisha sana na siasa ya uhamiaji pamoja na kashfa hii ya kuuzwa na kununuliwa watumwa huko Libya. Pia, serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa iliahidiwa kusaidiwa ili iondokane na kambi hizo. Kutokana na malalamiko kutoka mashirika ya kiraia, siku chache zilizopita nchi zaidi za Kiafrika zimeondosha mabalozi wao kutoka Libya na zimeutaka Umoja wa Mataifa na Mahakama ya Kimataifa ya The Hague zilishughulikie suala hilo la unyama na uhalifu unaofanywa Libya.
Habari ya kuweko makambi ya utumwa nchini Libya si mpya, ila sasa malalamiko yaliotolewa ni makali zaidi, na mbinu zinazotumiwa na hao walanguzi wa biashara ya wanadamu ni za kikatili zaidi. Pia, licha ya nchi za Ulaya kulalamika juu ya kuweko kambi hizo, lakini nchi hizohizo zinafunga kabisa milango kwa wakimbizi. Nchi hizo za Ulaya zinataka hata wale wanaoomba ukimbizi ambao tayari wameshakanyaga ardhi ya Ulaya warejeshwe makwao. Shirika la Umoja wa Mataifa juu ya Uhamiaji (IOM), limetaja juu ya kuweko masoko ya watumwa huko Libya na limesema kwamba mustakbali wa watu hao haujulikani, si leo wala si kesho. Wengi wao wako karibu na maeneo ya Kusini kabisa ya Ulaya. IOM ilisema isitarajiwe kwamba hali ya mambo itabadilika.
Kwa mujibu wa mashahidi walioshuhudia minada hiyo ya kuuzwa binadamu huko Libya ni kwamba katika masoko hayo watu huuzwa na kununuliwa, halafu hupelekwa kufanya kazi ngumu. Watu wanaofanya biashara ya magendo ya binadamu humuuza kila mkimbizi kwa dola 200 hadi 500. Pia, hulazimihswa kuwapigia simu jamaa zao ili watume fedha zitakazowezesha wajikomboe. Pale familia zao wanaposikia sauti zao zikilia ndani ya simu, baadhi ya wakati fedha hutumwa. Hivyo ndivyo walanguzi wa biashara hii inayoshamiri wanavyotajirika. Wakimbizi ambao hawana bahati ya kutumiwa fedha za ukombozi na jamaa zao hunyimwa chakula hadi wanakufa. Kwa mujibu wa IOM hayo ni maelezo ya watu walioko sasa Niger na ambao wamerejea kutoka Libya.
Libya iliyosambaratika, ambapo haijulikani serikali gani inayoshika hatamu ni taabu kuinusuru. Nchini humo hakuna sheria, kila mtu anafanya anavyotaka ni shida kukomesha uuzaji na ununuzi wa binadamu, licha ya kuweko malalamiko mengi duniani.
Mara nyingi wanasiasa hujifanya “hamnazo”, hujitoa kimasomaso, bila ya kujali kama wanasiasa hao ni Waafrika au Wazungu, hulipuuza tatizo hasa ambalo liko machoni mwao. Viongozi wa Ulaya na Afrika wanatambua kuwapo Waafrika wanaokimbilia Ulaya ni kutokana na hali ngumu ya maisha katika nchi wanakotokea.
Karibu tutaingia mwaka 2018. Mambo hayaonyeshi yatabadilika, watu zaidi watarajiwe watajaribu kwa kila njia kuingia Ulaya kuliko miaka iliopita. Watajaribu kuivuka Bahari ya Mediterenia kwa kutumia boti za mbao zilizo mbovu na kongwe. Kwa wengi wao bahari hiyo itakuwa kaburi lao. Baada ya baridi ya sasa kupungua kidogo Ulaya, msimu wa kuangamia Waafrika wengi katika bahari hiyo utaanza. Inanihuzunisha.
Source: Mwananchi

TANESCO yaboresha mfumo Wa malipo




Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limeboresha mfumo wa malipo ya ankara na kuanzia sasa wateja wa mita za kawaida na wanaoomba kuunganishiwa umeme watalazimika kufanya malipo kwa mfumo wa kielektroniki.
Evaristo Winyasi, kaimu meneja wa Tehama, utafiti na utengenezaji mifumo wa Tanesco amesema mfumo huo umeanza Desemba 14,2017 kwa mikoa minne ya shirika hilo iliyopo Dar es Salaam na Pwani.
Amesema lengo la mfumo huo ni kutekeleza kwa vitendo matakwa ya sheria iliyopitishwa na Bunge, hivyo shirika limejiunga na mfumo huo ili kuhudumia wateja kwa kutumia benki na mitandao ya simu.
“Tumeshaungana na mfumo wa malipo ya Serikali wa GPG katika benki za NMB, CRDB na NBC. Kila benki imetoa njia zote za malipo ikiwemo ATM na simu,” alisema Winyasi jana Ijumaa Desemba 15,2017.
Amesema wateja wa Tanesco watafanya malipo kwa kutumia mitandao ya simu ikiwemo Airtel Money, M-Pesa na Tigo Pesa.
Winyasi amesema mteja hawezi kukamilisha malipo pasipo kufika ofisi za malipo na kupewa deni analodaiwa likiwa limeambatana na kumbukumbu namba ambayo itatumika kulipia kwa mfumo wa kielektroniki.
Meneja Masoko wa Tanesco, Mussa Chowo amesema madhumuni ya kujiunga na mfumo huo wa Serikali ni kurahisisha ukusanyaji wa mapato ya shirika.
Chowo amesema mfumo huo hautawahusu wateja wa mita za Luku. Amesema wataendelea kupokea malipo kwa wateja watakaolipia kwenye ofisi, huku wakipewa maelekezo na ukomo.
“Wiki tatu kutoka sasa; Januari (2018) kwa mikoa ya Dar es Salaam tutasitisha malipo kwenye ofisi na wateja watayafanya kupitia benki na mitandao ya simu,” amesema.

Ramsey Noah Atua BONGO azungumza na wanafunzi UDSM



Mwigizaji na mtayarishaji wa filamu wa Nigeria, Ramsey Nouh amewataka vijana wa Tanzania kuwa na shauku ya mafanikio na kutokubali kurudishwa nyuma katika juhudi za kujikwamua.
Nouah ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mradi wa uhamasishaji na kuwajengea uwezo vijana, kutambua na kusimamia ndoto zao unaoratibiwa na kampuni ya mafuta ya Sahara Group ukilenga kuwafikia zaidi ya vijana 10 milioni.
Nouah ambaye pia ni balozi wa Sahara Group amesema hakuna mafanikio ambayo yanaweza kufikiwa bila kupitia changamoto hivyo ni muhimu kwa vijana kukabiliana nazo bila kuyumbishwa.
Akijitolea mfano amesema mafanikio aliyoyapata hakuja kwa urahisi kwani alipigana na kusimamia alichokuwa akiamini.
“Imani yangu ilikuwa kwenye filamu, nilikuwa na shauku ya kufanya vizuri kwenye tasnia hiyo, sikujali changamoto nilizokutana nazo. Nilisimama na kufanya kazi kwa juhudi zaidi hadi pale watu walipoanza kunielewa,”
Sambamba na Ramsey, wengine waliopata nafasi ya kuzungumza na vijana hao ni mjasiriamali Jokate Mwegelo na mshindi wa Big Brother Africa mwaka 2014 Idris Sultan.
Kwa upande wake Jokate aliwataka vijana kuwa wabunifu na kutumia mawazo katika kuleta mabadiliko na maendeleo kwenye jamii.
“Ni nadra sana ukafanikiwa kwa kuiga kitu cha mwingine. Tujaribu kuwa na ubunifu, nilipomaliza chuo nilipata ufaulu mzuri ulioniwezesha kuendelea kubaki kufundisha chuoni lakini sikutaka nikafungua kampuni ya urembo, wengi walinishangaa wakaniona kama nimechanganyikiwa. Hilo halikunipa shida kwa sababu kichwani mwangu nilijua nini nataka,

maji maji yaibomoa ngome ya lipuli FC


Klabu ya Majimaji imefanikiwa kuipata saini ya mshambuliaji Waziri Ramadhan kutoka Lipuli FC kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Meneja Mkuu wa Majimaji, Geofrey Mvula alisema kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa timu hiyo Peter Mhina alihitaji kufanya usajili wa mshambuliaji pekee ili kukiongezea nguvu kikosi hicho.
"Tumefunga usajili kwa mchezaji huyo pekee na hawa wengine tutaendelea nao kwani tumeona wako vizuri.”
Mvula alisema Ramadhan amefanyiwa uhamisho kutoka Lipuli lakini alikuwa na mkataba na wanapaluhengo nao.

Kumbe Zari na Kajala hawapiki chungu kimoja,,,



Baada ya kuenea taarifa kwa muda mrefu kuwa hawapikiki chungu kimoja, staa wa filamu Bongo, Kajala Masanja amedhihirisha msemo huo baada ya kumkimbia ukumbini mjasiriamali maarufu Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Kwa mujibu wa chanzo kilichokuwepo eneo la tukio hilo lililojiri katika Ukumbi Cardinal Rugambwa Hall maeneo ya Oysterbay hivi karibuni, Kajala alikuwa mmoja kati ya mastaa waalikwa katika sherehe ya harusi na alipofika ukumbini alikaa siti ya nyuma.
“Hatukuwa tukijua kama Kajala naye amealikwa. Aliingia ukumbini na kusalimiana na mastaa wenzake kadhaa kisha akaenda kuketi siti ya nyuma kabisa akifuatilia sherehe inavyoenda,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo kiliendelea kupenyeza ubuyu kuwa, wakati shangwe zikiendelea ukumbini hapo ilifika muda wa kufungua shampeni ambapo mastaa kibao walienda mbele akiwemo msanii wa Bongo Fleva pamoja na mzazi mwenziye, Zari na baada ya muda MC alimuita Kajala naye ajumuike nao.
“Hapo ndipo Kajala akaona isiwe tabu, akainama na kupitia mlango wa nyuma kisha akaondoka zake na kuwaacha na mshangao,” kilimaliza chanzo.
Akizungumzi ishu hiyo Kajala alisema “Ni kweli nilikwenda kwenye hiyo harusi na nikaitwa mbele lakini niliamua kuondoka zangu kwa sababu sikutaka kuonana na baadhi ya watu (Zari).”

Mwarubaini ni mti Wenye kutibu maradhi mbali mbali,,



KATIKA karne hii ya sayansi na teknolojia, Mwenyezi Mungu amewajaalia baadhi ya wanadamu (Madaktari) kuwapa taaluma (elimu) ya kufahamu maradhi yanayosumbuwa wanaadamu wenzao kwa kutumia vifaa mbalimbali ikiwemo vya kisasa na dawa katika kuwatibu.Hata
hivyo uwezo wa aina hii ulikuwepo hata kabla ya kuja sayansi na teknolojia ambapo binadamu wa awali alitumia tiba za asili kwa kujitibu na maradhi ya aina mbalimbali.Hivi sasa toka kuwepo sayansi na teknolojia, asilimia kubwa ya watu wanadharau kutumia dawa za asili na
badala yake wameelemea sana katika matibabu ya dawa za kemikali.Kwa mtazamo, takribani miti yote iliyopo duniani ni dawa hivyo ni vizuri kwa jamii kuelimishwa ili kuweza kujuwa ni jinsi gani wataweza kuitumia miti hiyo kwa kuitibu miili yao.Kutokana na hali hiyo na matibabu
hayo, inaonekana wazi kuwa mti wa Muarubaini ama wengine huita Mtunda, ni mjarabu kwakutibu maradhi mbalimbali na hivyo upo umuhimu wa kila mtu kuupanda katika makaazi yake na pia kwa kupitia Wizara ya kilimo kutenga eneo maalum kwa ajili ya kupanda miti ya
aina hii.Mti wa Mwarubaini ambao kwa kiingereza unajulikana kama ‘Neem’ , ulianza kugunduliwa kama tiba ya maradhi zaidi ya miaka 4.000 iliyopita.Mti huu hutibu maradhi ya aina mbalimbali kwa kuanzia mizizi, magome, mbegu na majani yake.Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa
baraza la tiba asilia Zanzibar Mayasa Salum Ali, alisema mti wa Mwarubaini unapatikana au unaota zaidi katika nchi za joto kote Ulimwenguni.Mwenyekiti huyo ambae pia ni mtaalam wa fani hiyo alisema kwa upande wa watu wa India, kwao mti huu unasifa sana katika matibabu yao na unajulikana kama duka la dawa la kijiji.Aidha alifahamisha kuwa wanauthamini kama dawa kutokana na matibabu yake
kwani unatibu maradhi ya aina mbalimbali ambayo humuandama mwanadamu na hata wanyama na mimea ya shambani.Hata hivyo kwa upande wa wataalamu wa India kutokana na umuhimu wa dawa hizi za asili, wamefakiwa kutengeneza bidhaa mbalimbali kupitia mti huu ili kurahisisha matumizi ya watu kwa kupitia tiba ya mwarubaini.Bidhaa hizo ni pamoja na dawa za kumeza, dawa za mswaki, sabuni, vipodozi
vya aina mbalimbali kama vile krimu, mafuta ya kujipaka ‘lotion’ , majani ya chai na vitu vingine vingi.China nayo haipo nyuma katika kutumia dawa za mti huu kwani nao wameweza kutengeneza bidhaa za aina mbalimbali ili kurahisisha matumizi.Kwa upande wa Zanzibar,
sehemu ndogo sana ambayo inatumia mti huu kama ni dawa ya malaria na sehemu hiyo ni kwa wale watu wazima wanaoishi vijijini. Wao kidogo wanatumia mti huu kama ni dawa ya kutibu malaria sugu huku ikiwa mti wa Mwarubaini unatibu maradhi ya aina mbalimbali.Watu wengi husikia wakisema kuwa Mwarubaini ni dawa ambayo inatibu maradhi arobaini (40) kumbe sivyo ilivyo kwani mti huu unatibu zaidi ya
maradhi arubaini lakini tu jamii haijui na haina utaalam wa kufahamu kwa maradhi mengi yanayotibiwa kwa kutumia mti huo.Hivyo upo umuhimu kwa upande wa wataalamu wa tiba asilia kutoa elimu hiyo kwa jamii ili kuweza kujuwa kutumia mti huo ili kuweza kuondokana na maradhi ya aina mbalimbali.Kutokana na ufahamu huo mdogo kwa Wazanzibari katika tiba zinazopatikana kutokana na Mwarubaini, wengi
wanapoumwa na maradhi ya aina mbalimbali na hata malaria hukimbilia hospitali kupata dawa za vidonge au sindano vitu ambavyo hutokana na mchanganyiko wa kemikali mbalimbali ambazo zinauwezo wa kusababisha madhara makubwa kwa mwili wa mwanadamu.Miongoni mwa dawa ambazo zina madhara yanayoweza kumpata mwanadamu ambayo husababisha na vidonge au sindano
hizo ni pamoja na Fansida au Chloroquine ambapo utafiti unaonesha kuwa baadhi ya wagonjwa waliotumia dawa hizo wameathirika aidha kwa kuwashwa na mwili na wengine wameathirika na macho kwa kutumia Fansida.Ili kuondokana na athari kama hizo, Mwenyekiti huyo amewashauri Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kutumia dawa za asili ili kuondokana na matatizo kama hayo.Hata hivyo Mwenyekiti
huyo alifahamisha kuwa katika baadhi ya maradhi badala ya kutumia pesa nyingi kwa kununua dawa za kemikali ambazo bei zake zinapanda siku hadi siku ukilinganisha na dawa za asili ambazo bei zake ni nafuu.Hata hivyo aliwashauri wagonjwa kufuata ushauri wa kitaalamu kabla ya kutumia dawa hizo ili kuzidi kuboresha afya na kujiepusha na matatizo yasiyo ya lazima.Majani ya mti wa Mwarubaini
yanatumika kwa kutibu maradhi mbalimbali kama vile homa za watoto, suruwa na kwa upande wa watu wazima hutibu malaria, muwasho, maradhi ya moyo, Ukimwi, mkanda wa jeshi na maradhi ya buba.Mengne ni maradhi ya ganzi ya mwili, kisukari na mtu ambae anaupungufu
wa kinga mwilini, mapele sugu yalioshindikana kutibika hospitali na maradhi mengine.Dk. Mayasa pia alifahamisha majani hayo yanauwezo wa kuuwa hata kwa upande wa wadudu wa shambani ambao wanakula mazao.Mbegu za Mwarubaini zinatengenezwa mafuta ambayo
mafuta hayo yanajulikana kwa jina la (Neem oil) ambayo yanauwezo wa kutibu maradhi ya aina mbalimbali kama vile kuondoa chunusi, mapele, fangasi na mabaka mwilini.Pia mafuta hayo huuwa wadudu mbalimbali ambao wanatambaa na kuruka nyumbani na hata vijidudu
(bacteria), sisimizi na wadudu wengine.Mizizi na magome ya mwarubaini huuwa wadudu wa aina mbalimbali kama vile funza, maradhi ambayo huwapata wanawake kama vile vikanga na maradhi mengine mengi ambayo ni maradhi sugu na yameshindwa kutibiwa basi
Mwarubaini huyatibu.“Kwani hata wanyama tunaofuga nyumbani mfano ng’ombe na wengine ambao hugandwa na kupe na wadudu wengine, mnyama huyo ukimkogeshea maji hayo uliosaga magome ya mti huo huondoa wadudu wote”, alifahamisha dk. Mayasa.Mtaalamu huyo alifahamisha kuwa dawa za mti huo hazina madhara kama zilivyo dawa nyengine za kemikali lakini kwa ushauri unatakiwa kumuona
Daktari mwanzo alio karibu nawe kabla ya kuanza kutumia.Alifahamisha kuwa dawa za kemikali zinatibu haraka kuliko dawa za asili lakini dawa za asili ni bora zaidi kuliko dawa za kemikali kwani zinatibu kidogo kidogo na zikitibu zimetibu na hazina maradhi yanayosababishwa na dawa hizo.

Figo kushindwa kufanya. kazi ( RENAL/KIDNEY FAILURE )



Figo ni miongoni mwa viungo muhimu sana katika mfumo wa utendaji kazi wa mwili wa binadamu. Kwa kawaida, mwili wa binadamu una figo mbili zenye maumbo yanayofanana kama yale ya maharage, yakiwa yamejificha nje ya utando unaozunguka tumbo, chini kidogo ya mbavu za chini.
Kazi za figo
Kazi kuu za figo ni kuchuja vitu mbalimbali pamoja na sumu kadhaa katika damu na hivyo kusaidia katika kuhifadhi na kuthibiti kiwango cha maji na madini (electrolytes) mwilini. Katika kutekeleza hayo, figo huchuja vitu hivyo pamoja na maji yaliyo mwilini na kutengeneza mkojo, huchuja pia maji yasiyohitajika mwilini huku yakinyonya madini na kemikali muhimu kuzirudisha katika mzunguko wa damu na kutoa nje uchafu usiohitajika.
Kazi nyingine za mafigo ni
Kurekebisha na kuthibiti kiasi cha vitu mbalimbali katika damu pamoja na kiasi cha maji katika mwili.
Husaidia kutengeneza kiasili cha erythropoietin ambacho ni muhimu sana katika utengenezaji wa chembe nyekundu za damu.
Husaidia uzalishaji wa vitamini D
Husaidia pia katika kuthibiti na kurekebisha shinikizo la damu mwilini (blood pressure)
Utengenezaji wa mkojo
Kwa kawaida damu inayozunguka mwilini hatimaye huingia kwenye figo kwa ajili ya kuchujwa, kutoa uchafu pamoja na sumu nyingine zisizohitajika mwilini. Kitendo hiki cha utengenezaji mkojo hufanyika katika hatua kuu zifuatazo;
Hatua ya kwanza ni uchujaji. Damu kutoka nje huingia ndani ya mafigo na kupita kwenye glomeruli, lenye umbo kama chekeche/chujio ambalo limeundwa na mishipa mingi midogo ya damu iliyojizungusha pamoja. Vitu mbali mbali, maji pamoja na sumu zilizo katika damu inayopita kwenye vimishipa hivi na kisha kuingia katika mirija mingine mikubwa kwa ajili ya uchujaji zaidi.
Mirija inayofuata huendelea kuchuja damu na kunyonya baadhi ya vitu vilivyo chujwa kimakosa kuvirudisha mwilini, mpaka kiasi sahihi cha uchafu kinachotakiwa kuchujwa kinapokuwa kimefikiwa.
Mara baada ya mkojo kutengenezwa na kutolewa kwenye figo, husafiri kuingia kwenye kibofu cha mkojo kwa kupita kwenye mirija ijulikanayo kama ureta. Kutoka kwenye kibofu, mkojo hutolewa nje ya mwili kupitia kwenye mrija waurethra.
Figo kushindwa kufanya kazi (Renal Failure/ Kidney Failure)
Kushindwa kufanya kazi kwa figo hutokea iwapo sehemu ya figo au figo lote litapoteza uwezo wake wa kuchuja maji na uchafu kutoka katika damu na kutengeneza mkojo. Kitendo hiki husababisha kusanyiko la uchafu pamoja na sumu kadhaa katika damu ambazo ni hatari kwa afya ya mhusika.
Aina za figo kushindwa kufanya kazi
Figo kushindwa kufanya kazi kumeganyika katika makundi yafuatayo
Figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla (Acute Renal Failure (ARF) au Acute Kidney Failure (AKF).
Figo kushindwa kufanya kazi kwa kiasi (Mild renal/kidney insufficiency)
Tatizo sugu la figo kushindwa kufanya kazi (Chronic renal failure)
Figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla (Acute Renal Failure (ARF)
Hii ni hali inayotokea kwa ghafla, na kudumu kwa saa chache mpaka siku chini ya 14, na kusababisha ongezeko la kiwango cha creatinine na urea katika damu. Hali hii huwapata karibu asilimia 5% ya wagonjwa waliolazwa hospitali kwa sababu ya matatizo mbalimbali. Aidha hali hii hutokea zaidi kwa wagonjwa mahututi na wale wanaohitaji uangalizi wa kipekee, yaani waliolazwa ICU.
Katika makala hii tutatumia zaidi kifupisho cha ARF.
Visababishi na aina za ARF
Visababishi (au aina) vya ARF vinaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu:
Matatizo yanayoathiri mtiririko wa damu kabla ya kuingia katika figo (Prerenal causes/failure)
Matatizo ndani ya figo lenyewe yanayozuia na kuathiri uchujaji wa damu au uzalishaji wa mkojo (Renal causes/failure)
Matatizo yanayoathiri mtiririko wa mkojo nje ya figo (Postrenal causes/failure)
Matatizo yanayoathiri mtiririko wa damu kabla ya kuingia katika figo (Prerenal
causes/failure)
Aina hii hutokea kwa takribani asilimia 60 mpaka 70 ya ARF zote. Katika kundi hili, figo hukosa damu ya kutosha kwa ajili ya kuchuja na hatimaye hushindwa kufanya kazi yake ipasavyo. Mambo yanayoweza kusababisha prerenal failure ni pamoja na:
Upungufu wa maji mwili unaosababishwa na kutapika kupita kiasi, kuharisha, au kupoteza damu kupita kiasi (kwa sababu ya ajali au kuumia)
Kuvurugika kwa mtiririko wa damu inayoingia kwenye figo kwa sababu ya:
Kushuka kwa ghafla kwa shinikizo la damu kwa sababu ya kupoteza damu nyingi wakati wa upasuaji mkubwa, kuumia au kuungua sehemu kubwa ya mwili, au maambukizi katika mfumo wa damu (sepsis) yanayoweza kufanya mishipa ya damu kutanuka na kushusha shinikizo la damu
Kuziba au kusinyaa kwa mishipa inayopeleka damu kwenye figo
Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure) au shambulio la moyo (heart attack) linalosababisha kushuka kwashinikizo la damu
Ini kushindwa kufanya kazi (liver failure) kunakoweza kusababisha mabadiliko katika mfumo wa homoni zinazoathiri shinikizo la damu pamoja na mtiririko wa damu kwenda kwenye figo.
Mwanzoni kabisa mwa pre-renal failure huwa hakuna athari yoyote inayotokea kwenye figo, na mara nyingi, figo laweza kurudi katika hali yake ya kawaida iwapo chanzo cha tatizo kitagunduliwa na kushughulikiwa ipasavyo.
Matatizo ndani ya figo lenyewe yanayozuia na kuathiri uchujaji wa damu au uzalishaji wa mkojo (Renal causes/failure)
Mambo yanayosababisha madhara katika figo husababaisha karibu asilimia 25 mpaka 40 ya vyanzo vyote vya ARF. Visababishi vilivyo katika kundi hili hujumuisha vile vinavyoathiri uchujaji, mtiririko wa damu ndani ya figo na seli za figo zinazoshughulika na uchujaji na ufyonzaji wa chumvi na maji.
Visababishi hivyo ni pamoja na:
Magonjwa katika mishipa ya damu
Kuwepo kwa damu iliyoganda ndani ya mishipa ya damu inayopita katika figo
Ajali/Kuharibika kwa tishu na seli za figo
Magonjwa ya mzio katika glomeruli na figo kwa ujumla (glomerulonephritis). Magonjwa yanayoweza kusababisha hali hii ni pamoja na maambukizi (infection) ya bacteria jamii ya streptococci.
Magonjwa ya mzio katika nyama za figo (acute interstitial nepthritis). Mambo yanayoweza kusababisha hali hii ni pamoja na matumizi ya baadhi ya madawa kama vile Aspirin, Ibuprofen (Brufen), baadhi ya antibiotics, na baadhi ya dawa za kutoa maji mwilini (antidiuretics); magonjwa kama vile saratani ya damu (leukemia), lupus na lymphoma. Magonjwa ya mzio katika nyama za figo husababisha madhara katika seli zinazohusika na uchujaji na ufynzaji wa chumvi na maji.
Magonjwa ya ukosefu wa damu katika mirija ya figo (acute tubular necrosis) ambayo hufanya seli na tishu za mirija hii kufa na hivyo mirija kushindwa kufyonza chumvi na maji kuyarudisha mwilini. Mambo yanayosababisha hali hii ni pamoja na shock (upungufu wa damu kuingia kwenye figo), matumizi ya madawa kama vile baadhi ya antibiotiki, sumu, dawa zinazotumika viwandani na kwenye x-rays na baadhi ya madawa yanayotumika kutibu saratani.
Matatizo yanayoathiri mtiririko wa mkojo nje ya figo (Postrenal causes/failure)
Mambo yanayosababisha hali hii huchangia kati ya silimia 5 mpaka 10 ya vyanzo vyote vya ARF. Postrenal failure wakati mwingine huitwa pia obstructive renal failure kwa sababu husababishwa na mambo yanayozuia utoaji wa mkojo nje ya figo.
Kuziba kwa ureta moja ama zote mbili kunaweza kusababishwa na:
Vijiwe figo (renal stones)
Saratani ya viungo vya njia ya mkojo au viungo vilivyo karibu na njia ya mkojo kiasi cha kuzuia mkojo kutoka nje ya figo
Matumizi ya baadhi ya madawa
Kuziba kwa njia ya mkojo katika eneo la kibofu cha mkojo kunaweza kutokana na:
Kijiwe kibofu (bladder stone)
Kuvimba kwa tezi dume (hii ni kwa wanaume)
Kuwepo kwa damu iliyoganda katika kibofu
Saratani ya kibofu cha mkojo
Matatizo ya mfumo wa fahamu yanayoathiri utendaji kazi wa kibofu cha mkojo
Tafsiri nyingine ya ARF
Wagonjwa wa ARF wanaweza kupata mkojo kidogo sana au wasipate kabisa., au wanaweza kuwa na ongezeko la creatinine kwa kasi ya kutisha au kwa kasi ndogo sana. Hali hizi zinaweza pia kutumika kutoa tafsiri nyingine ya maana ya ARF.
Mtu anayetoa kiasi cha mkojo chini ya 400mL kwa siku hujulikana kama ana oliguria, na huchukuliwa kuwa ana hali mbaya ya kutoweza kupona.
Mtu anayetoa mkojo chini ya 100mLkwa siku husemwa ana Anuria, ambayo kama imetokea ghafla, huashiria kuwepo kwa tatizo la kuziba kwa mirija inayotoa mkojo kwenye figo zote mbili, na mara niyingi hali hii ni ya hatari zaidi. Tafsiri hii husaidia sana katika kuamua aina ya matibabu na muda wa kumpatia mgonjwa matibabu ili kuepusha madhara zaidi yanayoweza kumpata.
Dalili za ARF
Katika hatua za mwanzo mwanzo, baadhi ya waathirika wanaweza wasioneshe dalili zozote za tatizo hili. Dalili ni kama
Kupungua kwa uzalishaji mkojo
Kuvimba mwili
Kupoteza umakini
kuchanganyikiwa
Uchovu
Kulegea mwili
Kichefuchefu na kutapika
Kuharisha
Maumivu ya tumbo
Kuhisi ladha ya chuma na uchachu mdomoni
Na katika hatua za mwisho kabisa, mgonjwa anaweza kupata degedege na hatimaye kupoteza fahamu (coma).
Vipimo na uchunguzi
Kama ilivyoainishwa hapo juu kuwa baadhi ya wagonjwa wanaweza wasiwe na dalili zozote za tatizo hili. Hata wale wenye kuonesha dalili, zinaweza zisiwe mahsusi (non-specific). Uchunguzi wa mwili unaweza usioneshe tatizo lolote lile, au kukawa na dalili chache sana ambazo zinaweza zisimsaidie sana daktari kufikia uamuzi.
Baadhi ya vipimo vinavyoweza kugundua uwepo wa ARF ni pamoja na Kipimo cha utendaji kazi wa figo (Renal function tests) ambacho husaidia kuchunguza kiwango cha urea (blood urea nitrogen (BUN) katika damu. Aidha husaidia pia kuchunguza ongezeko la kiwango cha creatinine katika damu.
Uchunguzi wa kiwango cha madini mbalimbali katika damu (blood electrolytes)
Uchunguzi wa damu (Full Blood Picture): Husaidia kuonesha uwepo wa maambukizi ya bacteria na/au upungufu wa damu mwilini (anaemia)
Kupima kiasi cha mkojo kinachotolewa na mgonjwa katika masaa 24
Uchunguzi wa mkojo (Urine analysis): Rangi ya mkojo, kiasi cha electrolytes, uwepo wa usaha au damu au casts.
Ultrasound ya figo na kibofu cha mkojo
Renal biopsy.
Matibabu ya ARF
Matibabu ya ARF hutegemea kwanza chanzo chake na pili ukubwa wa tatizo. Kujua chanzo cha tatizo husaidia kufahamu ni aina gani ya matibabu yanayohitajika wakati kufahamu ukubwa wa tatizo huathiri uchaguzi wa aina ya matibabu na hata hitaji la kufanya dialysis. Hata hivyo inashauriwa sana kumpeleka mgonjwa kwa daktari bingwa wa magonjwa ya figo (nephrologist) kwa matibabu zaidi.
Kulingana na chanzo cha ARF, baadhi ya matibabu yanayoweza kufanyika, hutolewa yakiwa na lengo la:
Kurekebisha kiasi cha upotevu wa maji mwilini ambapo mgonjwa hupewa i.v fluids pamoja kurekebisha kiasi cha madini (electrolytes) kilichopotea
Kupunguza au kuzuia ongezeko la maji kwa wagonjwa ambao figo zao zimeshindwa kabisa kutoa maji nje ya mwili
Kuongeza uwezo wa moyo kufanya kazi vizuri au kuongeza shinikizo la damu husaidia kuongeza mtiririko wa damu kwenda kwenye figo
Kurekebisha kiasi cha madini mwilini kitendo ambacho husaidia mwili kufanya kazi zake vema
Dialysis
Iwapo pamoja na matibabu hayo, figo za mgonjwa zinaendelea kudorora, mgonjwa hana budi kufanyiwa dialysis. Dialysis ni kitendo cha kutoa uchafu na maji yasiyohitajika katika damu. Kitendo hiki hufanywa kwa kupitia mishipa ya damu iliyo chini ya ngozi (hemodialysis) au kwa kupitia tumboni (peritoneal dialysis). Katika hemodialysis mirija hii huunganiswa kwenye mashine ambayo hufanya kazi kama figo. Damu kutoka kwa mgonjwa huingia katika mashine kisha huchujwa ili kuondoa sumu, uchafu pamoja na maji yasiyohitajika kabla ya kurejeshwa tena mwilini.
Kitendo hiki hufanyika angalau mara mbili mpaka tatu kwa wiki, na kwa kiasi fulani ni ghali na si watu wote wa kipato cha chini wanaoweza kumudu gharama zake.
Katika peritoneal dialysis, uchafu pamoja na maji kutoka katika mzunguko wa damu huingia katika nafasi inayotenganisha tumbo na utando wake (peritoneal space), huchujwa kwenye utando huo kisha hutolewa kupitia sindano maalum (catheter ) iliyowekwa juu ya ngozi na kuingia ndani ya tumbo (peritoneal cavity).
Matarajio
Wagonjwa wengi wenye ARF hupona bila hata kuhitaji dialysis mara tu chanzo cha tatizo kinapogundulika na kushughuikiwa mapema. Hata hivyo wakati mwingine, pamoja na matibabu, baadhi ya figo hushindwa kurudia kufanya kazi kwa ufanisi wake wa awali. Watu kama hawa hawa wanahitaji kufuatiliwa kwa ukaribu na umakini mkubwa.
Kinga ya ARF
Inashauriwa
kufanya uchunguzi wa figo walau mara moja kila mwaka. Hii husaidia kuchunguza utendaji wa figo na hivyo kuepuka madhara kabla hayajatokea.
Kunywa maji kwa wingi ili kuyafanya mafigo yatende kazi zake kwa ufanisi.
Kuepuka matumizi ya vitu ama madawa yanayoweza kuathiri nyama, seli au tishu za figo. Ni vema kutumia dawa pale tu unaposhauriwa na daktari.
Watu wenye hatari ya kupata tatizo sugu la kushindwa kufanya kazi kwa figo (Chronic Renal Failure) wanashauriwa kufanya vipimo na cuhunguzi mara kwa mara
Muone mtaalamu wa afya mara tu uonapo dalili za kuwepo kwa shida katika kukojoa au uonapo damu katika mkojo.

Cervical Cancer Saratani ya Mlango Wa kizazi



Saratani ya mlango wa kizazi
Hii ni njia ya kizazi kati ya uke na mji wa mamba.Ugonjwa huu ukijulikana mapema unweza kutibiwa, wakati wa kufanyiwa uchunguzi wa ubwabwa na fupa nyongo.
Nani yumo hatarini
Wanawake wengine wamo hatarini mwa kupata saratani ya mlango wa kizazi:
Wanawake wasioenda kwa uchunguzi wa kila mwaka wa fupa nyongo na ubwabwa
Wanawake walio na “human papillomavirus” HPV au genital warts
Kuvuta sigara, kuwa na ukimwi,na kutokula vyakula bora huweza kusababisha saratani ya mlango wa kizazi.
Dalili ya saratani ya mlango wa kizazi
Hamna dalili zozote mpaka unaposambaa nje ya mlango wa kizazi.
Hali hii ikitokea waweza kuwa:
Kuvuja damu katikati ya siku za hedhi, unaposhiriki ngono au baada ya hedhi kukatika
Kuvuja damu nyingi zaidi ya kawaida.
Ukiona dalili hizi pata ushauri wa daktari.
Saratani ya Utumbo Mpana na Sehemu za Siri za Nyuma
Saratani ya sehemu za siri za nyuma zipo. Huambukiza sehemu za mmeng’enyo (digestive system) wa chakula. Watu wengi wanaopata ugonjwa huu ni wa umri wa zaidi ya miaka 50.
Matibabu yake yameimarika, lakini ni vyema kugundua mapema.Watu wanahitaji kufahamu madhara, dalili na umuhimu wa kupimwa na madaktari wao.
Walio hatarini kupatwa na saratani ya utumbo mpana:
Ajuza wa miaka 50 na zaidi.
Wanaokula vyakula vya mafuta mengi
Walio na maoteo (ndani ya utumbo mpana )
Wanawake ambao washaugua saratani ya matiti, au mji wa mimba au yai la mwanamke
Aliye wahi kuugua saratani ya utumbo mpana
Aliye na mzazi, jamaa au motto aliye na saratani ya utumbo mpana
Aliye na utumbo mpana wenye kiungulia (donda au uvimbe)
Dalili za saratani ya utumbo mpana ni:
Kuvimbiwa, kusokotwa au kujihisi tumbo limejaa sehemu ya chini
Kuhara, kufunga choo au kujihisi haukamilishi haja kabisa
Damu katika kinyesi
Kinyesi chembamba zaidi
Kupoteza uzito bila ya kufahamu kisababu
Kujihisi mchovu kila wakati
Kutapika
Hizi dalili zinaweza kusababishwa na shida nyingine ambazo si saratani. Muulize daktari wako ili ufahamu
Saratani ya Mapafu
Saratani ya mapafu ndio aina hatari ya magonjwa ya saratani, lakini ndio rahisi kuzuia.Uvutaji wa sigara husababisha asilimia 9% kwa 10% ya kesi za ugonjwa huu.Matibabu ya ugonjwa huu yameimarika lakini bado hakuna tiba.Ili kuimarisha afya yako na walio karibu yako usivute sigara.
Pia hakikisha nyumba yako haina 'radon' gesi hatari isababishayo saratani ya mapafu.
Watu wengine wamo hatarini zaidi ya kupata saratani ya mapafu.
Wanaovuta sigara au kiko, na hata usipo vuta moshi ndani, umo hatarini kupata saratani ya domo. Kukaa karibu na mvutaji sigara au kuishi naye ama kufanya kazi katika mazingira yenye moshi huongeza hatari hasa kwa watoto wasio na namna.
Kiwango kingi cha madini ya radon nyumbani mwako.
Kufanya kazi karibu na asbestos, aseniki, uranium au bidhaa kutokana na mafuta.
Kuwa na kifua kikuu.
Ishara ya saratani ya mapafu ni nini?
Kikohozi kisicho kwisha.
Kuumwa na kifua.
Kukohoa damu
Shida ya kupumua au kukorota upumuapo
Nimonia(kichomi) au mkamba usiyokwisha
Uvimbe shingoni au usoni.
Kupoteza uzito wako bila sababu au kutohisi njaa.
Kujihisi mchovi kila wakati.
Ukiwa na mojawapo ya dalili hizi, hasa ikiwa umo hatarini ya kupata huu ugonjwa, mwone daktari.
Saratani ya Mdomo
Saratani ya mdomo husambaa kinywani kwenye ulimi, ufizi, kidakatonge na koromeo.Watu hawatambui ugonjwa huu upesi.Wanaovuta sigara,kuvuta tumbako au kunywa kunywa pombe wamo hatarini mwa kupata sratani yam domo.Unaweza kusaidiwa ili kuwacha sigara au pombe.Ugonjwa huu unaweza kitibiwa ukiuwahi mapema.
Ishara ya saratani ya Mdomo ni kama zifuatazo;
Uvimbe sehemu yoyote mdomoni, ambao hauponiau kutokuwa na damu kwa urahisi.
Kuhisi uchungu au kufa ganzi mdomoni.
Kuhisi uchungu unapo tafuna, kumeza chakula ulimi unapotumika au taya.
Kubadilika kwa sauti yako.
Kuumwa na sikio.
Koo linalowasha bila kupona.
Ukiwa na ishara hizi mwone daktari haraka sana.

Waziri kalemani awawashia moto watendaji Wa TANESCO kanda ya kusini akataa kupokea taarifa ya meneja Wa REA


Na. Ahmad Mmow. WAZIRI wa nishati, Merdard Kalemani jana aliwajia juu watendaji wa TANESCO kanda ya kusini. Huku akikataa kupokea taarifa ya meneja wa wakala wa umeme vijijini(REA), mkoani Lindi, Jackson Lawuo, nakumtaka naibu mkurugenzi mkuu wa TANESCO amchukulie hatua meneja wa TANESCO mkoa wa Lindi.
Kalemani alifikia uamuzi huo kutokana na kutoridhirishwa na hali ya mambo na utendaji wa shirika hilo katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Miongoni mwa sababu zilizosababisha akatae kupokea taarifa ya meneja wa wakala wa umeme vijijini ni kuchelewa kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini katika awamu ya tatu mkoani humu.
Kuhusu meneja wa TANESCO mkoa wa Lindi, Johnson Mwigune, waziri Kalemani amemuagiza naibu mkurugenzi mkuu wa TANESCO amchukulie hatua meneja huyo kutokana na kutoridhirishwa na utendaji wake. Hasa kwakushindwa kutoa taarifa kwa wakati kwa waziri mwenye dhamana ya nishati kuhusu hali ya umeme na kuchelewa kuanza utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijiji awamu ya tatu.
Waziri huyo licha ya kumuagiza naibu mkurugenzi huyo, lakini pia alimtaka meneja huyo ahakikishe anamsimamia mkandarasi wa usambazaji umeme vijijini aharakishe zoezi la usambazaji. Huku akiagiza utekelezaji wa mradi huo uanze ndani ya mwezi huu katika vijiji Vilivyopo kwenye mpango huo.
Waziri Kalemani aliyetoa maagizo hayo jimboni Mtama wilaya ya Lindi ameutaka pia uongozi wa TANESCO kanda ya kusini uhakikishe unarekebisha miundombinu ya umeme ndani ya siku tatu. Ikiwamo nguzo za umeme. Akibainisha kuwa tatizo la nguzo linachangia kukosekana upatikanaji umeme kwa uhakika katika baadhi ya maeneo. Japokuwa mashine zakufua umeme zimetengenezwa.
"Umeme unakatika mara kwa mara licha ya mashine kukarabatiwa nakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 15.8 ambazo zingekidhi mahitaji ya mikoa hii ya Lindi na Mtwara, "alisema Kalemani.
Awali mkuu wa mkoa Lindi, Godfrey Zambi katika taarifa yake kwa waziri huyo alieleza kutoridhishwa na utoaji taarifa sahihi za hali ya upatikanaji umeme mkoani humu. Huku tatizo la umeme likiendelea kuwaathiri wananchi, taasisi za umma nakukwamisha shuguli za maendeleo na kiuchumi mkoani humu.

Balozi alnajem amkabidhi diwani bharwani wa vigwaza vifaa vya mil. 4.5



Na Omary Mngindo, Vigwaza
BALOZI wa Kuwait nchini Tanzania Jasem Alnajem amemkabidhi Diwani wa Kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze Alhaj Mohsin Bharwani mabeseni 100 yenye thamani ya sh. Mil. 4.5 yatayotumika kwa wajawazito wataofika kujifungulia kwenye Zahanati iliyopo Kijiji cha Vigwaza.
Mabeseni hayo yenye sabuni, poda na vifaa vyote muhimu kwa ajili ya matumizi ya mtoto anayezaliwa ni sehemu ya vifaa ambavyo mpango wake ulizinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassani Suluu kwa kushirikiana na Ubalozi huyo wa Kuwait.
Akizungumza na wananchi hao, Balozi Alnajem kwanza alielezea furaha yake ya kufika Vigwaza kukutana na wakazi hao, pia ameangalia madhari ya eneo hilo huku akisema kuwa kufika kwake Vigwaza kumetokana na juhudi za Diwani huyo kumtafuta ofisini kwake kisha kumwelezea changamoto zinazowakabiri wananchi waishio Kijiji cha Vigwaza na Kata hiyo kwa ujumla.
Aliongeza kuwa amefika Vigwaza lengo kusaidia Mama na mtoto na wananchi si kujitangaza na kuwa hatua hiyo imetokana na kuguswa na changamoto alizoelezwa na Diwani wao, pia ataendelea kusaidi sekta ya afya na elimu huku akisisitiza misaada iwafikie walengwa wa mpango huo na kuwa uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Kuwait utaendelezwa kwa maslahi ya nchi na watu wake.
Kwa upande wake akizungumza baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo, Bharwani alianza kwa kumsukuru Balozi kwa msaada huo unaolenga kuwasaidia mama wajawazito wanaojifungulia katika Zahanati hiyo huku akisema utakuwa msaada walengwa wanaofika kwa ajili ya kupata huduma hiyo na kwamba anaimani vitatumika kama malengo yalivyokusudiwa.
"Mabeseni haya mabeseni 100 yatawasaidia wajawazito kabla ya kujifungua na baada ya kujifungua vyote vinagharimu kiasi cha sh. Mil. 4.5, hii ni sehemu ya mpango uliozinduliwa na Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluu kwa kushirikiana na Ubalozi wa Kuwait hapa nchini nasi Vigwaza tumeambulia msaada huu" alisema Bharwani.
Aidha Diwani huyo aliongeza kuwa mbali ya vifaa hivyo pia Balozi kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu amezindua mpango mwingine unayogusa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), miguu, mikono pamoja na wasioona ambapo amekabidhi miwani, magongo, baskeli yenye mataili manne pamoja na mafuta kwa wenye ulemavu wa ngozi vyote vikiwa na thamani ya sh. Mil. 13.
"Nilipokutana na Balozi nilimgusia mambo mbalimbali yakiwemo sekta za maji, afya pamoja na elimu ambazo sisi wana-Vigwaza bado tunauhitaji mkubwa wa huduma hizo kutoka kwa wadau, katika kufanikisha hili la leo namshukuru sana ndugu yangu Muna amenipatia ushirikiano mkubwa, asingekuwa yeye nisingeonana na Balozi," alisema Diwani huyo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Thomas Mollel alielezea shukrani zake kwa Balozi huyo kwa kuona umuhimu wa kufika ndani ya wilaya hiyo huku akisema misaada hiyo itatumika kama ilivyokusudiwa huku akiwaomba wataosimamia zoezi hilo kuhakikisha wanalitekeleza kwa walengwa na si vinginevyo.

Friday 15 December 2017

Yanga na Timu ya Polisi kucheza Jumapili badala ya Jumamosi

Mechi ya kirafiki iliyopangwa kuchezwa kesho Jumamosi kati ya Yanga na Polisi Tanzania itachezwa keshokutwa Jumapili.

Awali, mechi hiyo ilipangwa ichezwe kesho Jumamosi maalumu kwa Yanga kuangalia nyota wake baada ya kufanya mazoezi.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata salehjembe, mechi imehairishwa kuchezwa mechi hiyo iliyopangwa ichezwe Uwanja wa Taifa kutokana na nyasi kufyekwa bila ya viwango ambazo ni fupi zaidi.

Meneja Mkuu wa Yanga, Hafidh Saleh alithibitisha hilo kwa kusema kuwa "Mechi yetu tuliyopanga tucheze kesho Jumamosi itachezwa Jumapili na siyo Jumamosi kama tulivyopanga baada ya kutokea matatizo.

Guardiola aweka rekodi kushinda tuzo ya kocha bora

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameendelea kuweka rekodi katika ligi kuu ya soka nchini England (EPL) baada ya kushinda tuzo ya kocha bora wa mwezi Novemba.


Kwa kushinda tuzo hiyo leo, Guardiola sasa ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kuchukua tuzo hiyo mara tatu mfululizo. Mhispania huyo ameshinda katika miezi ya Septemba, Oktoba na Novemba ambayo ameshinda leo.

Pep amechukua tuzo hiyo leo akiwashinda waliokuwa wapinzani wake kwenye kuwania tuzo hiyo Antonio Conte, Sean Dyche, Jurgen Klopp, Jose Mourinho na Arsene Wenger.

Jumatano wiki hii Pep aliweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kushinda michezo 15 mfululuizo kwenye EPL na kuzikaribia rekodi zake mwenyewe ambazo amewahi kuziweka kwenye ligi za La Liga (16) na Bundesliga (19).

Ulega akamata tani 11 za samaki wakiandaliwa kusafirishwa nje

Mwanza. Naibu Waziri wa Uvuvi, Abdalla Ulega, leo Ijumaa amefanya ziara ya kushtukiza katika soko la kimataifa la samaki la Kirumba jijini Mwanza na kukamata tani 11 za samaki waliokuwa wakiandaliwa kusafirishwa nje ya nchi kinyume cha sheria.

Shehena hiyo ya samaki  ambao hawaruhusiwi kuvuliwa kisheria, wanadaiwa kuwa walitaka kusafirishwa kwenda nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) kupitia mpaka wa Rusumo mkoani Kagera.

Pamoja na kukamata samaki hao, naibu waziri huyo pia ameagiza kuondolewa mara moja kutoka sokoni hapo maofisa uvuvi kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela waliokuwa na dhamana ya kusimamia ukaguzi katika soko hilo kwa kushindwa kutimiza wajibu.

Iniesta hana tatizo na Neymar kwenda Madrid

KIUNGO mkongwe wa Barcelona, Andres Iniesta amesema hana hofu kuhusu Neymar kujiunga na Real Madrid lakini akakiri kuwa ikitokea hivyo haitampendeza kutokana na uhusiano wa Neymar na mastaa wengine wa Barcelona wakati alipokuwa akiichezea timu hiyo.

Iniesta amecheza na Neymar kwa miaka minne kabla ya mchezaji huyo kuondoka na kuhamia Paris Saint- Germain lakini kumekuwa na taarifa za kuwaniwa kwa ukaribu na Real Madrid.
 “Chochote kinaweza kutokea kwenye soka, kuna mambo ambayo yalionekana ni magumu kutokea na yakatokea, sitashangaa lakini haitapendeza kwa kuwa kwa kuwa ni mchezaji mzuri lakini sina hofu,” alisema Iniesta.

Mwenyekiti wa zamani wa CCM apata dhamana

Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano wamefanikiwa kupata dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Ni baada ya Wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro kuwasilisha cheti kutoka Kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambapo kimeipa mamlaka mahakama hiyo ya Kisutu kusikiliza kesi hiyo.

Hata hivyo, washtakiwa hao walisomewa mashtaka mapya matano mahakamani hapo leo Ijumaa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa.

Katika mashtaka hayo mawili ni ya kusambaza dawa bandia za kufubaza makali ya ukimwi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, uzembe wa kuzuia kosa kutendeka na kusababisha hasara.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa walikana na wapo nje kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wanaominika, kila mdhamini akisaini bondi ya Sh 12 milioni.

Pia washtakiwa hao watoe fedha taslimu Sh 12 milioni ama mali isiyo hamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.
Facebook Tw

Diamond azidi kukimbiza Afrika Mashariki


Wakati wimbo mpya wa Diamond Platnumz aliomshirikisha Rapper Rick Ross kutoka Marekani unatoka haukuwa na nguvu kubwa pengine kutokana na kuahirishwa kwa tarehe iliyotakiwa kutoka video ya wimbo.

Lakini hiyo haikuwa kigezo kikubwa kwa wimbo huo wa ‘Waka’ kwani ndani ya siku tatu ulikuwa tayari umefikisha views milioni 1.

Ukweli ni kwamba ‘Waka’ ulipata mapokezi ya kawaida ukilinganisha na nyimbo nyingine za Diamond Platnumz kama Hallelujah, Salome, Kidogo n.k , Lakini kitu cha kushangaza wimbo huo kadri siku zinavyozidi kwenda ndio unazidi kutazamwa zaidi sio tu Tanzania bali na nchi nyingine za Afrika Mashariki.
 

Diamond azidi kukimbiza Afrika Mashariki


Wakati wimbo mpya wa Diamond Platnumz aliomshirikisha Rapper Rick Ross kutoka Marekani unatoka haukuwa na nguvu kubwa pengine kutokana na kuahirishwa kwa tarehe iliyotakiwa kutoka video ya wimbo.

Lakini hiyo haikuwa kigezo kikubwa kwa wimbo huo wa ‘Waka’ kwani ndani ya siku tatu ulikuwa tayari umefikisha views milioni 1.

Ukweli ni kwamba ‘Waka’ ulipata mapokezi ya kawaida ukilinganisha na nyimbo nyingine za Diamond Platnumz kama Hallelujah, Salome, Kidogo n.k , Lakini kitu cha kushangaza wimbo huo kadri siku zinavyozidi kwenda ndio unazidi kutazamwa zaidi sio tu Tanzania bali na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Kwa sasa wimbo wa ‘Waka’ unaweka rekodi ya kuwa wimbo wa kwanza kutrend namba moja kwa nchi tatu za Afrika Mashariki kwenye mtandao wa YouTube.

Video hiyo mpaka jana usiku ilikuwa ndiyo video inayotazamwa zaidi mtandaoni (Trending) kwa kushika namba moja kwa nchi za Kenya, Uganda na Tanzania.

Wimbo wa ‘Waka’ awali ulipotoka ulikaa siku mbili kwenye mtandao wa YouTube hapa Tanzania  bila kukaa kwenye namba 1 ya video zinazotrend hapa nchini. Lakini mpaka sasa video ya wimbo huo yenye siku saba mtandaoni ipo namba moja kwenye Trending.

Awali rekodi ya video iliyotrend namba 1 kwa nchi mbili tofauti tofauti ilikuwa ilikuwa inashikiliwa na video ya wimbo wa ‘Zilipendwa’ wa WCB , Salome ya Diamond Platnumz na Video ya wimbo wa ‘Seduce Me’ wa Alikiba ambapo video zote wakati zinatoka zilishika namba moja Tanzania na Kenya kwa muda tofauti tofauti.

Komando Jide azidi kudata na Spicy


BAADA ya mwanadada ‘lejendari’ kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ kufanya vyema na Ngoma ya Together Remix akiwa na mpenzi wake, Spicy, staa huyo amejipanga kutengeneza naye ngoma tena.




BAADA ya mwanadada ‘lejendari’ kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ kufanya vyema na Ngoma ya Together Remix akiwa na mpenzi wake, Spicy, staa huyo amejipanga kutengeneza naye ngoma tena.

 Akizungumzia stori hiyo, Jay Dee alisema kwamba ameamua kurudi tena na Spicy na ngoma mpya ya Baby baada ya kolabo ya Together Remix kufanya vizuri ambapo anaamini itampeleka mbali zaidi kimuziki kuliko alipo kwa sasa.


“Nimeamua kumganda Spicy kwa sababu ninaamini ni mwanamuziki mzuri na muungano wetu huwa unafanya vizuri, angalia ngoma iliyopita na hii utagundua kwamba tunapokuwa pamoja tunatengeneza kitu kizuri sana,”alisema Spicy.

 Akizungumzia stori hiyo, Jay Dee alisema kwamba ameamua kurudi tena na Spicy na ngoma mpya ya Baby baada ya kolabo ya Together Remix kufanya vizuri ambapo anaamini itampeleka mbali zaidi kimuziki kuliko alipo kwa sasa.

Mugabe ajitokeza hadharani kwa mara ya kwanza








Mugabe ajitokeza hadharani kwa mara ya kwanza

Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza  tangu awasili wiki hii nchini Singapore kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.

Kiongozi huyo aliyekuwa  madarakani kwa miaka 37 ameonekana akiwa amezungukwa na walinzi wake huku kwa mbele akionekana mwanamke ambaye inaaminika atakuwa mke wake, Grace Mugabe.

Picha za tukio hilo zinamwonyesha akiwa amevalia shati jeupe na suruali nyeusi wakati mtu anayedhaniwa kuwa mke wake akiwa katika vazi jekundu na beki ya mkononi lenye rangi ya zambarau.










Mugabe ajitokeza hadharani kwa mara ya kwanza

Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza  tangu awasili wiki hii nchini Singapore kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.

Kiongozi huyo aliyekuwa  madarakani kwa miaka 37 ameonekana akiwa amezungukwa na walinzi wake huku kwa mbele akionekana mwanamke ambaye inaaminika atakuwa mke wake, Grace Mugabe.

Picha za tukio hilo zinamwonyesha akiwa amevalia shati jeupe na suruali nyeusi wakati mtu anayedhaniwa kuwa mke wake akiwa katika vazi jekundu na beki ya mkononi lenye rangi ya zambarau.

Walinzi wake pia wameonekana kuvalia katika hali ya kawaida ikiwa mashati na suruali. Mara nyingi Mugabe pamoja na walinzi wake wa karibu huonekana wakiwa wamevalia suti isipokuwa wakati alipokuwa akishiriki shughuli za chama au katika sherehe za uhuru.