Friday, 29 December 2017

Yanga yatua Mwanza Salama, kuivaa Mbao FC


Kikosi cha Yanga kimetua salama Mjini Mwanza tayari kwa pambano lake la Jumapili dhidi ya wenyeji Mbao FC, pambano la Ligi Kuu ambalo limepangwa kupigwa uwanja wa CCM Kirumba.

Kocha msaidizi wa timu hiyo Shadrack Nsajigwa amesema, timu imewasili salama na leo wanatarajia kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Kirumba, pamoja na kesho kabla ya kujiandaa na mchezo huo ambao wameupa umuhimu mkubwa.

“Nashukuru tumewasili salama Mwanza, hali ya hewa ni nzuri na kufika mapema siku mbili kabla ya mchezo kutatusaidia kufanya vizuri kwenye mchezo wetu wa keshokutwa kwasababu tumedhamiria kushinda mchezo huo ukizingatia Mbao ni timu nzuri na imeuwa ikitusumbua sana,” amesema Nsajigwa.

Kocha huyo amesema ukitoa wachezaji Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa wachezaji wote waliobaki na kusafiri na timu hiyo niwazima na wapo katika ari kubwa ya kuhakikisha wanacheza na kuhakikisha wanapata pointi tatu.


Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, ikiwa na pointi 21, huku mahasimu wao Simba wakiwa ndiyo vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 23 huku Azam FC wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi sawa na Simba.

VIDEO: Rais Magufuli amwagiwa sifa na Sheikh Kishki


Mhadhiri wa Kimataifa wa Kiislamu, Sheikh Nurdeen Kishki amemmwagia sifa Rais wa DK John Magufuli kutokana na uamuzi wake wa kupiga vita uvaaji wa nguo zisizo na maadili katika video za muziki nchini.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI..USISAHAU KUSUBSCRIBE




VIDEO: KAKOBE Aendelea Kupeta Mtaani



Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amefunguka na kusema kuwa jeshi la polisi mpaka sasa halijamkamata Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zakaria Kakobe kama baadhi ya taarifa zinavyosamabazwa.

Kamanda Mambosasa amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa bado hawajamtia nguvuni Askofu huyo na pindi watakapomkamata kwa makosa aliyotenda basi watatoa taarifa hizo.

"Baba Askofu Kakobe bado hatujamkamata pale atakapokuwa amekamatwa kwa makosa aliyotenda nitawaambia lakini kwa sasa hajakamatwa mchungaji huyo, jeshi la polisi huwa halipangi kumkamata mtu bali mtu anapofanya kosa la jinai ndipo anakamatwa hivyo na yeye kama amefanya kosa hili basi tutamkamata" alisisitiza Mambosasa

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE


Dk Mollel awaomba msamaha wanachama wa Chadema



Siha. Aliyekuwa mbunge wa Siha, Dk Godwin Mollel amewaomba msamaha wanachama wa Chadema kwa uamuzi wake wa kujivua ubunge na kujiunga na CCM.

Dk Mollel aliyetangaza uamuzi wa kujivua ubunge Desemba 14,2017 na kukabidhiwa kadi ya CCM Desemba 15,2017 amesema upepo wa kisiasa umebadilika na safari aliyoianzisha ni ya kusafisha upinzani kanda ya kaskazini.

Amesema hayo wakati wa kukabidhiwa kadi za CCM madiwani wawili waliojiuzulu nyadhifa zao na kuhama Chadema hivi karibuni, ambao ni wa Donyomurwak, Lwite Ndosi na wa Gararagua aliyekuwa pia mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Siha, Zakaria Lukumay.

Dk Mollel alisema jana Alhamisi Desemba 28,2017 kuwa amelitazama goli na ndiko alikokwenda ili kuweza kufunga.

“Natambua kuna watu walipoteza muda mwingi, walitumia fedha zao kunichangia na wengine walimwaga damu ili niweze kuwa mbunge lakini hivi majuzi nilijivua ubunge hatua ambayo iliwaumiza wengi. Niombe mnisamehe kwa kuwa nilishindwa kuwafuata siku ile nikihama kwa kuwa nilijua mngeweza kunipiga au kusababisha sintofahamu kubwa,” amesema Dk Mollel.

Amesema uamuzi wenye tija siku zote lazima ulete machungu.

Dk Mollel amesema ameingia kwenye vita kuhakikisha anayafikia malengo ya kuwaletea wananchi wa Siha maendeleo waliyoyatarajia kwa kipindi kirefu.

“Niwahakikishie wananchi wa Siha kwamba hamtajuta mimi kuhama chama, kwa kuwa niliisoma ramani yote ya Siha na kuelewa maendeleo yaliko, hivyo sijawaaibisha, niungeni mkono sasa na ninaahidi sitawaangusha,” amesema.

Pia, ametaka viongozi wa CCM kutambua kuwa wana kazi kubwa ya kuhakikisha walio nje ya chama hicho wanavutiwa na matendo ya chama na si kukatishwa tamaa.

Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya amesema, “Kuna watu wanawatisha watu kuwa wakiondoka na kuja CCM hawatapata nafasi, tunawakaribisha kwa kuwa nafasi ziko wazi na wakihitaji kugombea watapata nafasi.”

Mabihya amesema CCM imeongeza idadi ya wapambanaji ambao wameamua wenyewe kuungana na timu ya maendeleo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi amesema milango iko wazi kwa anayetaka kujiunga na chama hicho.

“Wanaorudi CCM wanarudi nyumbani, ninaomba Watanzania waelewe kuwa hakuna biashara ya binadamu na CCM hatuwezi kufanya biashara hiyo,” amesema.

Ndosi aliyekuwa diwani wa Donyomurwak ametaka maneno yanayoendelea kuhusu kuhama kwake Chadema yaishe, kwa kuwa haitaji mashindano ya maneno bali kufanya kazi ili kuyafikia maendeleo.


Ronaldo amtaka Philippe Coutinho kutojiunga na Barcelona



Aliyekuwa mshambuliaji hatari wa timu ya taifa ya Brazil na vilabu vikubwa vya Ulaya, Ronaldo Luís Nazário de Lima amemuonya kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho kuhusu kujiunga na Barcelona.

Coutinho ambaye amekuwa akiwindwa na vinara hao wa La Liga tangu msimu uliopita, ameambiwa na Ronaldo kuwa Barca ni timu ambayo imekuwa na matatizo makubwa na wachezaji wa kutoka nchini Brazil.

Nilijisikia furaha zaidi na zaidi nilipojiunga na Real Madrid, licha ya kuwa nilikuwa na mwaka mzuri huko Barcelona,” Ronaldo amesema hayo wakati akiongea na kituo cha runinga cha Esporte Interativo


Ronaldo de Lima

“Mwishoni, historia yangu na Barça ilikuwa mbaya sana, sawa na ile Neymar aliyokuwa nayo. Barcelona daima imekuwa na matatizo na wachezaji wa Brazil: Neymar, Romario, Ronaldinho na mimi. Sisi wote tulitendewa vibaya na klabu mwishoni licha ya michango yetu yote na kujitolea,” ameongeza.

De Lima aliichezea Barca kwa msimu mmoja wa mwaka 1996–1997 katika mechi 37 na alifanikiwa kufunga magoli 34 na baadaye alihamia Inter Milan ambapo alicheza kwa misimu mitano.



VIDEO: Diamond Platnumz Awakabidhi mashabiki zawadi ya Pikipiki


Msanii wa bongo fleva nchini Tanzania ambae amefanikiwa pia kuvuka boda kwa hatua kubwa Nasibu Abdul alimaarufu kama Diamond Platnumz amewapa mashabiki wake zawadi za pikipiki na zawadi nyingi ikiwemo chibu perfume na nyingine kibao.

Angalia Full Video Hapa na Usisahau ku Subscribe......



Thursday, 28 December 2017

Serikali yapiga hodi mgodi wa Geita



Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi ameunda kamati maalumu ya kuchunguza wanaofuja fedha za wananchi, huku akiwaagiza mkuu wa wilaya hiyo Herman Kapufi, Mkurugenzi wa mji Modest Apolinary kuwasiliana na mgodi wa Geita (GGM) waharakishe kuikabidhi serikali ya mkoa huo majengo yaliyojengwa kwa ufadhili wa mgodi huo yaliyopo magogo ili yabadilishwe kuwa chuo kikubwa cha ufundi kwa lengo la kuwasaidia vijana na watoto katika mkoa wa Geita.

Amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya kalangalala katika shughuli ya uchimbaji misingi ya majengo ya shule ya secondary GEITA,na kwamba baada ya GGM kukabidhi majengo hayo,ndani ya mwezi mmoja watahakikisha wanakamilisha taratibu za kuwa chuo ili watoto wapate kujiunga hasa wale wanaotaka kusomea kozi mbalimbali zikiwemo computer ,makanika,ujenzi, kuchomelea vyuma na madini hakuna haja ya kuwatoa mkoani hapa kuwapeleka kusoma kwenye mikoa mingine.

Katika hatua nyingine baadhi ya wananchi wa kata ya Nyankumbu wamelalamikia baadhi ya viongozi kukwamisha shughuli za maendeleo na kumlazimu mkuu wa wilaya kuahidi kula nao sahani moja.


Manyara bado inasumbuliwa na uhaba wa Walimu



Waalimu na wanafunzi katika shule ya Umbur iliyopo wilayani Mbulu mkoa wa Manyara wanakabiliwa na changamoto kutembea umbali mrefu upatao kilomita 20 kufuata shule,ikiwemo kukosekana uwiano wa walimu na wanafunzi ambapo mwalimu mmoja anafundisha darasa moja lenye watoto zaidi ya 100.

Akizungumza kwa njia ya simu na kunukuliwa na channel ten Mkuu wa wilaya ya mbulu Chelestino Mofuga ameiambia kituo hiki kuwa sera ya elimu inaeleza juu ya uwiano wa wanafunzi wanaopaswa kufundishwa katika chumba kimoja cha darasa kuwa ni kati ya 45 kwa shule za sekondari na 35 kwa shule za msingi ambapo shule ya umbur hali hiyo ni mara tatu zaidi kwa mujibu wa waalimu shuleni hapa wameeleza kuwa wanakailiwa na upungufu wa vyumba vitatu vya madarasa pamoja na waalimu ambapo wanafundisha hadi wanafunzi zaidi ya mia moja.

Umburu shule ya msingi pia kwa sasa inakumbwa na wasi wasi juu ya umiliki wa eneo la shule kwakuwa shule hii haina hati miliki ya ardhi ya eneo iliyopo shule hii.

Watoto hawa licho ya umri wao hutembea kilomita zaidi ya 20 kufuata huduma itakayowapa mwanga kwenye maisha yao jambo linalowaacha wazazi katika maswali mengi wakijiuliza uwezekano wa watoto wao kufanya vizuri katika masomo.

Uzinduzi wa madarasa mawili kwenye shule hii inayofanywa na halmashauri kupitia mkurugenzi wa mbulu vijijini inaongeza idaidi ya vyumba vya madarasa na kufikia vinne lakini haimalizi tatizo uhitaji wa vyumba zaidi vya madarasa kutokana na watoto kutoka wilaya ya karatu mkoa wa arusha pamoja na wilaya ya mbulu mkaoni Manyara kuendelea kuongezeka zaidi.

Benki Kuu yaipa Serikali Bilioni 300


Benki Kuu ya Tanzania imetoa gawio la Shilingi Bilioni 300 kwa Serikali kutokana na faida iliyopatikana kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Taarifa iliyotolewa na Benki Kuu imesema kwamba gawio hilo kutoka benki kuu kwenda kwa Serkali linafikisha jumla ya Bil 780  kwa kipindi cha miaka mitatu (2014/2015- 2016-2017)

Hata hivyo taarifa hiyo imewekwa wazi kwamba majukumu ya msingi ya Benki Kuu siyo kutengeneza faida na inapotokea faida imepatikana , sehemu kubwa hutolewa kama gawio kwa serikali.



Harmorapa amuomba msamaha Master Jay


Msanii wa muziki wa bongo fleva Harmorapa amefunguka na kumuomba radhi mtayarishaji mkongwe wa muziki wa bongo fleva na mmiliki wa studio za Mj Records, Master J na kusema kuwa amegundua kuwa alimkosea mkongwe huyo kwenye muziki.

Harmorapa alifunguka hayo alipohojiwa kwenye kipindi cha eNewz cha EATV na kusema katika mwaka 2017 amemkosea sana Master J kufuatia kauli yake aliyoitoa kipindi cha nyuma kupitia kipindi hicho kuwa hamjui wala hamtambua mtayarishaji huyo mkongwe wa bongo fleva.

"Nimegundua kuwa nilifanya makosa sana, unajua kipindi kile nasema vile nilikuwa bado sijamjua vizuri Master J hivyo naomba anisamehe tu kwani ulikuwa ugeni katika tasnia hivyo nilikuwa sijamjua vizuri" alisikika Harmorapa.

Harmorapa alishawahi kumkana mtayarishaji huyo kuwa hamfahamu baada ya Master J kunukuliwa akisema kuwa msanii huyo hana kipaji cha muziki na kuimba labda kama atakwenda kufanya vichekesho, jambo ambalo lilionesha kumkwaza Harmorapa.


Serikali yawapiga mkwara viongozi wa Dini




Serikali imewaonya viongozi wa dini wanaotumia mahubiri yao kuchambua masuala ya kisiasa, ikiwataka kuheshimu msingi wa uanzishwaji wa taasisi zao la sivyo taasisi zao zitafutwa.

Taarifa iliyotolewa leo Desemba 28 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali mstaafu Projest Rwegasira imesema taasisi za dini zinapaswa kuzingatia sheria na masharti ya kuanzishwa kwake ambayo yapo kwenye Katiba za taasisi husika.

"Baadhi ya jumuiya zimekuwa zikifanya shughuli zao kinyume na malengo yaliyomo kwenye Katiba zao bila kuiarifu Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za kidini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, " amesema na kuongeza,

"Hivi karibuni kumekuwepo na tabia ya baadhi ya viongozi wa jumuiya kutumia mahubiri yao wakati wa ibada kuchambua masuala ya siasa kinyume na Katiba zao. Hakuna jumuiya iliyosajiliwa chini ya sheria ya jumuiya ili kufanya siasa."

Amesema kufanya hivyo ni kwenda kinyume na malengo na ukiukwaji wa Kanuni ya 7 ya Kanuni za Jumuiya zilizoundwa chini ya sheria ya Jumuiya, inayotamka pamoja na mengine kuwa Jumuiya yoyote hairuhusiwi kufanya mabadiliko ya malengo yake bila kibali cha msajili.

“Ofisi ya Msajili inazikumbusha Jumuiya zote kwamba ukiukaji wowote wa Sheria ni kosa ambalo linaweza kupelekea Jumuiya husika kufutiwa usajili wake kama ilivyoelezwa kwenye kifungu cha 17 cha Sheria husika," amesema.

Mwananchi.

Rais Magufuli akutana na kamati ya uhakiki CCM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  John Magufuli amekutana na kamati maalum aliyoiunda kwa lengo la kuhakiki mali za chama hicho, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais amekutana na kamati hiyo leo Desemba28 kwa mara ya kwanza tangu alipoitangaza  Desemba 20, Mkoani Dodoma ambayo inaongozwa na Dk. Bashiru Ally.

Katika Mazungumzo hayo  Rais Magufuli amewataka wajumbe wa kamati hiyo kufuatilia na kuhakiki mali zote za chama, kumhoji mtu yeyote ambaye atahitajika kutoa taarifa juu mali za chama na kubaini thamani ya mali, mahali zilipo, makusanyo ya mapato na wanazozishikilia ama kutumia mali hizo.

Rais Magufuli pia ametoa wito kwa wanachama wa CCM na wananchi wengine kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zote zinazohusu mali za chama kwa kamati hiyo, na watakaoitwa kuhojiwa waitikie wito huo.

“Nataka mali za chama zikinufaishe chama, nataka mkamhoji mtu yeyote, awe kiongozi, awe mwanachama, awe mfanyabiashara, mtu yeyote. Mkazihakiki mali zote ili chama kipate haki yake” amesema  Rais Magufuli.

Akizungumza kwa niaba ya kamati hiyo, Dk Bashiru Ally amesema kamati imeanza kazi rasmi na ametoa wito kwa wanachama, wananchi na wote wanaozitumia mali za chama kutoa ushirikiano watakapoitwa kuhojiwa.

“Tumezungumza na Mwenyekiti kwa karibu saa mbili, katueleza matarajio yake, sababu za kuunda tume hii, kazi zake na faida zake kwa chama na kwa nchi, kwa hiyo ametukabidhi vitendea kazi na taarifa mbalimbali na ametuambia kazi yetu ni kuhakiki mali zote za chama kwa kushirikiana na wanachama na wale wanaoshirikiana na chama kuzitumia hizo mali kama vile wapangaji, wasimamizi, nakadhalika” amesema Dk  Ally.


Kiwanda cha Alizeti chafungwa Singida


Serikali imekifungia Kiwanda cha kukamua mafuta cha  Alizeti Mount  Meru Millers Ltd kwa  muda usiojulikana kwa madai ya kukaidi agizo la kulipa faini ya Sh20milioni.

Uamuzi wa kukifunga kiwanda hicho umetolewa jana Jumatano na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira ,Kangi Lugola  alipokuwa kwenye kwanda hicho kilichopo  kijiji cha Manguanjuki Manispaa ya Singida.

Kabla ya kutoa uamuzi huo  mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Singida, Lugola alisema Novemba 29 mwaka jana, mtangulizi wake Luhaga  Mpina, aliuagiza uongozi wa  kiwanda hicho ulipe  faini ya Sh20milioni kwa kosa la kutiririsha  maji taka yenye kemikali kwenye makazi ya watu .

“Maji taka yameelekezwa kwenye makazi ya wananchi wanaokizunguka kiwanda .Pia maji  hayo yenye kemikali, yameelekezwa kwenye ziwa la Singidani lenye viumbe hai wakiwemo samaki. lakini hadi leo, agizo la Waziri  Mpina, halijatekelezwa’’ amesema Lugola na kuongeza kwamba

‘’Kutokana na  ukiukwaji wa  sheria za mazingira, Mpina alikipa adhabu ya kulipa faini  Sh20milioni ambayo haijalipwa hadi leo”, amesema Waziri Lugola kwa masikitiko.

Lugola amesema kwamba  kiwanda hicho kimetekeleza agizo la kununua mashine ya kutibu maji taka, lakini maji taka hayo, hayajaelekezwa kwenye mashine hiyo.

 “Maji hayo yenye kemikali bado yameendelea kuwa kero kwa wananchi hadi leo, na yanaathiri viumbe hai vilivyopo kwenye ziwa Singidani. Hii dharau kwa serikali haikubaliki”, amesema

Naibu waziri huyo, amesema  wananchi wanaozunguka kiwanda hicho wamekuwa wakitoa kilio chao serikalini kwa miaka minne, kwamba wanaathiriwa na maji yenye kemikali  na moshi mnene wa kiwanda cha Maount Meru.

“Binafsi leo nimefika kwenye kiwanda hiki na baada ya kufanya ukaguzi wa kina, nakiri kwamba kilio cha wananchi wa Manguanjuki ni cha kweli na kinahitaji tiba ya kudumu. Mkuu wa wilaya ya Singida, naagiza kuanzia sasa, usimamie kufungwa kwa kiwanda hiki”,amesema na kuongeza;

“OCD pia nakuagiza uwatafute Wakurugenzi wa kiwanda hiki Atul Nittal, Arvind Mittal na Tarsem Aggarwal, popote walipo na kuwakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria kwa kukaidi agizo la Serikali”.

Kwa upande wake meneja Uhusiano, Nelson Mwakambuta, amesema kiwanda hicho kimekuwa kikifanyiwa ukaguzi mara kwa mara na mamlaka mbalimbali. Lakini  wamekuwa wakiwaambiwa na viongozi hao kuwa   kiwanda hicho, hakina tatizo lolote linalohusiana na kwenda kinyume na sheria za  mazingira.

“Kufungwa kwa muda usiojulikana kwa kiwanda hiki, kutaathiri ustawi wa watumishi wengi wa kiwanda na familia zao. Pia  wakulima wa zao la alizeti ndani na nje ya mkoa wa Singida, nao watakuwa wamepata pigo. Hatupingani na serikali tutatekeleza yale yote tuliyoagizwa”,amesema meneja huyo.



Orodha ya wachezaji wanaolipwa mkwanja mrefu EPL



Ligi Kuu ya Uingereza ni miongoni mwa Ligi Kubwa Ulaya lakini ni miongoni pia mwa Ligi za Ulaya zenye mashabiki wengi ukanda wa Afrika husani Afrika Mashariki, inawezekana kuna mambo mengi ambayo huyafahamu katika Ligi Kuu England.

Hii hapa chini ni orodha ya mastaa wa Soka kwenye Ligi hiyo wanaolipwa mkwanja mrefu zaidi kwa wiki.

1- Paul Pogba analipwa pound 290000/Tsh 872,087,739 (ManUnited)

2- Romelu Lukaku pound 250000/Tsh 752,068,375 (ManUnited)

3- Sergio Aguero pound 220000/Tsh 661,820,170 (ManCity)

= Yaya Toure pound 220000/Tsh 661,820,170 (ManCity)

= Zlatan Ibrahimovic pound 220000/Tsh 661,820,170 (ManUnited)

6-Kevin De Bruyne pound 200000/Tsh 601,609,900 (Man City)

= David De Gea pound 200000/Tsh 601,609,900 (ManUnited)

= Eden Hazard pound 200000/Tsh 601,609,900 (Chelsea)

9-Virgil van Djik pound 180000/Tsh 541,448,910 (Liverpool)

= Philippe Coutinho pound 180000/Tsh 54,1448,910 (Liverpool)


Familia yafukua kaburi la Baba yao




Familia ya watoto wanne wakiongozwa na mama yao mzazi Julieta Majaliwa wamelazimika kufukua kaburi la baba yao Stanford Gombo, wakidai kuwa na mashaka na sababu ya kifo cha baba yao.

Tukio hilo limetokea huko katika cha kijiji cha Kilimani wilayani Gairo mkoani Morogoro ikiwa ni utekelezaji wa amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani humo baada ya familia hiyo kutaka mwili huo kufanyiwa uchunguzi.

Wanafamilia hao walifika kijijini hapo wakiwa na ulinzi wa polisi kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa amri ya mahakama inayoelekeza kufukuliwa kwa kaburi hilo, ili watoto wapate nafasi ya kuhakiki mwili uliozikwa kama ni wa baba yao pamoja na kufanyiwa uchunguzi kubaini sababu zilizopelekea kifo chake.

Kwa upande wake Mke wa marehemu ,Bi. Julieta Majaliwa amesema mara ya mwisho kuwasiliana na mumewe walikua  nyumbani kwao jijini Dar es salaam ambapo alimuaga anaenda kijiji kwao kuwajulia hali lakini tangu alivyo ondoka hawa kuwa na mawasiliano hadi kifo chake.

Chifu ashambuliwa kwa kupiga vita pombe haramu



Chifu wa eneo la Elburgon, Kaunti ya Nakuru nchini Kenya alijikuta akishambuliwa na kundi la vijana wenye hasira alipoongoza msako dhidi ya pombe haramu.

Chifu huyo anayejulikana kwa jina la Francis Ngacha, alikuwa ameongozana na wanachama wa kundi la nyumba kumi aliposhambuliwa na vijana hao, wakimlaumu kwa kuwaharibia sherehe zao za Krismasi.

“Nilikuwa nimeongoza kikundi hicho kufanya msako dhidi ya vijiwe vya kuuza pombe haramu katika eneo hilo, na ndipo kundi la vijana zaidi ya 10 lilipoanza kuturushia mawe,” amesema Bw. Ngacha.

Kwa upande mwengine Naibu Kamishna wa Kaunti hiyo Bw. Naftaly Korir, alituma kikosi cha polisi kufanya msako huo, lakini hawakufanikiwa kuwakamata vijana waliomshambulia chifu, kwani walitoroka eneo hilo.

Polisi wamesema wanawatafuta vijana hao waliohusika kumshambulia chifu, ili wachukuliwe hatua za kisheria.



Audio | Joh Makini – Mipaka | Mp3 Download

Audio | Joh Makini – Mipaka | Mp3 Download


Audio | Joh Makini – Mipaka | Mp3 Download

DOWNLOAD

Video | Nancy Hebron ft Vanessa Mdee, Mimi Mars – Beautiful Jesus | Mp4 Download

Video | Nancy Hebron ft Vanessa Mdee, Mimi Mars – Beautiful Jesus | Mp4 Download


Video | Nancy Hebron ft Vanessa Mdee, Mimi Mars – Beautiful Jesus | Mp4 Download


Video | Joh Makini – Mipaka.| Mp4 Download

Video | Joh Makini – Mipaka.| Mp4 Download

Video | Joh Makini – Mipaka.| Mp4 Download

DOWNLOAD

Video | Samir – Zuzu.| Mp4 Download

Video | Samir – Zuzu.| Mp4 Download

Video | Samir – Zuzu.| Mp4 Download

DOWNLOAD


Audio | Mercy Masika – Upendo | Mp3 Download

Audio | Mercy Masika – Upendo | Mp3 Download



Audio | Mercy Masika – Upendo | Mp3 Download

DOWNLOAD

Audio | Saida Karoli – Kabaka | Mp3 Download

Audio | Saida Karoli – Kabaka | Mp3 Download

Audio | Saida Karoli – Kabaka | Mp3 Download

DOWNLOAD

Audio | Orbit – 1000 -100,000 “Buku kuwa Laki | Mp3 Download

Audio | Orbit – 1000 -100,000 “Buku kuwa Laki | Mp3 Download

Audio | Orbit – 1000 -100,000 “Buku kuwa Laki | Mp3 Download


DOWNLOAD

Audio | Chemical – Struggle | Mp3 Download

Audio | Chemical – Struggle | Mp3 Download

Audio | Chemical – Struggle | Mp3 Download

DOWNLOAD

Audio | B2k – Tunaendana | Mp3 Download

Audio | B2k – Tunaendana | Mp3 Download

Audio | B2k – Tunaendana | Mp3 Download

DOWNLOAD

Video | Tiwa Savage – SugarCane | Mp4 Download

Video | Tiwa Savage – SugarCane | Mp4 Download

Video | Tiwa Savage – SugarCane | Mp4 Download


DOWNLOAD

Guardiola afunguka asema Barcelona yapewa jeuri na Messi


Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema Lionel Messi ndio mtu anayeifanya Barcelona iwe timu yenye nafasi kubwa ya kutwaa Ligi ya mabingwa Ulaya msimu huu.

Guardiola ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa habari ambaye alimuuliza kuhusu timu yake ya Man City kama ina nafasi kubwa ya kushinda ubingwa wa Ulaya msimu huu.

Pep alimjibu mwandishi kwa kumuuliza swali kuwa, “Ni timu gani anachezea Lionel Messi”, ? Baada ya mwandishi kujibu kuwa ni Barcelona ndipo Guardiola akamwambia kuwa ndio timu yenye nafasi ya kutwaa UEFA.

Guardiola alifafanua kuwa aina ya uchezaji wa Barcelona kwa sasa ni hatari zaidi kwani wanaanza kumiliki mpira kwenye eneo la ushambuliaji kwa kumtumia zaidi Messi.

“Hakuna asiyejua ubora wa Messi, na kama Barcelona inamtumia kwenye eneo la adui unategemea nini kama sio kukumaliza tu mpinzani”, ameeleza Guardiol



Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB atangaza kujiuzulu


MTENDAJI Mkuu wa CRDB Bank, Dr Charles Kimeo, leo ametangaza kustaaafu ifikapo Mei 2019. Dkt. Kimei aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwamba hatua hiyo ni kwa ajili ya kuanzisha mchakato wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo kupata mtu atakayeshika nafasi yake kwa mujibu wa taratibu na kanuni zilizopo.

Kabla ya kujiunga na benki hiyo, Dk Kimei alifanya kazi Benki Kuu ya Tanzania kama Mkurugenzi Mfawidhi wa Shughuli za Benki, Mkurugenzi wa Sera, Uchumi na Utafiti, Meneja wa Idara ya Utafiti wa Uchumi na Sera na nyadhifa nyingine mbalimbali katika Idara ya Utafiti. Hivi sasa ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki Mabenki nchini.

Amewahi pia kufanya kazi katika bodi mbalimbali ikiwemo ya Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Mamlaka ya Elimu nchini, Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kampuni ya Huduma za Mikopo Midogo ya CRDB na tawi la CRDB nchini Burundi.

Dkt. Kimei ana Shahada ya Uzamivu katika Uchumi aliyoipata Chuo Kikuu cha Uppsala cha Sweden, Shahada ya Uzamili katika Uchumi aliyoipata Chuo cha Uchumi cha Stockholm na Shahada ya Sayansi (Uchumi) aliyoipata Chuo Kikuu cha Taifa cha Moscow.


Baada ya kuwashuku wachezaji kuiba blanketi, shirika la Ndege lawaomba radhi


Shirika la American Airlines limewaomba msamaha wachezaji wawili wa mpira wa kikapu ambao walifukuzwa kutoka kwa ndege kwa kuwashuku kuiba.

Marquis Teague na Trahson Burrell waliabiri ndege hiyo siku moja kabla ya krismasi wakielekea kucheza mechi.

Lakini kabla ya ndeye kuondoka uwanjani, mhudumu mmoja wa ndege alidai kuwa wanaume hao walikuwa mablanketi kutoka upande wa kifahari wa ndege ambapo walilazimishwa kushuka kutoka kwe ndege hiyo.

Baadaye ilibainika kuwa ni abiria walikuwa wamewapa mablanketi hayo.

Wachezaji hao wote walikuwa wa asilia ya Afrika akiwemo mhudumu wa ndege.

Hakuna mchezaji kati ya hao wanaochezea timu ya Memphis Hustle amezungumzia kisa hicho.

Laiki naibu kocha wa Hustle, Darnell Lazere aliandika katika twitter kuwa kitendo hicho kilichochewa na ubaguzi wa rangi.

Wachezaji walikuwa wakisafiri kutoka uwanja wa Dallas-Fort Worth kwenda Sioux Falls, South Dakota wakitumia ndege ya Envoy Air iliyo sehemu ya American Airlines.




Nikki wa Pili atupa dongo hili



 Msanii Nikki wa Pili ambaye ni miongoni mwa wasanii wachache wanaofanya uchambuzi wa masuala mbali mbali ikiwemo uchumi wa taifa, ametupa jiwe gizani kuhusu sera mpya ya viwanda.

Kupitia ukurasa wake wa twitter Nikki wa Pili ameandika ujumbe kuhusu sera mpya ya Tanzania ya viwanda inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano, na kusema kwamba ni vyema tukajitafakari kwa hili kwani nchi ambazo zimefanikiwa, zilitumia mfumo wa ruzuku na sio wawekezaji pekee.

"Kupitia ruzuku ya serikali, na ulinzi dhidi ya ushindani wa kisoko kwa miaka 40 ndipo Japan wakafanikiwa kuisimamisha secta ya viwanda vya magari, sasa tunao hubiri Tanzania ya viwanda kupitia wawekezaji na ushindani wa kisoko tujitafakari",ameandika Niki wa Pili.

Sasa hivi Tanzania inapambana kuleta mapinduzi ya viwanda ili nchi iweze kuzalisha vitu vingi yenyewe bila kuagiza nje, huku ikitoa fursa kwa wawekezaji mbali mbali kuja nchini kuwekeza kwenye sekta ya viwanda.




Lissu huenda akakaa hospitali miezi sita zaidi


Dar es Salaam. Siku moja baada ya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kusimama kwa mara ya kwanza tangu Septemba 7, amesema huenda akakaa hospitalini kwa miezi sita zaidi.

Juzi, Lissu anayepata matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya alisimama kwa msaada wa madaktari.

Akijibu swali ni lini atarejea nchini na kama atasafiri nje ya Afrika kwa matibabu zaidi aliloulizwa jana na mwandishi wetu, Lissu alisema, “Ndio kwanza nimesimama jana (juzi), kuna miezi sita ya ‘rehabilitation’ (kumrudisha katika hali ya kawaida). Madaktari waliniambia kuna miezi sita au tisa.”

“Kwanza nimesimama kwa mara ya kwanza uamuzi wa je, nitamalizia hapa au nitakwenda bado, itategemea ushauri wa madaktari na kisha majadiliano na familia kwa sasa bado sijajua.”

Tangu mwanasheria huyo mkuu wa Chadema aliposhambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi akiwa katika makazi yake Area D mjini Dodoma Septemba 7, hakuwahi kusimama na wakati wote alikuwa akionekana amelala au amekaa hadi juzi.

Katika picha iliyomwonyesha Lissu akiwa amesimama, madaktari wawili walimshika huku mmoja akiurekebisha mguu wake wa kulia.

Lissu alituma ujumbe kwa wapigakura wa Singida Kaskazini akisema; “Wajiandae kwa mapambano makubwa ya kisiasa… kila mmoja atimize wajibu wake na kuacha visingizio.”

Akizungumzia hatua ya Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) kusimama, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema, “Ni jambo la kumshukuru Mungu, tulikuwa tunapigania mwenzetu asimame, tunamshukuru Mungu kwa hatua hii.

“Itachukua muda kidogo ili aweze kurejea katika hali yake, lakini tumshukuru sana Mungu kwa kutupa Lissu, lakini tuwashukuru sana madaktari waliomuuguza na hili ni funzo kwetu,” alisema.

Alipoulizwa iwapo wanamkumbuka Lissu katika harakati zake, Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alisema, “Kila kiongozi ana wajibu wake wa kiharakati, uongozi si shule unakwenda kujifunza, kila mmoja ana vipawa vyake, wengine ni wazuri katika kuhoji, wengine katika mikutano ya hadhara, wengine mikakati na kila mmoja ana wajibu wake.

“Lissu ni moja ya wanasiasa makini na mahiri hasa linapokuja suala la kuhoji, amekuwa msaada mkubwa katika kambi ya upinzani bungeni na zaidi katika masuala ya sheria na Mahakama, kila mmoja anajua hivyo, kwa hiyo ni kweli tunaposema ‘tumemmisi’ ni kweli tumemmisi sana,” alisema.

Mbowe alisema, “Tunawashukuru Watanzania walio wengi walioshiriki kumuuguza Lissu, kumwombea, kutoa michango na salamu zao hadi amefikia hatua ile ambayo wengi hawakutegemea.Tunawashukuru viongozi wa dini na watu waliomwombea kamanda wetu aweze kupona.”



Sakata la Airtel, Wafanyakazi TTCL wajitosa


Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Mawasiliano Tanzania (Tewuta) kimepongeza hatua ya Rais John Magufuli kumtaka Waziri wa Fedha kuanza uchunguzi kubaini ukweli kuhusu ubinafsishwaji wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

Katibu Mkuu wa Tewuta, Junus Ndaro amesema chama hicho kinatambua fika kuwepo mchezo mchafu uliosababishwa na Watanzania wachache wenye uchu wa fedha wakisaidiana na wawekezaji kupora rasilimali hiyo ya Taifa.

Ndaro amesema leo Alhamisi Desemba 28,2017 kuwa, kwa muda mrefu chama hicho kimekuwa kikitoa malalamiko kuhusu ufisadi huo serikalini lakini hakikusikilizwa.

“Tunampongeza Rais Magufuli kwa kuthubutu kutamka pasipo shaka kuwa taarifa alizonazo zinaonyesha kampuni ya Airtel ni mali ya TTCL, jambo hili tulilipigia kelele kwa muda mrefu,” amesema.

Ndaro amesema mara zote hawakusita kutamka kuwa Celtel ambayo sasa ni Airtel ni mali ya TTCL iliyoporwa pasipo kulipwa chochote.

“Wafanyakazi tunatambua kuwa TTCL haikuporwa Celtel pekee bali ilinyang’anywa pia Chuo cha Posta na Simu hali iliyosababisha tukose mahali pa kupata mafunzo,” amesema Ndaro.

Kutokana na kuanza uchunguzi wa sakata hilo, Ndaro amesema viongozi wa Tewuta wako tayari kutoa kila aina ya ushirikiano kuhakikisha Serikali inashinda na kuirudisha Airtel mikononi mwa TTCL.

JPM aagiza TCRA kuzifuta kampuni za simu zitakazoshindwa kujiunga na soko la hisa

“Tuna ushahidi wa kutosha na tuko tayari kutoa ushirikiano kwa Serikali katika hatua zote kuleta haki iliyopotea ya Kampuni ya Simu Tanzania,” amesema.




Askofu wa KKKT ahoji mipaka ya dini na siasa



Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera, Benson Bagonza amehoji mipaka ya kuzungumzia masuala ya siasa na dini, huku akitaka wananchi kutojengewa hofu ya kutoa maoni yao.

Kauli ya askofu huyo inafanana na iliyotolewa na Mkuu wa Kanisa hilo, Askofu Fredrick Shoo katika ibada ya Krismasi Jumatatu iliyopita kwamba kuna baadhi ya watu wanawajengea wananchi hofu ili wasiweze kutumia uhuru wao kutoa mawazo.

Askofu Bagonza alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na mwandishi wetu, ikiwa ni muda mfupi baada ya kuweka ujumbe katika ukurasa wake wa Facebook, akihoji sababu za watu kuwasakama viongozi wa dini wanaojadili masuala ya siasa.

Alipotakiwa kuthibitisha kama ujumbe huo ni wa wake, Askofu Bagonza alisema “Ni kweli ni wa kwangu na kama huuoni, vijana watakuwa wamechezea mtandao.”

Ujumbe huo unasema, “Wakijenga shule hawaingilii wizara ya elimu, wakijenga hospitali hawaingilii wizara ya afya, wakijenga kisima cha maji hawaingilii wizara ya maji. Wakiombea mvua hawaingilii mamlaka ya hali ya hewa.

“Wakihimiza kilimo hawaingilii wizara ya kilimo, wakitoa msaada wa dawa kwa mgonjwa, wanapongezwa, wakihoji kwa nini hakuna dawa hospitali, wanaambiwa wanachanganya dini na siasa na wakikosoa mfumo wa kisiasa, wanaambiwa wanaingilia siasa! Kuna kitu hakiendi sawa.”

Akifafanua kuhusu ujumbe huo alisema, “Tujenge utamaduni wa kujenga hoja na kutotukanana matusi. Kuna watu wengine wanaamini uhuru wa kusema umetoweka. Nasema, kuwapa uhuru watu kusema na kutoa mawazo yao kunajenga kuliko kuwazuia au kuwajengea hofu.”

Askofu Bagonza pia alizungumzia madai kwamba viongozi wa dini wamekuwa wakimya sasa, “Si kama huko nyuma tulikuwa tunasema na sasa hatusemi hapana, Krismasi hii tumeanza kusema, lakini tukisema mnasema tunasema sana, tukikaa kimya mnasema tunakaa kimya.”

Alisema haki huliinua Taifa na mlinzi mkubwa wa amani ni haki.

“Vyombo vya dola wanahitaji haki, kila mtu anahitaji haki na silaha pekee ya amani ni haki. Tuwape uhuru watu waseme bila kuwazuia, tujenge utamaduni wa kujenga hoja,” alisema.

Askofu Shoo akihubiri katika ibada Krismasi kwenye Usharika wa Moshi Mjini wa Dayosisi ya Kaskazini ya kanisa hilo alisema watu wanajazwa hofu ili wasiseme ukweli wa kile wanachokiamini.

“Kuna watu wanajaribu kuwajaza watu hofu ili watu wasiseme ukweli na wasikae katika kweli. Watu wanajazwa hofu ili wasitetee kile wanachokiona ni cha haki,” alisema Dk Shoo ambaye pia ni Askofu wa dayosisi hiyo.

Alisema, “Watu wanajazwa hofu ili wasiwe huru kutoa mawazo wanayojisikia kuhusu Kristo, nchi yao na imani yao. Tukidumu katika kweli inatupa nguvu na uhuru wa kusema na kutembea bila woga.”

“Yesu amezaliwa si kutuletea tu neema lakini anatuletea kweli kuhusu maisha ya hapa duniani. Mafundisho yanatufundisha tumpokee ili atawale maisha yetu. Tudumu katika ukweli huu na daima tusimame katika kweli hiyo, wala tusione aibu wala tusione woga wa kusimama katika kweli hiyo. Wala tusione woga wa kutetea kweli hiyo,” alisema.

Jeshi la Polisi lasema wahalifu wamehamia Digitali



Msemaji wa Jeshi la Polisi Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Barnabas Mwakalukwa amedai kwamba pamoja na kwamba sikukuu ya Krismas kupita kwa amani pasipo matukio ya uhalifu, anaamini kwamba hali ya maisha imebadilika hali inayowafanya wahalifukuachana na uhalifu wa analogia na kwenda digitali.

Akizungumza na Mtangazaji wa East Africa Drive ya EA Radio Bi Scola Kisanga, Kamanda Mwakalukwa amesema kwamba wizi wa analogia umepungua kabisa na wahalifu hao wamebadili mbinu za kufanya na ndiyo asababu watu wengi bado wanalalamika kutapeliwa kwa njia ya simu.

"Uhalifu umehama na hakuna ule wa kizamani. Zamani walikuwa wanadanganya labda muonane ndo wanafanya uhalifu lakini sasa hivi wamejificha nyuma ya mitandao lakini hata huko pia tunafanya doria. Wananchi wasisite kutoa taarifa polisi wanapokumbwa na matatizo hayo".

Akizungumzia kuhusu vyombo vya usalama nchini kujipanga kwenye sikukuu za mwaka mpya, Mwakalukwa amesema kwamba kila Mkoa unampango kazi wake wa kusimamia hiyo siku na kuongeza kuwa wao kama jeshi la polisi wamekataza kupiga fataki, kuchoma matairi na vitendo vyote ambavyo vitavunja sheria.

Mwanaume auwa watoto wake wawili kwa sumu



KIAMBU, KENYA: Jeshi la Polisi linamshikilia Mwanaume mmoja aliyewaua Watoto wake wawil 2 na yeye kunywa sumu ambayo haikumuua.

Watoto hao waliouawa mmoja alikuwa na miaka 7 na mwingine miaka 3

Inadaiwa kuwa siku moja kabla ya Sherehe ya Christmas familia hiyo ilisafiri hadi Narumoru ambako Mama wa Watoto hao alibakia huko kwasababu ambazo hazijajulikana.

VIDEO: TEWUTA wawataja Wahujumu wa TTCL



Chama cha wafanyakazi wa sekta ya Huduma za mtandao wa mawasiliano Tanzania (TEWUTA), wawataja wahujumu wa TTCL ambao walihusika katika kuihujumu shirika hilo kongwe, na pia kutaja baadhi mali ambazo zilikuwa zikimilikiwa na shirika hilo ikiwemo eneo la standi kuu ya mabasi la ubungo.

ANGALIA FULL VIDEO ..............HAPA USISAHAU KU SUBSCRIBE........


Ndalichako asema Wizara yake haina urasimu


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema Wizara yake haina urasimu wowote katika usajili wa shule zinazoanzishwa ikiwa tu zimetimiza vigezo vinavyozingatiwa.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo alipotembelea shule ya Sekondari Chegeni inayoendelea kujengwa Kijiji cha Bulima wilayani Busega pamoja na Shule ya Msingi Njalu iliyopo Wilayani Itilima zote zikiwa mkoani Simiyu zinajengwa kwa nguvu ya wananchi.

“Lengo la Serikali ni kuwa na shule nyingi lakini ni lazima vigezo na masharti yaliyowekwa na Wizara yazingatiwe, kuna watu ambao siyo waaminifu, zamani ilikuwa hata mtu akiwa na madarasa matatu akiomba usajili anaruhusiwa na shule inasajiliwa lakini wakisharuhusiwa wanabweteka na matokeo yake wanaleta shida kwa watoto wetu” amesema Profesa Ndalichako.

Kwa upande mwingine Waziri Ndalichako ameahidi kuchangia ujenzi wa shule hizo kwa kutoa saruji mifuko 100 kwa Shule ya Njalu(Itilima) na Mifuko 150 kwa Shule ya Chegeni (Busega) huku akiwataka Wakurugenzi wa Halmashauri hizo kuhakikisha kuwa wanatafuta vifaa vingine ili kukamilisha miundombinu inayotakiwa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema Serikali ya Mkoa na Wilaya ya Itilima itachangia  saruji mifuko 100 kwa shule ya Msingi Njalu na Serikali ya Mkoa na Wilaya ya Busega itachangia mifuko 50 kwa Shule ya Sekondari Chegeni.


Zari aendeleza bifu lake na Mobeto


Baada ya mwanamitindo Hamisa Mobetto kumtibua upya mama watoto wa Diamond, Zari The Boss Lady ikiwemo kumuita mcheza picha chafu, Zari ajibu mapigo tena.

Mobetto ambaye alikuwa nchini Uganda weekend iliyopita kwaajili ya show ya Girls Power, alimtupia dongo Zari na kumuita mcheza picha za uchi.

Alhamisi hii Zari ameamua kumtolea uvivu Mobetto kwa kuandika ujumbe mkali mfululizo kupitia mtandao wa snapchat.

“Bora mimi changudoa mzee niliye na mafanikio na bado ananipenda kuliko kijana wa miaka 20+ mama uliyeachwa solemba mara mbili na tuzo juu #MchepukoUsioNaAKili #MweweWaMwaka,” , aliandika Zari Snapchat.

“Kijana, kijana kila siku kijana, kijana na mzuri lakini huwezi kutafuta mwanaume wa kwako mwenyewe….namna chan**doa usivyojiamini, Kama unajiamini na uzuri na akili basi acha tuone mwanaume gani atakutaka baada ya drama hizi, baby daddy 3 loading ukiwa na miaka 20+ atakuwa mjinga pia,” alisema Zari kupitia ujumbe huo.

Zari akaongeza “sio wewe cha***doa uliyelia social media ukidai Lulu kakuibia bwana’ko lakini umegeuka kufanya hicho hicho ulicholilia wakati unajua inavyouma, Mungu hawezi kubariki furaha yako juu ya maumivu ya mwanamke mwingine…ng’oo!!!”
“Unaweza kupost picha zote za nyuma ukiwa nae, lakini tayari nimekwisha msamehe makosa yake yaliyopita. Siwezi kubadilisha historia….nimechukulia kawaida naendelea kujenga maisha yangu ya kesho. Uchawi wote unaisha nguvu na sasa anarudi kwa akili zake kumrudia,” amesema Zari na kusisitiza.



Pretyy Kind aingizwa mjini na muhuni


Kisura wa filamu Bongo, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuibiwa hela kiasi cha shilingi milioni moja alizokuwa ameweka kwenye gari lake pamoja na kadi ya benki, baada ya kumpa mtu funguo ili asogeze gari lake ambalo lilikuwa limeziba njia.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, ishu hiyo ilijiri siku chache zilizopita, ambapo msanii huyo alikuwa studio moja maeneo ya Sinza, ndipo kijana mmoja ambaye si mwenyeji wa studio hiyo akamuomba funguo akamsogezee gari yake ambayo ilikuwa imezuia njia, akampa. Baadaye wakati anaondoka, mrembo huyo alibaini kuwa amelizwa fedha hizo.

Kutokana na sekeseke hilo Pretty alipotafutwa alisema; “Nimekoma kuwapa watu hovyo gari langu, maana bora kaiba hivyo tu, angeiba gari sijui ingekuwaje, nilimuweka ndani mtu wa studio amuonyeshe huyo mwizi alipo, eti anadai ni mtoto wa mkubwa hawezi kupatikana, nimeumia sana,”alisema bishosti huyo ambaye amefungua jalada la kesi Kituo cha Polisi Kijitonyama KJN/RB/12224 WIZI.



OMG kufunga mwaka na kolabo ya Kimataifa


Kundi la muziki la OMG limesema linatarajia kuachia kolabo kubwa na msanii mkubwa kutoka Afrika.

Member wa kundi hilo Young Lunya ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa pia katika kolabo hiyo kuna msanii mwingine kutoka nje ya Afrika.

“Na kabla mwaka hajaisha kuna zawadi moja kubwa sana naona tuiachie, kuna kolabo kubwa sana tumefanya na msanii wa Afrika ila kuna mmoja ni nje ya Afrika,” amesema.

Kwa upande wake Con Boi amezungumzia utendaji kazi wao kwa mwaka huu, 2017 kwa kusema; “Mwaka huu hatukuachia kazi nyingi lakini tunafanya kazi, zipo zinafanyika, 2018 utakuwa ni mwaka wa ku-release, tutaachia sana nyimbo kuanzia mwezi wa kwanza hadi wa 12 ni mauaji kutoka OMG,”.




Wasomi waeleza athari za kurudia uchaguzi


Utashi wa kisiasa wa wabunge kuvihama vyama vyao umetajwa kulisababishia Taifa hasara kutokana na Serikali kutumia fedha nyingi kugharamia chaguzi za marudio.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa waliozungumza na gazeti hili wamesema hali hiyo inaweza kuepukwa iwapo wananchi wataanza kuchagua chama badala ya mtu.

Wamesema katika utaratibu huo, ikiwa mbunge atahamia chama kingine, chama chake cha awali kitapitisha mtu mwingine kuchukua nafasi yake, bila kulazimika kuingia kwenye uchaguzi.

Hivi karibuni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alieleza jinsi ofisi yake ilivyookoa Sh156 bilioni ambazo zingetumika iwapo Serikali ingeshindwa kesi na kurudia uchaguzi katika majimbo 52.

Hiyo inamaanisha kwamba kwa wastani, Sh3 bilioni hutumika kugharamia uchaguzi wa ubunge katika jimbo moja.

Hivi karibuni wabunge wawili wa upinzani, Dk Godwin Mollel wa Siha (Chadema) na Maulid Mtulia wa Kinondoni (CUF) walijivua uanachama wa vyama vyao na kujiunga CCM sawa na Lazaro Nyalandu ambaye alijiuzulu uanachama wa CCM na ubunge wa Singida Kaskazini na kuhamia Chadema.

Mbali na majimbo hayo ambako utafanyika uchaguzi unaotokana na utashi wa wanasiasa, majimbo ya Longido na Songea Mjini yatafanya uchaguzi kutokana na sababu zisizoepukika.

“Nadhani umefikia wakati wa wananchi kuchagua chama, mfano mbunge akihama chama chake, chama hicho kipitishe mtu mwingine kuwa mbunge wa jimbo husika bila NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi) kuitisha uchaguzi mwingine,” alisema Dk Vincent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema.

Kwa kurejea wastani wa jimbo moja kugharimu Sh3 bilioni, majimbo hayo matatu yatatumia kiasi cha Sh9 bilioni. Gazeti hili limechambua kiasi hicho cha fedha na kubaini kuwa kinaweza kutumika kununua magari manne ya kubebea wagonjwa, kujenga zahanati tano, madarasa 400 na mashine mbili za CT-Scan kwa pamoja.

Magari moja la kubebea wagonjwa linagharimu Sh300 milioni, hivyo Sh1.2 bilioni za sehemu hiyo ya fedha zingeweza kutumika kununua magari manne na kuwezesha mikoa minne nchini kupata magari hayo.

Pia, zahanati moja yenye vifaa vyote muhimu, ujenzi wake unagharimu kati ya Sh600 milioni na Sh700 milioni. Hivyo, Sh3 bilioni zingeweza kutumika kujenga zahanati tano.

Pia fedha hizo zingeweza kujenga vyumba 400 vya madarasa kwa kutumia Sh3 bilioni. Ujenzi wa chumba kimoja cha darasa ni Sh7.5milioni.

Kipimo maarufu cha CT-Scan kinauzwa kwa wastani wa Sh900 milioni hivyo Sh1.8 bilioni zingeweza kutumika kununua mashine hizo mbili.

Wanasiasa, wasomi walonga

Katika ufafanuzi wake Dk Mashinji alisema, “Tukiwa na mfumo wa watu kuchagua chama tutaepuka gharama za chaguzi ndogo na hili wimbi la watu kuhama halitakuwa na athari zozote kwa maendeleo ya nchi. Unajua kinachoendelea sasa ni athari za demokrasia ambayo tumeichagua wenyewe.”

Alisema mgombea ubunge hubebwa na ajenda na ilani ya chama chake si yake binafsi, hivyo ikitokea akahama, chama alichokikimbia ndicho kinapaswa kuteua mtu mwingine kuwa mbunge, si uchaguzi kurudiwa.

“Huu utaratibu ndio unaotumika hata Afrika Kusini. Wananchi wanapaswa kuchagua chama si mtu.”

Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ngemela Lubinga alifafanua jambo hilo kwa kina na kusisitiza, “Kama wanataka kuondoa gharama ya uchaguzi wapeleke muswada bungeni maana suala la uchaguzi halipo kwa matakwa ya kikundi au matakwa binafsi, ni sheria na kanuni tulizojiwekea.”

“Kwamba ili tutekeleze demokrasia Tanzania yafuatayo yatatekelezwa, moja wapo ni ikiwa mbunge, diwani au mwenyekiti wa kijiji akifa au akijiuzulu lazima uchaguzi ufanyike.”

Alisema ikiwa wananchi watahoji jambo hilo na kupelekwa bungeni linaweza kubadilishwa na kwamba utaratibu huo ndio utekelezaji wa demokrasia.

Dk Charles Kitima wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (Saut) alisema jimbo likiwa wazi, uchaguzi unapaswa kufanyika ila kinachopaswa kujadiliwa ni baadhi ya wabunge kuwa kigeugeu na kujiuzulu ubunge na kujivua uanachama wakati waliomba kura wakiahidi kuwatumikia wananchi kwa kipindi cha miaka mitano.

Alisema inasikitisha kuona gharama kubwa inatumika kurudia uchaguzi uliotokana na watu kujiuzulu wakati bado kukiwa na uhitaji wa dawa hospitalini, ajira kwa vijana, ujenzi wa barabara na shughuli nyingine nyingi za maendeleo.

“Kwa hiyo hili liwe fundisho kwa wananchi wakati wanapochagua wawatafakari wagombea, wasiwapigie kura vigeugeu,” alisema Dk Kitima.

Mwingine aliyezungumzia suala hilo ni Dk Jimson Sanga wa Chuo Kikuu cha Iringa (UoI). Alisema ni bora Serikali ingesitisha uchaguzi kwenye majimbo ambayo wabunge wake wanajiuzulu ili kuepuka matumizi makubwa ya fedha ambazo zingetumika kwenye kazi nyingine za maendeleo ya wananchi.


Alisema haiingii akilini mbunge kujiuzulu kwa madai ya kuunga mkono sera na utendaji kazi mzuri wa Rais John Magufuli wakati uamuzi wake wa kuhama unapingana na sera ya kubana matumizi.

“Sasa kama wanaunga mkono kazi nzuri za Rais kwa nini wasipande majukwaani kuhubiri sera hizo badala ya kujiuzulu? Ni bora wangefukuzwa na vyama vyao kwa kuunga mkono jitihada za Rais jambo ambalo lingekuwa na namna nyingine ya kujadilika,” alisema Dk Sanga.

Alisema kazi ya mbunge kwenye jimbo ni kuwawakilisha wananchi na inapotokea Serikali inatekeleza sera za wananchi hao haimaanishi kuwa mbunge anatakiwa kuwasaliti na kuachia madaraka.

Aliongeza kuwa ipo miradi mingi ya maendeleo inayohitaji fedha nyingi ambazo badala ya kupelekwa huko, zitapaswa kutumika kwenye uchaguzi, hilo si jambo sahihi.

Katibu Mkuu wa zamani wa NCCR-Mageuzi aliungana na Dk Mashinji na kusisitiza, “Iweje mbunge uhame kwa madai ya kuridhishwa na juhudi anazozifanya Rais Magufuli. Kwa nini juhudi hizo usiziige kwa kuliletea maendeleo jimbo lako.”

“Katika majimbo yao hakuna maji, umeme, huduma za afya ni duni lakini wanakimbia wananchi waliowachagua na kwenda kumuunga mkono Rais. Kwanini wasishirikiane na Rais kuwaletea wananchi maendeleo.”





Kardinali Pengo alilia wimbi la watoto wa mitaani


Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp Kardinali Pengo `amewalilia’ watoto wa mitaani wanaoomba akisema wanafanya hivyo kwa kutumwa na wazazi au walezi wao.

Akihubiri katika misa takatifu ya watoto mashahidi leo Alhamisi Desemba 28, 2017 katika viwanja vya Msimbazi Center wilayani Ilala, Pengo amesema watoto wanateswa na wazazi ama walezi.

Misa hiyo ni sehemu ya kumbukumbu Mfalme Herode aliyemuru mauaji ya watoto wote wenye umri wa miaka miwili ili aweze kumuangamiza Yesu huko Bethrehem.

Akisimulia kisa kimoja, Pengo amesema “siku moja nilikuwa naendesha gari siku hizo nikiwa na nguvu,” amesema

“Nilisimama mbele ya mtoto mmoja aliyekuwa akiomba msaada katika mtaa mmoja wa jijini Dar es Salaam,” amesema .

 “Nikamuuliza wewe umekaa hapa jua linakuwakia mchana kutwa, mvua ikija inakunyeshea, je ungependa nikakuandikishe shule ili uweze kuwa na maisha yako,” amesema Pengo.

Amesema  baada ya kumuuliza kuhusu shule yule mtoto alitoweka na kutokomea kusikojulikana.

“Mtoto yule hakutaka kusikia neno linaloitwa shule, nikajiuliza huyu mtoto anataka kubaki hapa mtaani kuombaomba na adha zote hizi,”amesema.

Amesema  alikuja kugundua baadaye kwamba wengine ni watoto yatima ambao wanalazimika kuomba ili wapate mahitaji yao.

Amesema  watoto wengi wanaoomba mitaani wanafanya hivyo kwa kutumwa na wazazi wao ua walezi.

“Wanatumwa na wazazi wao kuomba lakini fedha zinazopatikana ni za wazazi wao na wasipopata wanalala na njaa,  inasikitisha,” amesema.

Kardinali Pengo amesema wako baadhi ya wazazi ambao wanawapa ulemavu wa kudumu watoto wao ili wawe kivutio wakati wa kuomba.

“Kuna kesi moja ambayo mzazi alimvunja mkono mtoto wake akawa mlemavu ili awe kivutio wakati wa kuomba,”amesema.

Amesema  wako wazazi ambao kwa makusudi wanawapa upofu watoto wao ili mradi wao wanufaike.

“Kwa hiyo akina Herode wako hadi leo, unaweza kujiuliza mwenyewe Herode na wazazi wa aina hii nani katili,” alisema

Amesema  uovu dhidi ya watoto unafanywa hadi leo na akaishauri jamii ya watanzania kutoa taarifa kwa vyombo husika wanapobaini unyanyasaji dhidi ya watoto.

“Tusinyamaze kimya tunapobaini watoto wananyanyaswa,” amesema.


Katika misa hiyo, watoto wa kanisa hilo, Jimbo la Dar es Salaam walimkabidhi Askofu Pengo kiasi cha Sh1.8 milioni ili ziweze kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Kwa upande wake, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa amewapongeza watoto hao kwa kuchanga fedha kwa ajili ya kuwasaidia wenzao wenye mahitaji.

“Endeleeni hivyo hivyo kila mnachokifanya tangulizeni upendo wa Mungu kwa kuwajali wengine, msiwe wabinafsi,” amesema  Nzigilwa.

Mwananchi.

Timu ya watu 50 kumkabidhi Nchi Weah


Wakati wananchi wa Liberia wakiendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi wa duru ya pili ya urais uliofanyika Desemba 26,2017 Rais anayemaliza muda wake Ellen Johnson Sirleaf ametangaza timu ya wataalamu watakaofanikisha mchakato wa kukabidhi madaraka.

Ikijulikana “Timu ya pamoja ya kukabidhi madaraka ya Rais” ndiyo yenye jukumu la kuratibu na kufanikisha hatua zote za ubadilishanaji madaraka kutoka yule anayemaliza muda wake kwenda kwa Rais ajaye.

Kulingana na waraka wa Rais, timu hiyo itaongozwa na marais wawili, anayemaliza muda wake na yule anayesubiri kuingia madarakani.

Iwapo wawili hao watakosekana waziri wa masuala ya nchi ndiye atakayeiongoza.

Pia, itakuwa na wajumbe wengine wanaofikia 50 ambao miongoni mwao ni mawaziri wanaohusika na Mambo ya Nchi na Masuala ya Rais;  Sheria; Mambo ya Nje; Fedha na Mipango; Mambo ya Ndani; na Ulinzi wa Taifa


Rais Sirleaf anamaliza kipindi chake cha uongozi ambapo sasa anatarajiwa kumkabidhi madaraka mwanandinga wa zamani wa Taifa hilo na Klabu ya AC Milan, George Opong Weah ambaye amefanikiwa kumshinda mpinzani wake ambaye pia ni Makamu wa sasa wa Rais.



JPM awaonya viongozi wa umma



Rais John Magufuli amewasilisha fomu ya tamko kuhusu rasilimali na madeni katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyopo Mtaa wa Ohio wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuwasilisha fomu leo Alhamisi Desemba 28,2017 ikiwa ni siku moja baada ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuwataka viongozi kuziwasilisha, ameipongeza sekretarieti kwa kazi inazofanya.

Pia, amemtaka Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Harold Nsekela kutopokea fomu ya kiongozi yeyote ambaye atakuwa hajawasilisha tamko lake ifikapo Desemba 31,2017.

“Ikifika Desemba 31, ambayo ni siku ya mwisho kwa mujibu wa sheria, weka mstari na usipokee fomu zingine, halafu tuone sheria itafanyaje, nakutakia kazi njema,” amesisitiza Rais Magufuli katika taarifa iliyotolewa na Ikulu.

Jaji mstaafu Nsekela amemshukuru na kumpongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza matakwa ya kisheria yanayomlazimu kujaza fomu hizo.

Amesisitiza kuwa ujazaji wa fomu hizo kwa viongozi wa umma si ombi.


Waziri atoa ogizo kwa TANESCO kuhusu Spea za akiba



Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ametoa agizo kwa shirika la umeme nchini TANESCO mkoa wa Kagera kuhakikisha linanunua Spea za akiba ili kuepuka usumbufu kwa wananchi kukosa umeme mara kwa mara.

Dkt. Kalemani ametoa agizo hilo leo wakati akiendelea na ziara yake mkoani Kagera ya kukagua miradi mbalimbali ya umeme.

"Lazima tuwe na Spea sasa hivi sio lazima tusubiri mpaka tatizo litokee ni bora muanze kuagiza mapema Spea ambazo mnahisi hazipo ili linapotokea tatizo la umeme muweze kukabiliana nalo," amesema Dkt. Kalemani.

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani yupo mkoani Kagera katika majukumu yake ya kazi ya kukagua miradi ya umeme mkoani hum