Nigeria wamepangwa kwenye kundi moja na Argentina kwa mara nyingine, Misri nao wakapangwa na Urusi na Uruguay baada ya droo ya Kombe la Dunia 2018 kufanywa nchini Urusi.
Panama, ambao wanacheza Kombe la Dunia mara ya kwanza wamepangwa na Ubelgiji na England na Tunisia.
Iceland, walioshangaza wengi kwa kufuzu, wamepangwa kucheza na Nigeria, Croatia na Argentina katika Kundi D.
Mechi ya ufunguzi itakuwa kati ya Urusi na Saudi Arabia.
Droo kamili ya Kombe la Dunia:
Kundi A: Urusi, Saudi Arabia, Misri, Uruguay
Kundi B: Ureno, Uhispania, Morocco, Iran
Kundi C: Ufaransa, Australia, Peru, Denmark
Kundi D: Argentina, Croatia, Iceland, Nigeria
Kundi E: Brazil, Uswizi, Costa Rica, Serbia
Kundi F: Ujerumani , Mexico, Sweden, Korea Kusini
Kundi G: Ubelgiji , Panama, Tunisia, England
Kundi H: Poland, Senegal, Colombia, Japan.
Fifa wamepokea maombi 3.5 milioni ya tiketi, 300,000 yakiwa maombi ya tiketi za mechi ya fainali uwanjani Luzhniki.
Asilimia 57 ya maombi yametoka kwa wakazi wa nje ya Urusi. Tiketi ya bei nafuu zaidi ya fainali Kombe la Dunia ambayo raia asiye wa Urusi anaweza kununua ni ya £345.