Tanzania\'s leading online News Edition (The National Newspaper). Get access to the most current and latest authoritative news on local issues, politics, events, celebrations, editorial, columnists, features, people and business.
Saturday, 25 November 2017
Lema amueleza Mrisho Gambo maneno haya
Mbunge wa Arusha Mjini, Mh. Godbless Lema amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kutojaribu kufanya hila zozote za kuisababishia CCM ipate ushindi kwenye uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika hapo kesho, Nov 26.
Lema amesema kwmba anafahamu kila hatua na vikao ambavyo Mkuu huyo wa Mkoa na kwamba ana ushahidi wa kutosha wa kila kitu kunachopangwa.
"Mrisho Gambo,unapaswa kujua kwamba huna mamlaka wala uwezo wa kushinda huu uchaguzi kwa nguvu/hila, hakuna kikao umekaa ambacho sina taarifa zake na ushahidi wa kila kitu". Lema
Aidha Lema ameongeza kwa kumkanya kiongozi huyo asijaribu kufanya hivyo.
"Unataka kushinda uchaguzi huu kwa gharama yoyete ile ?sababu polisi wako nyuma yako ? usijaribu" Lema ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter asubuhi ya leo
Kesho kata 43 zinatarajiwa kufanya uchaguzi wa marudio wa kuwapata madiwani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment