Saturday, 25 November 2017

Kumbe Cantona anamkubali Pep zaidi ya Mourinho



Mchezaji nguli wa zamani wa Manchester United Eric Cantona amesema anamkubali kocha wa timu hiyo Jose Mourinho lakini anapenda kuiona klabu yake hiyo ya zamani inacheza kama kikosi cha Pep Guardiola, Manchester City.

Cantona, ambaye alicheza Manchester United kwa  miaka mitano kati ya 1992 na 1997,amemwelezea Mourinho kama kocha mwenye mbinu nyingi za kushinda lakini si kuifanya timu icheze vizuri kama ilivyo kwa Pep Guardiola ambaye huvifanya vyote kwa pamoja.

"Wote Guardiola na Mourinho ni makocha wazuri, lakini mimi napendelea mchezo wa kushambulia zaidi kuliko kujihami kama ambavyo Mourinho anafundisha na huo sio utamaduni wa Manchestweerr United”, amesema Cantona.

"Sielewa kwa nini United ilichukua meneja ambaye anacheza kwa mbinu za kujihami kila wakati.Nampenda Mourinho, lakini napenda kutazama Barcelona ikiwa inacheza kwasababu soka lao linavutia”, ameongeza Cantona.

Cantona amemaliza kwa kuweka wazi kuwa anapenda kuangalia timu inayofundishwa na Guardiola na angependa kuona Mhispania huyo anaifundisha Manchester United kwasababu mara zote soka lake huwa ni lakuvutia zaidi.

No comments:

Post a Comment