Saturday 18 November 2017

Video | Memo _ Hallelujah (COVER) DIAMOND PLATNUMZ FT MORGAN HERITAGE

Video | Memo _ Hallelujah (COVER) DIAMOND PLATNUMZ FT MORGAN HERITAGE



Irene Uwoya atua Rwanda kuhani msiba wa aliyekuwa mumewake

Irene Uwoya atua Rwanda kuhani msiba wa aliyekuwa mumewake


Mrembo wa zamani wa taji la Miss Chang’ombe na mwigizaji maarufu nchini, Irene Uwoya amewasili jijini Kigali, Rwanda kuhani msiba wa aliyekuwa mumewe, Ndikumana Hamad.

Ndikumana aliyekuwa akijulikana kama Katatut, alifariki dunia ghafla siku chache zilizopita na kuzikwa juzi jijini Kigali.

Uwoya hakuwa jijini Kigali wakati wa mazishi na usiku wa kuamkia leo ametua jijini Kigali akiongozana na mwanaye, Klishy ambaye alizaa na marehemu. Pia aliongozana na mama yake mzazi.

Uwoya alijifunika sura muda wote wakati akiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kanombe jijini Kigali.

Wakati anatua, ndugu wakiwemo mashabiki wa michezo na burudani, walijitokeza uwanjani hapo.

Kataut ambaye alicheza soka katika nchi kadhaa za Ulaya, mauti yalimkuta akiwa kocha msaidizi wa Rayon Sports na siku moja kabla ya kifo chake alikuwa mazoezini.

Kwa hapa nchini, Kataut aliwahi kuichezea Stand United kabla ya Kocha Patrick Liewig raia wa Ufaransa, kupendekeza aachwe

Mr Nice amvaa Dudud Baya


Msanii Mr Nice ambaye kwa sasa ameachia kazi yake mpya ya Yaya, amejibu tuhuma za msanii mwenzake Dubu Baya aliposema kwamba maisha yamemshinda na kukimbilia Kenya, na kumjibu kuwa Dudu Baya ni msanii asiyejielewa, ndio maana hana mahali pa kuishi.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Teleivison, Mr.Nice amesema ni wakati sasa Dudu Baya akomae na game kama anavyofanya yeye, kwani muda wa malumbano na kuchafuana hautamsaidia chochote, na hastahili kufanya hayo kwakuwa umri umeshamucha.

Mr. Nice ameendelea kwa kusema kwamba Dudu Baya ni mlevi na anaishi maisha ya kuigiza, hivyo kabla hajaanza kumuongelea vibaya ni vyema akaanza kujilinganisha naye kama wanafanana kimaisha.

Serikali yakarabati vyuo 10 vya ualimu



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa 

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imetumia Sh11.9 bilioni kukarabati miundombinu ya kufundishia, kujifunzia na mabweni katika vyuo 10 vya ualimu nchini.

Amevitaja vyuo hivyo kuwa ni Morogoro, Mpwapwa, Butimba, Kasulu, Songea, Tukuyu, Marangu, Kleruu, Korogwe na Tabora.

“Ukarabati huu umewezesha wanachuo 5,920 waliokuwa wanasoma Stashahada maalumu ya Sayansi, Hisabati na Tehama katika Chuo Kikuu cha Dodoma -Udom kuhamishiwa katika vyuo hivyo,” amesema.

Waziri Mkuu Majaliwa alitoa kauli hiyo jana Ijumaa, Novemba 17,2017 bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa tisa wa Bunge la 11 ambalo limeahirishwa hadi Januari 30, 2018.

Amesema ili kuongeza fursa za wanafunzi kusomea ualimu, Serikali imepanga kujenga na kukarabati vyuo vya ualimu vya Kitangali, Ndala, Mpuguso na Shinyanga kwa thamani ya Sh36.47 bilioni.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema mradi huo ambao utatekelezwa kwa miaka mitatu kuanzia 2016/17 hadi 2018/19, unalenga kuongeza fursa kwa wanafunzi wenye sifa kupata nafasi ya kujiunga na elimu ya ualimu.

“Ujenzi na ukarabati huu utasaidia kuongeza udahili katika vyuo vya ualimu vya Serikali kutoka wanachuo 20,535 katika mwaka 2017 hadi kufikia wanachuo 23,835 katika mwaka 2019, ikiwa ni ongezeko la wanachuo 3,300,” amesema.

Wakati huohuo, waziri mkuu amesema Serikali imeanza maandalizi ya awamu ya pili ya ukarabati wa vyuo saba vya ualimu vya Serikali.

Amevitaja vyuo hivyo kuwa ni Tandala, Nachingwea, Tarime, Kinampanda, Mandaka, Patandi na Ilonga.

Amesema vyuo vya ualimu vya Murutunguru, Kabanga na Mhonda vitalazimika kujengwa upya baada ya wahandisi kubaini kuwa vyuo hivyo havifai kukarabatiwa kutokana na uchakavu mkubwa wa majengo yake.

Afande Sele awapa makavu Bongo Movie


Msanii mkongwe wa muzuki wa kizazi kipya, Selemani Msindi marufu kwa jina la Afande Sele, ameweka wazi juu ya chuki aliyonayo kwa tasnia ya filamu bongo (bongo movie).

Akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio, Afande Sele amesema hawachukii wasanii wa bongo movie, bali huchukia tabia zao chafu ambazo zinaharibu Tasnia.

Afande Sele ameendelea kwa kusema kwamba wasanii wa bongo movie wana tabia chafu hasa za kuwanyanyasa wanawake kwa kuwatumikisha kingono, huku akimtolea mfano muigizaji Elizabeth Michael (Lulu) ambaye amefungwa.

Waziri Mkuu Canada Aijibu Serikali ya Tanzania Sakata la B



Wakati katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akiwa nchini Canada kushughulikia suala la ndege ya Bombardier, waziri mkuu wa nchi hiyo, Justin Trudeau amesema hawezi kuingilia uhuru wa mahakama ambayo anaamini itatenda haki.

Hivi karibuni Rais John Magufuli alisema amemwandikia barua waziri huyo mkuu wa Canada ili kujua hatima ya ndege hiyo.

Hata hivyo naibu waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye alisema jana kuwa hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa sababu waziri mkuu yupo na wao hawajapata taarifa rasmi.

“Lakini kingine naomba utambue kuwa katibu mkuu bado yupo Canada, kwa hiyo mambo mengi mimi sijayapata hadi atakaporudi aje kutu-breaf kilichojiri huko,” alisema Nditiye.

Akizindua uwanja wa ndege mjini Bukoba, Novemba 6, Rais Magufuli alisema amemwandikia barua waziri mkuu wa Canada kumuomba kuachiwa kwa ndege hiyo na amemtuma mwanasheria mkuu wa Serikali, George Masaju kwenda nchini humo kushughulikia suala hilo.

Kwenye barua yake ya majibu ambayo yameripotiwa na gazeti la National Post la nchini humo, waziri mkuu wa Canada Trudeau amesema hana cha kufanya kwa kuwa shauri hilo lipo mahakamani.

“Ni bahati mbaya kwamba suala hili limechelewesha kuwasili kwa ndege hii. Serikali ya Canada haina uwezo wa kuingilia, ila tuna imani mahakama itaamua kwa weledi na haki,” amekaririwa akisema Trudeau katika gazeti hilo.

Ndege hiyo, Bombardier Q400-8 inashikiliwa kwa amri ya mahakama nchini humo kutokana na shauri lililopo kati ya Serikali na kampuni ya Stirling Civil Engineering.

Kampuni hiyo ilikuwa na mkataba wa ujenzi wa Barabara ya Wazo Hill – Bagamoyo ambao ulivunjika kabla haujakamilika, hivyo ikaamua kukimbilia kwenye Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa ambako ilishinda kesi. Baada ya kushinda kampuni hiyo ilipewa kibali cha kukamata mali za Tanzania katika nchi za Ufaransa, Uholanzi, Uingereza, Ubelgiji, Uganda na Canada.

Kwa miezi mitatu sasa, mahakama nchini Canada inaendelea kuishikilia ndege hiyo iliyonunuliwa kwa Dola 32 milioni za Marekani (zaidi ya Sh70.4 bilioni) kwa niaba ya kampuni ya Stirling inayoidai Serikali Dola 28 milioni (zaidi ya Sh61.6 bilioni) ambazo ni thamani ya mkataba uliovunjwa pamoja na riba.

Ndege hiyo ni miongoni mwa zile ambazo Rais Magufuli aliahidi kununua ikiwa ni mikakati ya kulifufua Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).

Awali, ndege hiyo litarajiwa kuwasili nchini mwezi Julai, lakini hilo halikufanyika na Agosti 18, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema ndege hiyo imekamatwa nchini Canada na inaweza kupigwa mnada kutokana na deni ambalo Serikali inadaiwa na kampuni hiyo yenye makao yake Montreal, Canada.

Agosti 19, Serikali ilifanya mkutano na wanahabari kukanusha taarifa hizo, lakini ilikiri kuwapo mgogoro na kampuni hiyo.

Aliyekuwa kaimu mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Zamaradi Kawawa alisema mgogoro kuhusu ndege hiyo upo na kimsingi umetengenezwa na Watanzania ambao kwa bahati mbaya wameweka masilahi ya kisiasa na ya binafsi mbele zaidi ya masilahi ya Taifa.

Alisema Serikali ilikuwa imeanza majadiliano ya kidiplomasia kwa ajili ya kulimaliza suala hilo. Kwa sasa, ATCL inamiliki ndege mbili mpya aina ya bombardier zilizoingia nchini Septemba 2016, na imeagiza ndege nyingine tatu za aina hiyo na Boeing Dreamliner moja.

Akizungumzia mafanikio ya miaka miwili ya Rais John Magufuli hivi karibuni msemaji mkuu wa Serikali, Hassan Abbasi alisema mpaka Juni mwakani ndege zote zitakuwa zimewasili nchini.

Mbowe Awataka Viongozi wa Dini Wasione Aibu Kuikosoa Serikali




Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amewataka viongozi wa dini kupaza sauti kukemea maovu ili kuiokoa nchi katika kilio.

Mbowe  alisema hayo jana wakati wa ibada ya kumuaga marehemu mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la Hai, Looka Mushi iliyofanyika katika Usharika wa Nkwarungo.

“Dunia yetu imejaa uovu, sisi ambao tuko kwenye siasa tunatambua nguvu ya viongozi wa kiroho, kauli yao moja kukemea uovu inatingisha nchi nzima,” alisema Mbowe. “Semeni tunatambua tangu enzi mmekuwa mkikemea maovu na ‘kui-shape’ nchi, msione aibu kuwakemea viongozi waovu.

“Viongozi wa dini msiingize roho ya uoga, mtaiponya nchi, mkikaa kimya nchi itakufa, nchi inateketea, nchi inaangamia viongozi msikae kimya watu wanauawa.

“Itafika kipindi kwa kiburi cha madaraka wataamrisha baba askofu alale rumande kwa mfano, Mungu akunusuru sana Baba Askofu Dk Frederick Shoo atakapoambiwa alale ndani ndiyo utakuwa ukombozi wa Taifa letu Bwana Yesu asifiwe,” alisema Mbowe.

Kwa upande wake, Askofu Shoo alisema viongozi wa dini waache unafiki na waige mwenendo wa Mchungaji Mushi.

“Watumishi wengi ni wanafiki, hivyo waache unafiki na kuwa na rangi mbilimbili muige mwenendo wa mchungaji Mushi,” alisema Dk Shoo.

Askofu mstaafu Erasto Kweka alisema matendo mema yaliyotangauliza neno la Mungu ndiyo silaha ya kweli ya kila binadamu.

Alisema jambo muhimu ni kuishi kwa kuangalia waliofanikiwa katika imani walifanya nini.

“Leo tunamuaga mpendwa wetu, anayesifiwa na kila mmoja kutokana na kutukuka kwa matendo yake mema, tutafakari na kutenda kwa kumpendeza Mungu kama alivyofanya Mchungaji Mushi,” alisema Kweka.

Muhubiri katika ibada hiyo, Mchungaji Lewis Hiza alisema watu wanashangaa kwa nini alikuwa na urafiki na Mchungaji Mushi.

“Jibu ni kuwa wazee wanaozeeka vizuri, huwa na urafiki na vijana ili kuwaachia yaliyo mema na neno alilokuwa akiniambia kila siku nishike neno kwa sababu litaniweka pazuri na litakuwa majibu ya kila swali,” alisema Hiza.

Akisoma wasifu wa marehemu, katibu mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini, Arthur Shoo alisema Mchungaji Mushi alipata tatizo la mapafu mwaka 2008 na kupata matibabu katika hospitali mbalimbali.

Alisema mwaka 2014 aliugua na kufanyiwa upasuaji na kutolewa uvimbe tumboni katika Hospitali ya Manipal Bangalore nchini India.

“Pia mwaka huohuo alifanyiwa upasuaji wa kuondoa tezi dume. Mwaka 2015 alirudi tena India kwa uchunguzi, alionekana anaendelea vizuri japokuwa aliendelea kusumbuliwa na tatizo la mapafu ambalo mzizi wa tatizo ulianza kwenye ugonjwa wa pafu mpaka alipofariki Ijumaa iliyopita,”alisema Shoo

Aishi Manula akalishwa na Rekodi za Manyika Jr


Peter Manyika Jr ambaye ni golikipa wa Singida United amemkalisha  golikipa wa Simba Aishi Manula kwa kucheza mechi nyingi bila kuruhusu goli (clean sheets). Mechi ya jana ambayo Singida walishinda 1-0 dhidi ya Lipuli,Manyika alifikisha jumla ya michezo saba bila kufungwa katika mechi 10 za VPL zilizopita.

Manula ambaye ndiye golikipa namba moja wa kikosi cha Taifa Stars, hajaruhusu goli katika mechi tano za VPL kati ya mechi tisa alizocheza hadi sasa. Amezidiwa cleans sheets mbili na Mayika Jr lakini wawili hao wametofauiana katika idadi ya mechi walizocheza. Manyika tayari amecheza michezo 10 wakati Manula akiwa na mechi tisa huku leo akitarajiwa kucheza mechi yake ya 10 VPL wakati Simba itakapokuwa ikicheza dhidi ya Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine Mbeya.

Manyika Jr taratibu anarejea kwenye ubora wake baada ya kuondoka Simba alipokuwa ‘anachoma mahindi’ kwa muda mrefu. Uwepo wa magolikipa wa kigeni Vicent Angban na Daniel Agyei kwa nyakati tofauti ulipelekea Manyika Jr kupoteza nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza pale Msimbazi.

Jana Ijumaa November 17, 2017 Manyika Jr ameandika rekodi yake ya kucheza mechi saba bila kuokota mpira ndani ya nyavu zake katika mechi 10 ambazo amesimama langoni, huku mchezo wa jana ukiwa ni wa tano mfululizo bila kufungwa. Hili si jambo dogo kwake amefikia rekodi ya golikipa wa Azam Razak Abarola ambaye hajaruhusu goli katika mechi saba za VPL katika mechi tisa alizocheza.

Clean sheets za Manyika Jr katika mechi 10 za VPL msimu huu

Stand United 0-1 Singida United

Singida United 1-0 Kagera Sugar

Ruvu Shooting 0-0 Singida United

Ndanda 0-0 Singida United

Mtibwa Sugar 0-0 Singida United

Singida United 0-0 Yanga

Singida United 1-0 Lipuli

Clean sheets za Manula katika mechi 9 zilizopita VPL msimu huu

Simba 7-0 Ruvu Shooting

Azam 0-0 Simba

Simba 3-0 Mwadui

Simba 4-0 Njombe Mji

Mbeya City 0-1 Simba

Baba mzazi wa golikipa huyo Manyika ambaye ni golikipa wa zamani wa Yanga na Taifa Stars alishawahi kuiambia shaffihdauda.co.tz kuwa,  kushuka kiwango kwa kijana wake wakati akiwa Simba kulichangiwa na mambo mengi ya nje ya uwanja na kutozingatia miiko ya soka.

Badae Manyika Jr alirudi kwa mzee wake baada ya kugudua amekosa mwelekeo na kipaji chake kimekosa njia, alipokelewa na baba yake kisha kurejeshwa kwenye kituo cha magolikipa kinachomilikiwa na baba yake (Manyika Sr) pale Karume. Alianzishiwa mazoezi maalum ya kupunguza uzito na kuwekwa fit hatimaye akarejea katika hali yake.

Baba yake ambaye ndio meneja wa mtoto wake alisema, mkataba wa Manyika Jr na Simba utakapomalizika hawatakubali kuongeza mwingine badala yake watamtafutia timu nyingine ambayo wataweka masharti ya kimkataba kuhakikisha anacheza mechi nyingi pale anapokuwa fit, hapo ndipo safari ya kwenda Singida United ikawadia baada ya timu hiyo kujiridhisha na ubora aliokuwanao Manyika Jr wakati huo.

Ubora wa Manyika katika milingoti mitatu umemrejesha Stars

Baada ya kufanya vizuri katika mechi za ligi kuu, kocha wa Stars Salum Mayanga alianza kumuita Manyika Jr kwenye timu ya taifa ili kutoa changamoto kwa Aishi Manula. Inawezekana wengi waliamini Manyika ndio basi tena, lakini baada ya kugundua alikosea wapi na anatakiwa kufanya nini amesimama kwa mara nyingine na kuwaamisha watu bado kipaji chake hakijapotea.

Manyika Jr vs Abarola

Wote hawajaruhusu magoli katika mechi saba hadi sasa, Manyika amecheza mechi 10 wakati Abarola amecheza mechi tisa. Abarola ndio wa kwanza kufikisha mechi saba bila kuruhusu goli lakini Manyika ameifikia rekodi hiyo ya golikipa kutoka Ghana baada ya mchezo wa jana Singida United 1-0 Lipuli.

Manyika Jr anampiku Abarola kwa kucheza mechi tano mfululizo bila kufungwa goli, katika mechi tano zilizopita mfululizo Manyika Jr ameidakia Singida United bila kuruhusu wavu wa goli lake kucheza. Abarora aliwahi kucheza mechi nne mfululizo za mwanzo wa ligi bila kufungwa, Abarola aliruhusu goli la kwanza dhidi ya Singida United timu hizo zilipotoka sare ya kufungana 1-1 kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma

Leo Jumamosi Nov 18, 2017 Abarola yupo kwenye nafasi ya kufikisha mechi nane bila kufunga na kumwacha  Manyika Jr endapo hatafungwa kwenye mchezo kati ya Njombe Mji dhidi ya Azam kwenye uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe


Vifo vya watoto njiti kudhibitiwa




Dar/Zanzibar. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya amesema Serikali inaendelea kupambana na vifo vya watoto njiti baada ya takwimu kuonyesha tatizo hilo ni la pili kusababisha vifo vingi nchini.

Takwimu za mwaka 2015 zinaonyesha kati ya watoto 200,036 waliozaliwa kabla ya siku zao (njiti), 9,400 walifariki dunia kutokana na huduma duni.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Watoto Njiti Duniani yaliyofanywa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Ujerumani, Dk Mpoki alisema kukosekana kwa weledi wa kuwahudumia watoto hao wanapozaliwa na uhaba wa vifaa, huchangia vifo hivyo.

Alisema kutokana na tatizo hilo, wataalamu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) kwa kushirikiana na Ujerumani walifanya utafiti na kubaini kuwa hali ni mbaya zaidi katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Dk Gwenchele Mkenge alikiri hali ya mkoa huo ilikuwa mbaya kabla ya kuanza kwa mradi wa kuokoa maisha ya watoto njiti.

Meneja wa Mradi wa Ujerumani wa Kusaidia Afya, Dk Susanne Grimm alisema inawezekana kuokoa vifo vya watoto njiti kwa kuwa wana haki ya kuishi kama wengine.

Alisema nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania kuokoa maisha ya mama na mtoto kwa kuhakikisha wanapatiwa huduma bora na stahiki.

Wakati huohuo, watoto njiti 335 wamezaliwa Zanzibar mwaka huu, ikiwa ni idadi kubwa ikilinganishwa na watoto 206 waliozaliwa mwaka 2016.

Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar, Moudeline Castico alisema hayo mjini Unguja jana. Alisema idadi hiyo ni kubwa, hivyo kunahitajika nguvu ya wananchi na Serikali kupitia wataalamu wa afya kutafuta njia ya kuvipunguza.

Mbunge Heche kuripoti Polisi



Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche 

Morogoro. Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche amesema ataripoti polisi mkoani Morogoro kuitikia wito wa jeshi hilo.

Heche amesema ataripoti polisi Jumatatu Novemba 20,2017 kwa kuwa ana taarifa kwamba anatafutwa na jeshi hilo.

Polisi walioelezwa kutoka mkoani Morogoro jana Ijumaa Novemba 17,2017 walifika eneo la Bunge na Heche alilieleza Mwananchi kuwa walimpatia wito kuwa anatakiwa kwenda kuhojiwa mkoani Morogoro.

Heche pia alieleza hofu yake kwamba polisi walikuwa wamkamate, hata hivyo hilo halikufanyika.

Mbunge huyo alisema hajui kosa alilotenda, isipokuwa anatakiwa kuhojiwa kwa kauli alizotoa alipomsindikiza mbunge wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali alipotoka gerezani.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Novemba 18,2017 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amesema mbunge huyo alifanya mkutano wa hadhara wilayani Kilombero Aprili 8, 2017.

Kamanda Matei alisema wanamtafuta Heche kwa kosa la kutotii amri za viongozi na kufanya mkutano Kilombero na kutoa lugha ya matusi hivyo kutaka kusababisha vurugu.

Amesema tangu siku ya tukio jeshi hilo limekuwa likimtafuta mbunge huyo bila mafanikio ndipo lilipoamua kulishirikisha Bunge.

Polisi iliandika barua kwa Spika wa Bunge kumtaarifu kuwa mbunge huyo anatafutwa kwenda kujibu tuhuma zinazomkabili mkoani Morogoro.

"Barua ni mambo ya siri kati ya jeshi na Bunge, tunachotaka sisi ni kumuona Heche hapa na asitake tutumie nguvu," amesema Kamanda Matei alipoulizwa kuhusu barua waliyoiandika kwa spika.

Nafasi za kazi leo November 18

KAMA UNATAFUTA SCHOLARSHIPS BASI HAPA NDIPO PENYEWE


Elimu solutions company limited ni kampuni ya kitanzania iliosajiliwa kwa ajili ya kufanya shughuli mbali mbali za kielimu.

ikiwemo kufanya shughuli za udahili wa wanafunzi katika vyuo vikuu mbalimbali  nchi china  kwa ngazi tofauti.

Kama wewe ni mmoja wapo unatafuta Scholarships basi wasiliana na sisi

TUNAPATIKANA
Elimu Solutions Tanzania Ltd. NHC Building Biashara Complex 1st Floor Suite No. 106 Mwananyamala Komakoma P.O. Box 5678, Dar es Salaam Tel: +255 22 2760260 Fax: +255 22 2760260 Mob: +255 718 782 424 +255 744 544 443 www.elimusolutions.co.tz  Hartmann O. Mbilinyi DIRECTOR OF LOGISTICS & FACILITATIONS.












Dk Shika aibuka na hili

Dk Shika aibuka na hili



Dar es Salaam. Dk Louis Shika, ambaye alijizolea umaarufu baada ya kushinda zabuni ya kununua nyumba tatu za kifahari kwa takriban Sh3 bilioni lakini akashindwa kulipa asilimia 25 ya fedha hizo, amedai ameanza mchakato wa kurejesha fedha zake zilizo nje ya nchi.

Dk Shika amedai leo Jumamosi Novemba 18,2017 kuwa amelipa dola 100 za Kimarekani (sawa na Sh220,000 za Kitanzania) kwa ajili ya bima ili aweze kutumiwa fedha zake nchini.

Waandishi wa habari waliokuwa katika ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye aliyeenda Shirika la Posta kuzungumza na wafanyakazi, walimkuta Dk Shika akiwa katika shirika hilo na walipozungumza naye alisema alifika hapo kwa ajili ya malipo.

Dk Shika, ambaye alishikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano akituhumiwa kuvuruga mnada wa nyumba hizo za mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam, Said Lugumi, alisema ametumia shirika hilo kulipa fedha hizo za bima kwa benki moja iliyoko Bangkok, Thailand.

"Kama mnavyoona hii karatasi,” alisema akionyesha fomu ya malipo.

“Nimelipa dola 100 za bima ili kukamilisha fedha zangu zije na nilipie zile nyumba. Hili la bima lilikuwa ni muhimu sana."

Hata hivyo, moja ya nyumba hizo tatu ilishauzwa kwa mshindi wa pili kwenye mnada huo, wakati kampuni ya udalali ya Yono imesema itaendesha mnada mwingine kuuza zilizosalia.

‘Bilionea’ huyo hakueleza fedha alizolipia ni kwa ajili ya kuingiza nchini kiasi gani cha fedha.

Dk Shika amesema bado anaamini kwamba nyumba hizo atazimiliki ili kuwaziba mdomo wale wote wanaombeza kwamba hana fedha

Waziri wa Fedha asema kuomba misaada kunadhalilisha Taifa



Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango 

Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema amechoka kuomba misaada nchi za nje kwa sababu ni aibu na hilo linalidhalilisha Taifa.

Dk Mpango amesema hayo leo Jumamosi Novemba 18,2017 alipofunga mafunzo ya wadadisi, wasimamizi na wahariri wa takwimu za mapato na matumizi binafsi katika ngazi ya kaya.

"Lazima tufanye kazi kwelikweli. Mimi kwa miaka kadhaa natumwa kwenda kutafuta misaada huko nje ya nchi, nimechoka. Imekuwa ikidhalilisha Taifa, wanasema kweli sisi ni nchi ya tatu katika upatikanaji wa dhahabu halafu waziri wao wa fedha  anakuja kuomba," amesema.

Dk Mpango amesema ni lazima kama nchi iwe na mkakati kuondokana na hali hiyo na kwamba, malengo yatafikiwa kama makusanyo ya takwimu yatafanyika na kutumiwa kwa weledi na umakini.

"Hamna budi kufuata sheria na kanuni za utumishi. Taarifa mtakazozipata ni za siri hamtakiwi kutoa kokote ni kwa ajili ya matumizi ya takwimu pekee. Mkifanya vinginevyo Mahakamani," amesema.

Dk Mpango amesema watakaovuruga kazi  inayoanza mwezi huu na kumalizika baada ya miezi sita watabanwa.

"Siku za nyuma kuna watu walikwenda kukusanya takwimu wakaleta tukaanza kuulizana ni kwa nini idadi ya watu imepungua? Kumbe walikwenda kupika takwimu katika mikorosho, msiende kutusaliti," amesema.

Amezitaka kaya zilizochaguliwa kutoa taarifa sahihi wanapofikiwa na wadadisi wa takwimu na viongozi wa ngazi ya Taifa hadi vijiji kutoa ushirikiano kwa wadadisi wanapofika kwenye maeneo yao.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu, Dk Albina Chuwa amesema kwa kutumia teknolojia wameweza kupunguza matumizi kutoka Sh20 bilioni hadi Sh10 bilioni, fedha ambazo zitakamilisha kazi hiyo.

Amesema huo ni utafiti wa saba na kwamba, watahakikisha wanatoa matokeo ya awali ya utafiti katika kipindi cha miezi sita kuanzia sasa ili yaweze kufanyiwa kazi.

"Nendeni mkafanye kazi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa bila kufanya udanganyifu wowote maana hatutashindwa kuchukua hatua kwa wale wote watakaobainika kufanya udanganyifu," amesema.

Dk Chuwa amesema kaya zisizopungua 10,460 zitahusika katika utafiti huo utakaohusisha wadadisi 620 baada ya wengine kuondolewa baada ya kushindwa mtihani kwa kupata chini ya asilimia 60.

Raia wamshinikiza Mugabe kujiuzulu



Raia wajitokeza Zimbabwe kumshinikiza Mugabe kung'atuka mamlakani

Maelfu ya raia wa Zimbabwe wamejitokeza barabarni hasa mjini Harare wakijiandaa kwa mkutano mkubwa unaoungwa mkono na chama tawala ZANU-PF katika jitihada za kuongeza shinikizo za kumtaka rais Mugabe ajiuzuulu,wakishikilia mabango yaliyoandikwa Mugabe Must Go.

Zanu-PF ndio chama kilichomsaidia Mugabe kuwa madarakani nchini kwa takriban miaka 40.

Lakini sasa inabidi wamshinikize ajiuzulu kufuatia mpasuko mkubwa katika chama tawala.

Kikubwa kinachozozaniwa ni nani atakayemrithi rais Mugabe atakapoochia madaraka.

Jeshi la nchi hiyo lilichukua hatamu za kiserikali na kumweka Mugabe chini ya kizuizi cha nyumbani tangu juzi na wamekuwa wakifanya mazungumzo ya kina.

MUgabe angependelea mkewe kumrithi lakini wapiganiaji wa uhuru nchini humo wanamtaka aliyekuwa makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa ambaye Mugabe alimfuta kazi wiki iliyopita, kutokana na uhasama mkubwa baina yake na mkewe rais Mugabe uliotokana na upiganiaji huo wa madaraka.

Zaidi ya hayo Bw. Mugabe angependa kuendelea kuwa uongozini hadi chama kitakapofanya mkutano wao mkuu mwezi ujao

Serikali yakiri umasikini kuwa juu

Serikali yakiri umasikini kuwa juu


Serikali imesema asilimia 28.2 ambayo ni sawa na Watanzania zaidi ya milioni 2 hawapati mahitaji ya msingi, na kwamba kiwango cha umasikini nchini bado kipo juu.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango, wakati wa uzinduzi wa zoezi la ukusanyaji wa takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi Tanzania bara kwa mwaka 2017/18, na kusema kwamba ni dhahiri kiwango cha umasikini kwa wananchi bado kipo juu.

Zoezi la ukusanyaji wa takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi litafanyika katika mikoa yote ya Tanzania bara, na kutarajiwa kufikiwa kaya 10,460, huku ikielezwa kwamba kukamilika kwa zoezi hilo kutawezesha serikali kutathmini hatua zilizofikiwa katika mpango wa pili wa maendeleo ya taifa, na utekelezaji wa malengo endelevu.

Ukusanywaji wa takwimu na utafiti huo unafanywa na wadadisi 620 walioandaliwa, ambapo mkurugenzi mkuu ofisi ya taifa ya takwimu Dk. Albina Chuwa, amewataka kutoa taarifa za ukweli, vinginevyo watakaodanganya watawajibishwa kwa mujibu wa sheria ya takwimu ya mwaka 2015.

Tazama video hapa chini Waziri Mpango akielezea hilo

Mke anyongwa na mumewe baada ya kumnyima tendo la ndoa


Maafisa wa polisi wanasema kuwa mwanamume mmoja katika jimbo la kaskazini mwa India la Haryana amemuua mkewe baada ya kukataa kushiriki naye tendo la ndoa.

Sanjiv Kumar mwenye umri wa miaka 35 alidaiwa kumyonga mkewe ,Suman wakati wa vita siku ya Jumanne.

Mwanamume huyo alikiri kutekeleza kitendo hicho baada ya kukamatwa , afisa wa polisi Ramesh Jaglan aliambia BBC.

Migogoro ya kiyumbani ndio yenye visa vingi vilivyoripotiwa dhidi ya wanawake nchini India kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.

''Alikuwa akikataa kufanya ngono kwa muda .Siku ya Jumanne alikataa tena, hatua iliomuudhi na kuamua kumnyonga.Tumemkamata'', bwana Jaglan aliambia BBC.

Wanandoa hao walikuwa wameoana kwa zaidi ya muongo mmoja. Wana watoto wawilii.

Ndege yachora sehemu nyeti angani

Ndege yachora sehemu nyeti angani


Onyo: Baadhi ya watazamani huenda wakaona picha hizi kama zisizo na maadili.

Maafisa wa jeshi la wanamaji wamesema kwamba haikubaliki kwamba mmoja wa marubani wake alitumia ndege moja ya kijeshi kuchora uume wa mwanadamu angani.

Mchoro huo uliokuwa katika kaunti ya Okanogan magharibi wa jimbo la Washington nchini Marekani ulizua hisia nyingi katika mitandao ya kijamii.

Lakini makomando katika kituo hicho cha wanamaji kilichopo katika kisiwa cha Whidbey hawakuona ucheshi wake na sasa wameanzisha uchunguzi.

Msemaji wa kambi hiyo ya kijeshi alithibitisha kuwa ndege iliohusika kuchora uume huo kwa kutumia moshi wake ni ile ya Boeing EA-18G Growlers.

Ndege hiyo hutumika maalum kwa vita vya kielektroniki na inaweza kusafiri mara mbili kasi ya sauti.

Msemaji Thomas Mills aliambia BBC : Mimi kama mwanamaji tunawapatia heshima kubwa marubani wetu na hili halikubaliki hata kidogo.

Watazamaji waliokuwa chini ardhini walichekeshwa na mchoro huo.

Source: BBC

Ngoma, Kamusoko waondolewa kikosi cha Yanga kesho

Ngoma, Kamusoko waondolewa kikosi cha Yanga kesho



Donald Ngoma (kushoto) akifanya yake.

WAZIMBABWE, Thabani Kamusoko na Donald Ngoma, wameondolewa katika kikosi cha Yanga kitakachocheza na Mbeya City kesho kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kocha wa Yanga, George Lwandamina, raia wa Zambia, amewatoa katika mipango yake nyota hao kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City.

Kamusoko anayecheza nafasi ya kiungo na Ngoma ambaye ni straika, wote kwa sasa ni majeruhi na tayari kocha huyo amewatafutia mbadala wao ambao watacheza mechi hiyo.

Daktari wa Yanga, Edward Bavu, ameliambia Championi Jumamosi kuwa, wachezaji hao bado wana matatizo kwani Kamusoko anaumwa kifundo cha mguu na Ngoma anasumbuliwa na nyama za paja.
“Kamusoko na Ngoma wameondolewa katika mipango ya kocha kuelekea mechi ya wikiendi hii, maana hawataweza kuwa sawa kwa siku moja,” alisema Bavu.

Kwa wiki nzima, wawili hao hawakufanya mazoezi ya maandalizi ya mchezo wao wa kesho na huenda
wakaonekana tena uwanjani mwezi ujao kama watakuwa fiti.

Mara ya mwisho kwa nyota hao kuonekana uwanjani, ilikuwa kwenye mechi ya ligi kuu msimu huu dhidi ya Mtibwa Sugar, iliyopigwa Septemba 30 kwenye Uwanja wa Uhuru na kumalizika kwa suluhu

Wasanii wa filamu waumbuliwa na Waziri Mwakyembe

Wasanii wa filamu waumbuliwa na Waziri Mwakyembe


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe amewataka wasanii wa filamu Tanzania kuacha kutumia 'soundtrack' kwenye filamu za kitanzania ili kuleta uhalisia wa utamaduni wetu, kwani kufanya hivyo ni ushamba mkubwa.

Waziri Mwakeyembe ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wageni waliofika kwenye uzinduzi wa television mpya ya Jasson, ambayo itakuwa inaonyesha kazi za sanaa za Tanzania, na kuwataka wasani wa Tanzania kutumia viu vya kitanzania ili kutangaza Utanzania na kuwa na maudhui ya Mtanzania.

"Soundtrack hakuna sababu kwa nchi tajiri kwa muziki kama Tanzania kwa msanii wa Kinyakyusa, msanii wa Kimakonde kutumia soundtrack eti za kizungu, ashakhum si matusi huo ni ushamba kwa kweli, ni matarajio ya wizara  baada ya miaka kadhaa mtu akisikia soundtrack ya , Mdumange, Mganda, Sindimba ajue anaangalia filamu ya Tanzania", amesema Waziri Mwakyembe.

Pamoja na hayo Waziri Mwakyembe amewataka wasanii hao kuzingatia matumizi ya lugha ya Kiswahili, ambayo kwa sasa inatambulika zaidi dunian

Thursday 16 November 2017

Breaking: Hatimaye Mhasibu mkuu wa Takukuru afikishwa mahakamani

Breaking: Hatimaye Mhasibu mkuu wa Takukuru afikishwa mahakamani



MHASIBU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai,  anayedaiwa kumiliki mali nyingi kuliko kipato chake, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma zinazomkabili.

Gugai amefikishwa katika mahakama hiyo baada ya taarifa iliyotolewa siku chache zilizopita na Naibu Kamishna wa Takukuru, Brigedia John Mbungo,  kwamba mtuhumiwa huyo alikuwa ametoroka.  Mtuhumiwa huyo anatajwa kumiliki majumba na viwanja karibu kila mkoa nchini.