Saturday, 25 November 2017

Mkutano wa Chadema wavamiwa na watu wasiojulikana




Watu  wasiofahamika  wamevamia  na kuvunja vifaa vya muziki vilivyopangwa kutumika katika mkutano wa kampeni za udiwani wa Kata ya Mbweni wilayani Kinondoni.

Meya wa Ubungo, Boniface Jacob  akiwa pamoja na Mbunge , Tarime Vijijini John Heche na Mbunge wa Kawe Halima Mdee ameliambia gazeti hili  leo Novemba 24, 2017 kuwa tukio lilitokea saa 9 alasiri katika uwanja wa  Mbweni Vijijini.

 Jacob ambaye pia ni diwani wa Kata ya Ubungo, amesema  wakati watu wakiwa pembeni wakisubiri viongozi na wanachama kufika eneo hilo ghafla lililotekea gari ndogo lililobeba vijana hao ambao walishuka na kufanya uharibifu huo.

“Walivunja muziki wote uliokuwa uwanjani kisha kuvunja kioo cha gari la matangazo  lililokuwa likitumika kuhamasisha watu kuhudhuria mkutano huu,” amesema Jacob.

Amesema hadi sasa bado hawajawatambua  watu hao ambao wamefanya uharibifu huo na kwamba, hali ya utulivu imerejea katika eneo baada ya polisi kuwasili na wakati wowote mkutano utaanza wa kumnadi mgombea wao.

No comments:

Post a Comment