Mshambuliaji wa Everton Oumar Niasse amepigwa marufuku ya mechi mbili kwa kupatikana na hatia ya kujirusha.
Mshambuliaji huyo wa Senegal ni mchezaji wa kwanza katika ligi ya Uingereza kupewa adhabu chini ya sheria za shirikisho la soka nchini Uingereza ambazo zilizinduliwa mnamo mwezi Mei.
Niasse alikabidhiwa penalti iliozua utata na refa Ccott Dann wakati wa mechi ya Jumamosi ambapo timu yake ilitoka sare ya 2-2 dhidi ya Crystal Palace.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 atakosa mechi ya Everton dhidi ya Southampton siku ya Jumapili na ile ya nyumbani dhidi ya West Ham tarehe 29 mwezi Novemba.
Tume huru ya shirikisho la soka nchini Uingereza ilitoa uamuzi huo kwa pamoja katika kumpata na hatia mchezaji huyo wakati ilipokutana siku ya Jumatano.
Niasse alikana kufanya makosa, hatua iliosababisha penalti kukabidhiwa katika dakika ya tano ya mchezo.
Leighton Baines alifunga mkwaju huo kabla ya Niasee kuifungia timu yake goli la kusawazisha katika uwanja wa Selhurst Park.
No comments:
Post a Comment