Thursday, 23 November 2017

Lema afunguka kuhusu Kafulila



Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA Godbless Lema, amefunguka kuhusu kitendo cha David Kafulila kuhama CHADEMA na kusema ana amini atamshauri mke wake naye afuate nyayo zake.

Kwenye ukurasa wake wa twiter Godbless Lema ameandika ujumbe akisema Kafulila ni rafiki yake wa karibu, lakini kwa namna alivyoamua hana shaka atamshauri mke wake ambaye ni mbunge kupitia chama cha CHADEMA, kufanya kama yale aliyoyafanya.

"David Kafulila ni rafiki yangu, nafikiri kwa namna hii alivyoamua ataweza bila shaka kumshauri Mbunge wa Chadema, Jesca Kishoa (mke wake) kufikiri kama yeye, hii inaweza kusaidia maoni yake juu ya uamuzi aliouchukua leo na kuthibitisha ukweli huu kama hupo", ameandika Godbless Lema.

Hii leo David Kafulila ametangaza kukihama chama cha CHADEMA akidai vyama vya upinzani havina nia ya kupambana dhidi ua ufisadi, lakini mke wake Jesca Kishoa ambaye ni mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA bado hajazungumza chochote.



No comments:

Post a Comment