
Baada ya jeshi kuchukua utawala nchini Zimbabwe,mkutano wa pili untarajia kufanyika kwa ajili ya kumshauri rais Robert Mugabe kuyaachia madaraka.
Kwa mujibu wa habari,katika mkutano ujao padri wa Katoliki Fidelis Mukonor,Waziri wa Ulinzi Aaron Nhepera na msemaji wa Mugabe George Charamba watahudhuria.
Ripoti zimeonyesha kuwa wananchi wamekuwa wakikusanyika barabarani wakimtaka rais Mugabe ajiuzulu.
Toka Jumatano jeshi kuu la Zimbabwe limechukua utawala wa nchi hiyo mpaka pale hatma itakapojulikana.
No comments:
Post a Comment