Wednesday, 22 November 2017

Ufaransa yathibitisha kuwapokea wahamiaji kutoka Libya watakao safirishwa na UNHCR



Ufaransa yatangaza kuwa itawapokea wakimbizi wa kwanza watakao safirishwa na shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kutoka nchini Libya

Serikali ya Ufaransa imetangaza kuwa utawapokea wakimbizi na wahamiaji wa kwanza watakaosafirishwa na shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kutoka nchini Libya.

Taarifa zinafahamisha kuwa wakimbizi watakao pokelewa na Ufaransa ni raia 25 kutoka Erytrea , Sudan na Ethiopia.

Wakimbizi hao watapokelea mwanzoni mwa Januari mwaka 2018.

Taarifa hiyo ilitolewa na Pascal Brice  mkurugenzi wa ofisi inayosimamia haki za wakimbizi baada ya mkutano uliofanyika Vovemba 20 mjini Niamey nchini Niger.

No comments:

Post a Comment