Sunday, 19 November 2017

Mugabe kukutana na makamanda wa jeshi leo



 Washirika wa karibu wa Rais Robert Mugabe kwenye chama alichokianzisha wanamtaka ajiuzulu wakati shinikizo dhidi yake zikiongezeka kufuata hatua za jeshi kutwaa madaraka.
Maafisa wa vyeo vya juu chamani wameanza kuwasili kwenye mkutano wa Zanu PF, ambapo watajadili ikiwa watamtimua chamani Mugabe.

Kitengo cha vijana wa chama ambacho awali kilkuwa mtiifu kwake Mugabe sasa kimemgeuka.
Nao makamanda wa jeshi wanatarajiwa kukutana na Mugabe baadaye leo.

Mkuu wa chama chenye nguvu cha wale waliopigania uhuru Chris Mutsvangwa, aliiambia Reuters kuwa Bw Mugabe anawea kuondolewa kutoka uongozi wa chama mke wake kupokonywa wadhifa wa mku wa kitengo ya wanawake.

Bw Mugabe amekuwa akizuiliwa nyumbani tangu jeshli litwae madaraka siku ya Jumatano.
Jeshi lilingilia kati baad ya Mugabe 93, kumfuta makamu wa rais Emmerson Mnangagwa.

Maelfu ya watu wakiwemo kutoka chama tawala na upinzani waliingia mitaani siku ya Jumamosi kushrehekea hatua ya jeshi na kumtaka Mugabe ang'atuke


Wanajeshi walidhibiti kituo kikuu cha matangazo cha serikali siku ya Jumatano.
Afisa mmoja wa jeshi jenerali Sibusiso Moyo, kisha akasoma taarifa kwenye televisheni akiihakikishia nchi kuwa Mugabe na familia yake walikuwa salama.

Jeshi linasema kuwa likuwa likiwalenga waalifu wanaomzunguka Mugabe na kukana kuwa hayo sio mapinduzi ya kijeshi.
Ijumaa Mugabe alionekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu aweke nchini ya kuzuizi cha nyumbani na jeshi, wakati alihudhuria sherehe za kufuza kwenye chuo cha Harare.

Hata hivyo Grace Mugabe hakuwa. Ilifikiriwa kuwa alikuwa ameondoka nchini humo lakini iliiibuka Alhamisi kuwa alikuwa nyumbani na Mugabe.


No comments:

Post a Comment