MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameipiga jeki Kampuni ya Msama Auction Mart inayojishughulisha na ufuatiliaji na ukamataji wezi wa kazi za wasanii kwa kuchoma CD feki.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar, Mkurugenzi wa Msama Auction Mart, Alex Msama alisema Makonda ameamua kuipiga jeki kampeni hiyo kutokana na matunda anayoyaona ya zoezi hilo kuendelea vizuri kwani amezunguka katika jiji lake hasa maeneo ya Kariakoo na kujionea biashara hiyo haramu ya kuchoma CD feki ikiwa imepungua na kuwaomba waendelee na zoezi hilo.
Alisema kutokana na kutiwa moyo na mkuu huyo wa mkoa, Kampuni ya Msama Auction Mart sasa imezidi kupata nguvu ya kuendelea na zoezi hilo popote pale, iwe mafichoni ama pembezoni mwa mji lazima wezi wa kazi za wasanii wakamatwe.
Stori zinazo husiana na ulizosoma
No comments:
Post a Comment