Tuesday, 21 November 2017

Bilioni tano zaokolewa

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) imeokoa zaidi ya shilingi Bilioni 5 ambazo zingetumika kusafirisha wagonjwa nje ya nchi kufuata matibabu.



Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya alipotembelea MOI na kukagua hali ya utoaji wa huduma, mazingira , miundombinu na kuwajulia hali wagonjwa pamoja na kukutana na menejimenti.

Dkt. Mpoki amesema kuwa fedha hizo zimeokolewa baada ya MOI kuanzisha huduma za kibingwa ambazo awali zilikua hazipatikani hapa nchini, hivyo kulazimu wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi hivyo kuongeza gharama.

Akizungumza na uongozi wa MOI, Dkt. Ulisubisya amepongeza kazi nzuri na kubwa inayofanywa ambayo imepelekea watanzania kupata huduma bora za kibingwa ambazo wangepaswa kuzifuata nje ya nchi.

Aidha, Dkt Ulisubisya amesema MOI imepunguza rufaa za kwenda nje ya nchi kwa asilimia 95% na asilimia 5% iliyobaki MOI inaweza kuimaliza kabisa na kusiwepo na mgonjwa wa kwenda nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment