Monday, 29 January 2018

Ndoa zilizofungishwa bila leseni kubatilishwa


Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini nchini RITA, imesema, ndoa zote zilizofungwa bila kuzingatia sheria ya ndoa ikiwemo viongozi wa dini waliofungisha ndoa hizo kutokuwa na Leseni ya kufungisha ndoa huenda zikabatilishwa.

Afisa Usajili Msaidizi wa RITA Jane Barongo, amefafanua kuwa ndoa hizo zitabatilishwa tu endapo itabainika viongozi waliofungisha ndoa hizo hawakuwa na Leseni ya kufungisha ndoa kutoka serikalini.

Barongo ameongeza kuwa kiongozi wa dini atakayebainika kufungisha ndoa bila kuwa na Leseni ya serikali anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria ya ndoa ambayo imeipa Rita mamlaka ya kisheria, kusajili ndoa zote zilizofungwa kihalali.

Kwa upande mwingine amesema tayari serikali imewakumbusha viongozi wote wa dini kuhakikisha wanakamilisha taratibu za kukata Leseni ya kufungisha ndoa kabla ya kufungisha ndoa yoyote nchini.

No comments:

Post a Comment