Tuesday, 30 January 2018

Rostand aiokoa Yanga na aibu kombe la FA


Kipa Youthe Rostand ameibuka shujaa baada ya kupangua penalti 3 na kuiwezesha Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Ihefu ya Mbeya.

Yanga ilikuwa ikiivaa Ihefu katika mechi ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, leo.

Kipa huyo wa Cameroon amepangua mikwaju mitatu ya penalti wakati wa changamoto za mikwaju hiyo.

Al manusura Yanga ing’olewe baada ya Obrey Chirwa kukosa penalti, lakini kipa huyo Mcameroon akapangua penalti iliyofuata na kuifanya Yanga iendelee.

Yanga ililazimika kuingia kwenye changamoto hizo na timu hiyo ya daraja la pili baada ya kusawazisha katika dakika za majeruhi baada ya kuwa imefungwa bao.

Chirwa ndiye aliyesawazisha kwa mkwaju wa penalti huku Ihefu wakiwa wanaamini mechi ilikuwa imeisha.

No comments:

Post a Comment