Tuesday, 30 January 2018

Wachimbaji wanne wa mchanga wafariki Arusha



Watu wanne wamefariki dunia huku mmoja akijeruhiwa vibaya baada ya mawe kuporomoka na kuwafukia wachimbaji  watano ambao walikuwa wakichimba mchanga kwenye eneo la mlima CCM Kata ya Muriet, Arusha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC), Charles Mkumbo akiongea na www.eatv.tv amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kudai kuwa majeruhi amepelekwa katika hospitali ya Mount Meru huku hali yake ikiwa ni mbaya sana.

"Kuna eneo lipo huku Kata ya Muriet ambapo huwa wanachimba mchanga mkavu hivyo wakati wanaendelea na kuchimba kuna sehemu nyingine huwa haichimbwi sasa wanasayansi wanatuambia dunia huwa inazunguka hivyo kuna mpasuko ulikuwa umetokea kwenye eneo ambalo wala halichimbwi huo mchanga, hivyo hilo gema lilipopasuka likaangukia upande ambao watu wanachimba mchanga huo na kuwafukia watu watano, wanne walipoteza maisha pale pale huku mmoja akiwa amejeruhiwa vibaya na kupelekwa hospitali ya Mount Meru kupatiwa matibabu" alisema Mkumbo.

EATV

No comments:

Post a Comment