Saturday, 3 February 2018

Singida United yaipiga Mwadui FC 3-2

Singida United wameshinda kwa mabao 3-2 dhidi ya Mwadui FC katika mechi kali ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.

Wageni Mwadui walitangulia kwa mabao mawili kabla ya Singida kusawazisha na kufunga la ushindi.

Mechi hiyo ilikuwa ni ya kushambuliana kwa zamu ingawa Singida United walifanya mashambulizi mengi zaidi mwishoni.

Shuja wa Singida United alikuwa Kenny Ally Mwambungu ambaye alifunga bao kwa shuti kali ndani ya dakika 3 za nyongeza baada ya mwamuzi kuongeza dakika 5.


Shuti kali alilopiga na kumshinda kipa Massawe wa Mwadui ni baada ya kupokea pasi nzuri ya Mudathiri Yahya.

Mabao mawili ya Singida United ikisawazisha, yalifungwa na Salum Chuku na Deus Kaseke aliyeng'ara katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment