Saturday, 3 February 2018

Mume aliyeweka pilipili kwenye nguo ya mkewe aadhibiwa


Mahakama moja wilayani Lira nchini Uganda imemuhukumu mwanamume kifungo cha siku 40 kutumikia jamii baada ya kupatikana na hatia ya kupaka pilipili nguo ya ndani (chupi) ya mkewe.

Akisoma hukumu, hakimu Hilary Kiwanuka alisema ushahidi uliotolewa mahakamani umejitosheleza pasipo kuacha shaka kwamba mtuhumiwa Moses Okello alitenda kosa hilo.

Okello, mkazi wa Kijiji cha Barmola, Kaunti Ndogo ya Bala wilayani Kole atatakiwa kufanya kazi za kijamii katika kipindi cha siku 40 kutokana na kosa hilo.

Mahakama ilielezwa Januari 20,2018, Okello alipaka pilipili kwenye nguo hiyo na baadaye alimshauri mkewe aivae.

“Alinishauri kuivaa siku hiyo, nilipoivaa nilianza kuwashwa na mwasho huo haukuisha hata nilipooga,” mwanamke huyo aliieleza Mahakama.

Haikuelezwa ni kwa nini Okello aliamua kufanya kitendo hicho kwa mkewe ingawa baadaye alidai alikuwa akimtania.

No comments:

Post a Comment