Meli ya mizigo imetipotiwa kupinduka na kusababisha kifo cha mtu mmoja China.
Kwa mujibu wa habari,wafanyakazi sita wa meli hiyo walianguka katika maji baada ya ajali hiyo kutokea.
Shirika la Shingua limetangaza kuwa ajali hiyo imetokea katika mto wa Yangtze katika mji wa Huanggang.
Meli hiyo ilikuwa ina wafanyakazi sita,mmoja wao akiwa amefariki huku watano wengine hawajulikani walipo mpaka sasa.
Timu ya uokoaji iliweza kumtoa mmoja wao katika maji lakini haikuwezekana kuyanusuru maisha yake.
Juhudi za kuwatafuta wafanyakazi watano waliobaki zinaendelea.
No comments:
Post a Comment