Monday, 29 January 2018

Lita 85 za Gongo zakamatwa Manyara


Jeshi la Polisi mkoani Manyara limesema limekamata mitambo ya kutengenezea pombe haramu ya gongo pamoja na lita 85 za pombe hiyo, ambayo ni kinyume na sheria za nchi.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga, amesema vifaa hivyo pamoja na pombe imekamatwa kutokana na operesheni maalum inayoendeshwa na jeshi hilo.

“Mkoa wetu wa Manyara umeendelea na misako mbali mbali ambapo tumekamata mitambo ya gongo pamoja na gongo huko mbulu, kijiji cha hydom Manyara, walimkata mtu mmoja Moshi Bula mwenye miaka 55, akiwa na mitambo minne ya kutengenezea mitambo ya gongo, hivi sasa yupo mahabusu na taratibu zikikamilika atafikishwa mahakamani,”, amesema Kamanda Senga.

Kamanda Senga ameendelea kuelezea kwamba...Sambamba na hilo tumekamata lita 65 za pombe haramu ya moshi pamoja na watu watatu wanaohusika na pombe hiyo, ambao ni Neema Doto Matayo, mwenye miaka 21, Lawawa Sakara na Patrima Bula na wote watafikishwa mahakani”.

Licha ya hayo Kamanda wa Senga amesema pia wamemkatama mwanamke mmoja akiwa na lita 20 za gongo, na kufanya idadi ya lita 85 za pombe hiyo haramu.

No comments:

Post a Comment