Gwiji wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina Diego Maradona amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutoswa visa ya kwenda nchini Marekani kutokana na matamshi aliyoyatoa dhidi ya raisi Donald Trump.
Maradona ana kesi na aliyekuwa mke wake aitwaye Claudia Villafane na alipaswa kwenda hadi Miami kusikiliza kesi hiyo lakini maofisa wa uhamiaji walimuwekea ngumu kupata visa ya kwenda nchini humo.
Maradona siku zilizopita alisikika katika moja ya interview zake akimuita raisi Donald Trump “chirolita” jina ambalo kwa Waargentina linatumika kwa watu ambao ni vibaraka wa watu wengine.
Baada ya Maradona kushindwa kwenda nchini Marekani sasa itabidi wakili wake akwee pipa kuelekea Miami kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo huku ikiwa bado haijafahamika kwamba inawezekana ukawa mwisho wa Maradina kwenda Marekani ama laa.
Huu ni muendelezo wa matukio na visa vya Maradona nje ya uwanja, kwani miaka ya karibuni amekuwa akiyafanya na kwa sasa mchezaji huyo yuko falme za kiarabu kama kocha wa klabu ya Al Fujairah.
No comments:
Post a Comment