Friday, 2 February 2018

DC Matiro akabidhi hundi za mikopo mil 25 vikundi vya vijana na wanawake

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amekabidhi hundi za mikopo shilingi milioni 25 kwa vikundi vitatu vya vijana na kimoja cha wanawake zilizotolewa na halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Fedha hizo zinatokana na asilimia 10 ya makusanyo kutoka katika vyanzo vya mapato ndani ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Julai 2o17 hadi Disemba 2017.

Vikundi vilivyokabidhiwa hundi ni kikundi cha Wanawake na Maendeleo kilichopo katika kijiji cha Ishololo kata ya Usule na vikundi vya vijana vya Umoja wa bodaboda, Jikwamue, Shukrani Group vilivyopo katika kijiji cha Didia kata ya Didia katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Akikabidhi hundi hizo kwa wawakilishi wa vikundi hivyo leo Ijumaa Februari katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo,Matiro aliwataka walionufaika na mikopo hiyo watumie pesa walizopata kwa malengo yaliyokusudiwa.

“Kila mtu aliyepata pesa akafanye kile alichokusudia kufanya, serikali inajitahidi kuwawezesha kwa kuwapatia mikopo ili mjikwamue kiuchumi,naomba mfanye kazi kwa bidii ili kubadilisha maisha yenu”,alieleza Matiro.DC

No comments:

Post a Comment