Saturday, 3 February 2018

Watatu wafariki kutokana na baridi kali

Watu watatu waripotiwa kufariki  nchini Uswidi kutokana na baridi kali Kaskazini mwa Uswidi.

Baridi kali katika eneo hilo la Kaskzini mwa Uswidi ilifuatiwa na theluji kali ambapo nyuzi joto ilikuwa 20 chini ya sifuri.

Uongozi wa eneo la Vesternorrland nchini Uswidi umefahamisha kuwa bariki kali katika eneo hilo imesababisha vifo vya watu watatu.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini Uswidi imetoa tahadhari kwa raia  kutokana na kiwango kşkubwa cha theluji ambacho kinatarajiwa katika za usoni.

No comments:

Post a Comment