Tuesday, 30 January 2018

Sumaye, Sosopi wamnadi Mwalimu leo


Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema, Salum Mwalimu amewaomba wananchi wa Kinondoni kumchagua awahi mkutano wa Bunge la bajeti utakaoanza Aprili, mwaka huu ili awasilishe hoja za maendeleo.

Amesema hayo leo Jumanne Januari 30,2018 alipohutubia mkutano wa kampeni Magomeni Morocco wilayani Kinondoni.

“Msifanye makosa siku ya uchaguzi, waacheni hao wengine wapige kelele. Mkimchagua mbunge dhaifu mtaendelea kubaki dhaifu katika kipindi cha miaka mitano,” amesema Mwalimu.

Amesema yeye ni mfuatiliaji  wa masuala ya  fidia na atakapokuwa mbunge, wananchi wa Kinondoni hawatapata shida kwa kuwa anajua kunusa zilipo fedha kwa ajili ya maendeleo.

Mkutano huo pia ulihutubiwa na viongozi mbalimbali wa Chadema, akiwemo mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Pwani na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye; mwenyekiti wa Baraza la Vijana la chama hicho (Bavicha), Patrick ole Sosopi na mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea.

No comments:

Post a Comment