Saturday, 3 February 2018

Majeruhi wailiza Azam FC


Kuelekea mchezo wa marudiano raundi ya pili ya ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC, klabu ya soka ya Azam FC imesema inakabiliwa na majeruhi wengi akiwemo nahodha wa kikosi hicho Himid Mao.

Akiongelea mchezo huo msemaji wa timu hiyo Jaffary Idd amesema pamoja na majeruhi hao lakini timu ina kikosi kipana hivyo mwalimu Aristica Cioaba amewaandaa wengine kupambana kwaajili ya kupata alama tatu.

Wachezaji wengine ambao ni majeruhi ndani ya kikosi hicho ni Waziri Junior, Joseph Kimwaga na Joseph Mahundi, wakati Abubakar Salum 'Sure Boy' anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo dhidi ya Yanga.

Azam FC inaingia katika mchezo wa leo utakaopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex ikiwa katika nafasi ya pili na alama 30, nyuma ya Simba yenye alama 35 kileleni. Ndanda inashika nafasi ya 8 ikiwa na alama 16.

No comments:

Post a Comment