Katika gazeti rasmi, imeandikwa kuwa "Baraza la Mawaziri lilipitisha Azimio No. 6056 la Januari 15, ambalo linasema kusimamishwe kwa mahusiano ya kidiplomasia na Korea ya Kaskazini".
Kwa mujibu wa habari,balozi wa Korea Kaskazini nchini Jordan atasimamishwa kazi.
Afisa Mkuu wa Jordan amesema kwamba uamuzi wa kukata mahusiano na Korea Kaskazini ni kutokana na maslahi ya serikali.
Umoja wa Mataifa umeiwekea Korea Kaskazini vikwazo kutokana na majaribio yake ya makombora ya nyuklia.
No comments:
Post a Comment