Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amemtakia furaha ya kuzaliwa mwanawe wa kiume Zuca baada ya kutimiza miaka 18 huku akiposti picha ya utotoni inayomuonyesha wakiwa pamoja katika kiboti.
Meneja huyo wa Man United ameposti picha hiyo huku akiandika “Furaha ya kuzaliwa Zuca sasa unamiaka 18 huitaji uwepo wangu tena kwenda kuogelea pamoja katika kiboti,”ameandika Mourinho kupitia mtandao wake.
Picha hiyo inamuonyesha Mourinho akiendesha kiboti hicho huku akiwa na Zuca.
Mwaka jana Mourinho aliwahi kumtakia furaha ya kuzaliwa mwanawe kwa kuposti ujumbe unao fanana na huo.
Zuca anacheza nafasi ya goli kipa katika academy ya Fulham akiwa amesaini kandarasi ya miaka miwili akiwa na umri wa miaka 16.
Hapo hawali Zuca alikuwa akiitumikia klabu ya Chelsea na Real Madrid wakati timu hizo zikitumikiwa na baba yake.
No comments:
Post a Comment