Klabu ya soka ya West Ham imemfuta kazi mkurugenzi wa uajiri wa wachezaji wa timu hiyo Tony Henry kutokana na kauli yake ya kuwabagua wachezaji kutoka Afrika.
Tony Henry hivi karibuni alinukuliwa akisema kuwa timu hiyo haiwezi kusaini wachezaji kutoka Afrika kutokana na wachezaji hao kutowajibika vizuri kwenye baadhi ya majukumu yao.
Taarifa ya klabu hiyo imeeleza kuwa maneno ya Tony Henry sio msimamo wa klabu kwasababu timu haiamini katika ubaguzi wa aina yoyote ndio mana imeamua kumfuta kazi Henry ili hatua zingine zichukuliwe.
West Ham ina wachezaji sita kwenye kikosi cha kwanza wenye asili ya Kiafrika ambao ni Cheikhou Kouyate, Pedro Obiang, Joao Mario, Angelo Ogbonna, Arthur Masuaku na Edimilson Fernandes.
Wengine ni mshambuliaji wa Senegal Diafra Sakho ambaye ameondoka kwenye dirisha dogo la Januari akajiunga na Rennes ya Ufaransa huku Andre Ayew wa wa Ghana akielekea Swansea.
No comments:
Post a Comment