Thursday 30 November 2017

Sam Allardyce ndio kocha mpya wa Everton



KOCHA mpya wa Everton, Sam Allardyce amesema kwamba wachezaji wamepoteza hali ya kujiamini na ameiagiza klabu kusajili mbadala wa Romelu Lukaku.

Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 63 leo amethibitishwa kuwa kocha mpya wa Everton na mwanahisa mkuu wa klabu, Farhad Moshiri amemtaja kama kiongozi wa nguvu' na amemtabiria ataifikisha timu panapohitajika.'

Lakini kuelekea utambulisho rasmi, Allardyce ameandika kwenye safu ya Paddy Power kutoa maoni yake juu ya kufanya vibaya kwa timu hiyo msimu huu.

The Toffees wanashika nafasi ya 17 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England pointi mbili tu kutoka nafasi za kuteremka daraja, licha ya kutumia Pauni Milioni 140 kufanya usajili mzuri kwa lengo la kumaliza ndani ya sita bora.

Allardyce amekiri klabu ipo katika nafasi mbaya kwa sasa na amesema jukumu lake la kwanza litakuwa ni kurejesha hali yab kujiamini.

Allardyce mwenye umri wa miaka 63, amerejea kutoka mapumzikoni leo na kukutana na Moshiri kusaini mkataba wa kufundisha Everton.

Atakuwa anapokea mshahara Pauni Milioni 6 kwa mwaka katika miezi 18 ya mkataba wake na ataanza rasmi kazi jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Huddersfield Town Uwanja wa Goodison Park.

Lakini leo atakwenda kushuhudia mchezo dhidi ya West Ham.

No comments:

Post a Comment