Msanii wa Bongo Flava, Abdu Kiba amesema hawezi kuomba sapoti kutoka team Diamond ingawa hana tatizo nao.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Single’ aliyomshirikisha Alikiba ameiambia Planet Bongo, East Africa Radio kuwa kufanya hivyo atakuwa ameenda kinyume na label yake ya sasa ‘King’s Music’.
“Sidhani, siwezi kufanya hicho kitu, mimi ni Abdu Kiba kama Abdu Kiba ila siwezi kuanza kufanya hivyo kwa sababu kwanza nitakuwa nimewakwaza mashabiki wangu, cha pili nitakuwa nimeruka miiko ya label yangu” amesema.
Alipoulizwa iwapo team zina umuhimu katika muziki, ajilibu; “kitu kama hicho lazima kiwepo kwa sababu ili aweze kupatikana bora ni lazima awepo mpinzani kuweza kumpata bora, so kitu kama hicho kinatakiwa kiwepo lakini siyo kiwe too much”.
“Still bado naona kawaida, nahitaji kuona mapambano bado yanendelea ili tuweze kujua nani bora” alisisitiza.
No comments:
Post a Comment