Friday, 1 December 2017

Manula hana wasiwasi wa kuifunga Libya



Mlinda mlango wa Timu ya Taifa ya Tanzania Bara “Kilimanjaro Stars” Aishi Salum Manula amesema kutokuwajua vizuri wapinzani wao Timu ya Taifa ya Libya hakutakuwa chanzo cha kutokufanya vizuri katika mchezo wa awali wa michuano ya CECAFA

Manula amesema mara nyingi Kocha hutoa mbinu kwa wachezaji wake kutokana na kuijua japo sio kwa undani timu wanayokutana nayo hivyo wanaamini Kocha anaifahamu Libya na mbinu walizofundishwa zitawasaidia kuweza kupambana nao ili kuibuka na ushindi katika mchezo huo na inayofuata.

"Timu ya Libya siijui kwa hivyo lakini nadhani kwa vile ambavyo Mwalimu amatufundisha na mbinu ambazo ametupa kuelekea katika mchezo wetu wa kwanza nadhani tutafanikiwa kwani nadhani yeye ameweza kuifuatilia vizuri zaidi na kwaundani na kujua kwamba Libya ipo vipi ili atupatie mbinu gani na tuweze kuushinda mchezo huo, " amesema.

Aishi ameongeza kwa kuwataka watanzania kuendelea kuwapa sapoti ikiwa ni pamoja na kuwaanini kwani wao wakiwa ni wachezaji wanajua dhamana ya watanzania waliyoibeba.

Kikosi cha Kilimanjaro Stars kilichoondoka hapo jana kimeshawasili nchini Kenya na leo kimeendelea na mazoezi kwaajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Libya utakaopigwa siku ya Jumapili nchini humo

No comments:

Post a Comment