Zaidi ya raia 100 kutoka Ghana walikuwa wanazuiliwa nchini Libya, wamerudi makwao baada ya Serikali kupata ndege ya kuwapeleka nyumbani.
Walienda Libya wakiwa na matumaini ya kufika Ulaya lakini wakasalia kuwekwa katika vituo vya kufungwa kama wahamiaji haramu.
Kurudi kwao kulifuatia hamaki iliyotanda dunia nzima baada ya kanda ya video kuibuka iliyoonyesha Waafrika wakiuzwa kama watumwa nchini Libya.
Viongozi kutoka Afrika na Ulaya wamekuwa wakijadiliana suala hilo katika mkutano nchini Ivory Coast na wameandaa mpango wa pamoja ili kujaribu kutatua shida hiyo
No comments:
Post a Comment