Mtanzania Jonesia Rukyaa Kabakama ameteuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), kuchezesha fainali zijazo za Kombe la Dunia kwa wanawake (Algarve Cup) zitakazofanyika nchini Ureno, mwezi Februari, mwakani.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka TFF, Jonesia, ambaye ni mwanamke, ameteuliwa kupuliza filimbi katika fainali hizo ambazo hukutanisha timu mahiri zilizofanya vema katika michuano ya kila Bara.
Lakini kabla ya kwenda Ureno, Jonesia anatarajiwa kushiriki semina maalumu iliyoandaliwa na FIFA. Semina hiyo itafanyika Doha, Qatar kuanzia Februari 12- 16, mwakani.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limempongeza Mwamuzi Jonesia kwa kuteuliwa na FIFA kuchezesha fainali za Kombe la Dunia na kuhudhuria semina hiyo muhimu kwa maendeleo ya mpira wa miguu.
Waamuzi wengine walioteliwa kutoka Afrika Lidya Abebe wa Ethiopia, Glady Lengwe wa Zambia na Salima Mukansanga wa Rwanda
No comments:
Post a Comment