Saturday, 2 December 2017

Mark Hughes aponda kiwango cha Atkinson



Meneja wa klabu ya Stoke City Mark Hughes amesema Martin Atkinson hafai kutumiwa kama mwamuzi mechi za Ligi ya Premia msimu huu baada ya kufanya "kosa kubwa" mechi za katikati ya wiki.

Atkinson alimpa mlindalango wa Liverpool Simon Mignolet kandi ya manjano pekee kwa kumwangusha mshambuliaji wa Stoke Mame Diouf, akiwa ndiye mchezaji wa mwisho Jumatano.
Stoke walikuwa 1-0 chini wakati huo.

Walishindwa 3-0 mwishowe na Hughes alisema "kila mtu alijua" hiyo ilifaa kuwa kadi nyekundu.
"Sioni ni kwa nini anafaa kusimamia mechi wikendi hii," aliongeza.

"Hisia zangu ni sawa na za kila mtu: waamuzi ambao walitazama tena kisa hicho na kila mtu uwanjani, kando na mmoja pekee.

"Kuna maamuzi yanayoniuma sana mimi kama meneja - na mameneja wengine.

"Sababu ya hiyo kutokuwa (kadi nyekundu) mimi sijui. Ulikuwa uamuzi rahisi sana kwangu lakini haukufanywa. Hilo lilitunyima fursa ya kujipatia nafuu. Nimekasirishwa sana na hilo."

Atkinson atasimamia mechi ya Watford nyumbani dhidi ya Tottenham Ligi ya Premia Jumamosi.

Aprili 2016, Bodi ya Kimataifa vya Soka (IFAB) iliidhinisha kubadilishwa kwa kanuni za soka na kuondoa hitaji la kadi nyekundu moja kwa moja kwa mchezaji anayefanya kosa linalomnyima mpinzani nafasi wazi ya kufunga bao.



No comments:

Post a Comment