Friday, 1 December 2017

Jay-Z akiri kuchepuka kwenye ndoa yake



Jay-Z na mke wake Beyonce

Mwanamuziki wa rap Jay -Z amekiri kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengine akiwa bado kwenye ndoa yake na Beyonce.

Amekiri hilo kwa mara ya kwanza alipokuwa akihojiwa kuhusiana na maisha yao na jarida moja.

Aliambia jarida la Style la gazeti la The New York Times kwamba alijiwekea vizuizi kutokana na matatizo aliyokumbana nayo alipokuwa mtoto, jambo ambalo lilimfanya kujifungia na kuwa uzinifu.

''Kitu kigumu ni kuona uso wa mtu uliojaa huzuni uliosababishwa na wewe, alisema Jay -Z."

Wanandoa hao walikuwa wamedokeza kuhusu Jay-Z kutokuwa mwaaminifu kwenye nyimbo zao.

Mwanamuziki huyo amesema kwamba wangetalikiana lakini alipata ushauri nasaha ili kumsaidia kukabiliana na matatizo yake ya hapo awali.

Kama unavyofahamu, watu wengi hutalikiana, na visa vya kutalikiana ni takriban asilimia 50 mambo kama haya yanapotokea.

Mwaka wa 2013, kulikuwa na uvumi kwamba mwanamuziki huyo wa nyimbo za rap hakuwa mwaminifu kwa mke wake na ilichochewa na kitambulisha mada cha #elevatorgate pale Solange Knowles alipomshambulia Jay -Z, huku Beyonce akionekana kunyamaza kimya.

Albamu ya hivi majuzi ya Jay -Z ya 4:44 ilizungumzia yeye mwaminifu.

Aliandika :''Naomba radhi / kwa kutoka nje ya ndoa/aliyemfanya mtoto wangu kuzaliwa kupitia kwa macho ya mamake.''

Mwaka mmoja kabla ya albamu hiyo ya 4:44 kuzinduliwa , Beyonce aliimba kuhusu ''Becky with good hair (Becky mwenye nywele nzuri)'' kwenye albamu yake ya Lemonade.

''Yeye hunihitaji wakati sipatikani, heri ampigie Becky ambaye ana nywele ndefu.''

Jay -Z na Beyonce walikuwa wamepanga kutoa albamu ya pamoja badala yake wakaishia kufanya nyimbo kila mmoja yake.

''Tunatumia sanaa kujiliwaza. Tulianza kutunga nyimbo zetu pamoja. Na nyimbo alizokuwa akibuni wakati huo zilikuwa mbele sana.

''Kwa hivyo albamu yake ilizinduliwa kinyume na matarajio ya kuwa albamu hiyo ingekuwa imewashirikisha wanandoa hao.

Pia Jay-Z hakuzungumzia kuhusiana na ndoa yake pekee, pia alizungumzia kuhusiana na mahusiano yake na Kanye West.

''Nilizungumza na Kanye wakati mmoja, kumwambia yeye ni kama kakangu. Nampenda Kanye. Kwa kweli. Ni mahusiano tata kati yetu.

Alikubali kwamba hawajakuwa na uhusiano rahisi.

Kanye West aliripotiwa kuacha kazi katika kituo cha umiliki wa huduma ya kusikiliza muziki ya moja kwa moja ya mwanamuziki ya Jay Z, Tidal ,kuhusiana na mzozo wa kifedha.

''Niko na uhakika anahisi nimemfanyia mambo kadhaa pia yeye.

''Natumai tutakapofika umri wa miaka 89, tutaangazia haya baada ya miezi sita au wakati wowote na kutafurahia haya yote.''

No comments:

Post a Comment