Saturday, 2 December 2017

Chege afananisha ustaa na Jela



Msanii wa Bongo Flava, Chege amesema msanii kuwa staa ni sawa na jela.

Muimbaji huyo wa ngoma ‘Run Town’ ameiambia 5 Selekt ya EATV kuwa kwa wale wasiofahamu wanaweza kuchukulia hilo kawaida lakini ukishakuwa staa ndio utagundua hilo.

“Mtu unapokuwa unaangaika kutafuta ustaa lakini ustaa ni jela moja mbaya sana kwa mtu ambaye hajawahi kupitia hiyo kitu anaweza akaona huyu anaongea tu lakini ukishakua pale kwenye ustaa ndio unajua majukumu ya ustaa yakoje” amesema.

Chege amepongeza kuwa hilo halijamsumbua kwani toka awali alikuwa kwenye mafunzo ya kuupokea ustaa na alikaa na mastaa kwa muda mrefu kabla hajawa staa.

“Siyo kukaa nao tu na kukutana masikani, no! nilikua ndani ya kundi ambalo lina staa namba moja Tanzania nzima kwa hiyo hadi nakuja kuwa staa ule ushamba wa ustaa siwezi kuwa nao tena” amesema Chege.

No comments:

Post a Comment