Muimbaji Diamond Platnumz wiki hii baada ya kuachia nyimbo mbili, Sikomi na Niache, aliahidi Ijumaa hii kuachia rasmi wimbo wake mpya uitwao ‘Waka’.
Meneja wa nyota huyo, Sallam SK amewaomba radhi mashabiki wa muimbaji huyo mwenye tuzo nyingi za kimataifa kwa madai kuna dharura imetokea hivyo atashindwa kuachia project hiyo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa muziki.
“Tunaomba msamaha wimbo wa ‘Waka’ ulitakuwa kutoka siku ya leo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu kwahiyo hautaweza kutoka leo lakini muda sio mrefu tutawajuza!! Sorry for any inconvenience,” aliandika meneja huyo.
Wadau wa mambo wamedai muimbaji huyo ameshindwa kuachia kazi hiyo mpya ili kuepusha kazi hiyo kushindanishwa na wimbo mpya wa msanii wa RockStar4000, Alikiba, ‘Maumivu Per Day’.
Hata hivyo mashabiki wa Diamond wameonyesha kuchukizwa vikali na uamuzi huo huku wengine wakiwa na maoni tofauti.
No comments:
Post a Comment