Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeziahirisha kesi za utakatishaji fedha inayowakabili Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na ile inayomkabili aliyekuwa Rais (TFF), Jamal Malinzi hadi December 14,2017 kwa sababu upelelezi haujakamilika.
Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Vitalis Peter amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa kesi ya Aveva na Malinzi zimeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa kesi hizo bado haujakamilika.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hizo hadi December 14/2017.
Kwa pamoja washtakiwa hao wanadaiwa kuwa walikula njama ya kughushi fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya March 15,2016 wakionesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa USD 300,000 kwa Evans Aveva wakati si kweli
No comments:
Post a Comment