Friday 1 December 2017

Apigwa faini kwa kuchora alama zake za barabarani


Apigwa faini kwa kuchora alama zake za barabarani China

Mtu mmoja raia wa China amepigwa faini baada ya kupatikana katika kamera akipaka rangi ishara mpya za barabarani ili kurahisisha safari yake kuwa rahisi.

Gazeti la Modern Express limeripoti kwamba mtu mwenye umri wa miaka 28 kwa jina Surnamed Cai, alipigwa faini ya Yuan 1000 mashariki mwa mji wa Lianyungang mkoani Jiangsu .

Alipatikana katika kamera mnamo mwezi Septemba 27 akiwa na mkebe wa rangi akipaka mistari mipya katika barabara ili kubadilisha mwelekeo wa trafiki na kuwaambia maafisa wa polisi kwamba alichukua hatua hiyo ili kupunguza tatizo la milolongo mirefu ya magari swala ambalo limekuwa likimchelewesha kila siku anapoelekea kazini.

Niliona kwamba barabara iliokuwa ikielekea moja kwa moja ilikuwa na mlolongo mrefu wa magari , huku barabara inayoelekea upande wa kushoto ikiwa na nafasi kubwa., aliambia maafisa wa polisi.

Nilidhani kubadilisha ishara hizo za babarabara kutarahisisha usafiri wangu kuelekea kazini.

Maafisa wa idara ya trafiki waliambia gazeti hilo kwamba walidhani kwamba tabia ya bwana Cai ilikuwa hatari na kwamba ingesababisha ajali.

Tayari wametuma wafanyikazi kuhadilisha ishara hizo za trafiki.

Hii sio mara ywa kwanza kwamba raia ametumia ujuzi wake wa sanaa kuweka ishara zao za barabara.

Mnamo mwezi Mei ,dereva mmoja mashariki mwa mji wa Zhejiang alipigwa faini baada ya kamera kumpata akichora eneo lake la kuegesha gari kwa kutumia chaki.


No comments:

Post a Comment