Kila timu sasa inahangaika kusaka wachezaji watakaowasaidia huku timu nyingi zikiwa zinawawinda wachezaji wa Yanga na Simba walio benchi au wasiopata nafasi ya kutosha ya kucheza.
Lakini Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amegoma kuwatoa wachezaji wake, Maka Edward ambaye ni kiungo na Yusuph Mhilu anayechezea nafasi ya ushambuliaji kwenda kwa mkopo katika timu ya Mbao FC kutokana na kuwahitaji katika kikosi chake.
Mbao FC iliwasilisha barua katika Klabu ya Yanga kuwaomba wachezaji hao kwa mkopo katika usajili wa dirisha dogo unaoendelea hivi sasa kwa lengo la kuongeza nguvu katika kikosi chao.
Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema walipokea barua kutoka Mbao ya kuwataka wachezaji wao Mhilu na Maka, lakini kocha Lwandamina amekataa kuwatoa.
No comments:
Post a Comment