Thursday, 30 November 2017

Abdu Kiba: Alikiba amenifanya chambo


Msanii Abdu Kiba ambaye ni mdogo wa Alikiba, amesema kitendo cha yeye kuachia kazi mpya badala ya wasanii wengine wapya waliopo kwenye lebo ya Kings Music iliyo chini ya kaka yake Alikiba ni kama chambo na sio kupendelewa kama wengi wanavyohisi.

Abdu Kiba ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba lebo iliamua kuanza kumtoa yeye ili kuangalia upepo utaendaje, kwani alikaa kimya sana kwenye game licha ya kuwa tayari ana mashabiki wake.
“Nimeanza mimi kutokana na ukimya wa muda mrefu, wasanii wapya wapo lakini isingekuwa vyema kukurupuka kuwaleta, mimi nimetumiwa kama chambo kwamba tuwalete kuangalia na mapokezi yatakuwaje, sio chambo kama nimetupwa”, amesema Abdu Kiba.
Hivi sasa msanii huyo ameachia wimbo wake mpya aliomshirikisha Alikiba unaoitwa 'Single', ambao ni kazi yake yake ya kwanza chini ya lebo ya Kings Music ambayo inamilikiwa na kaka yake Alikiba,


No comments:

Post a Comment