Wakati wananchi wa Liberia wakiendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi wa duru ya pili ya urais uliofanyika Desemba 26,2017 Rais anayemaliza muda wake Ellen Johnson Sirleaf ametangaza timu ya wataalamu watakaofanikisha mchakato wa kukabidhi madaraka.
Ikijulikana “Timu ya pamoja ya kukabidhi madaraka ya Rais” ndiyo yenye jukumu la kuratibu na kufanikisha hatua zote za ubadilishanaji madaraka kutoka yule anayemaliza muda wake kwenda kwa Rais ajaye.
Kulingana na waraka wa Rais, timu hiyo itaongozwa na marais wawili, anayemaliza muda wake na yule anayesubiri kuingia madarakani.
Iwapo wawili hao watakosekana waziri wa masuala ya nchi ndiye atakayeiongoza.
Pia, itakuwa na wajumbe wengine wanaofikia 50 ambao miongoni mwao ni mawaziri wanaohusika na Mambo ya Nchi na Masuala ya Rais; Sheria; Mambo ya Nje; Fedha na Mipango; Mambo ya Ndani; na Ulinzi wa Taifa
Rais Sirleaf anamaliza kipindi chake cha uongozi ambapo sasa anatarajiwa kumkabidhi madaraka mwanandinga wa zamani wa Taifa hilo na Klabu ya AC Milan, George Opong Weah ambaye amefanikiwa kumshinda mpinzani wake ambaye pia ni Makamu wa sasa wa Rais.
No comments:
Post a Comment