Habari rafiki na karibu sana katika safu hii ya makala za kilimo. Katika somo liliopita tuliangalia juu ya umuhimu wa kutumia mbegu bora na faida zake. Sasa leo tutaangalia kilimo cha matango kwa kutumia mbegu bora inayoitwa Hybrid Cucumber YETU F1 ambayo utaanza kuvuna baada ya siku 45-50 kutoka kupandwa kwake.
YETU F1 ni mbegu chotara ambayo ina umbo zuri na hupendwa sana na walaji. Kiasi cha mbegu 300g(Gramu 300) huweza kutosha ekari moja ambayo utainununua kwa shilingi laki tatu(300,000/=) za kitanzania.
UANDAAJI WA SHAMBA.
Chagua sehemu iliyo nzuri,na ukipata sehumu ya tifutifu iliyo changanyikana na mchanga itakuwa vizuri zaidi.
Pia ukipata sehemu yenye udongo mzito lakini usiwe una tuamisha maji.
Lima shamba na hakikisha umelisawazisha vizuri(yaani hallowing),baada yapo panga matuta yako.
KIASI CHA MBEGU.
Gramu 300 zenye kiasi ya YETU F1 kinatosha kupanda eneo la ekari moja(100m×40m).
Na hii aina ya mbegu 1g ina mbegu 30-40.
KUPANDA.
Kabla ya kupanda hakikisha una mbolea ya kupandia kama DAP ikichanganywa na Agrigrow starter yenye madini mengi ya phosphorus.
Panda mbegu kwa nafasi 150cm×45cm mbegu mbili mbili kila shimo.
Na hii mbegu huota baada ya siku tatu hadi tano,hivyo huchukua muda mfupi kuota.
Mara baada ya kuota tumia mbolea ya majani Agrigrow starter ambayo itaimarisha mizizi hivyo kurahisisha mmea kupata chakula kutoka kwenye udongo.
Huu mmea huchukua muda mfupi kukua hivyo hivyo mara baada ya kuota baada ya siku chache tumia mbolea ya yara mila winner kukuzia.
Pia yatakavyo anza kutambaa tumia mbolea ya majani Agrigrow vegetative hii itafanya yawe na matawi mengi hivyo kuongeza uzalishaji.
Maua yakianza kuonekana tuu,tumia mbolea ya majani Agrigrow flowering and fruiting,hii itasaidia maua kuto pukutika,pia itaboresha muonekano wa tunda,itafanya maua yawe mengi hivyo na kupatikana kwa matunda mengi.
Epuka kumwagilia maji jioni sana kwa kuwa unaweza ukasababisha magonjwa kama ya fangasi kwa mmea.
Pia epuka kupulizia dawa pale wadudu wa muhimu wawapo shambani(kama nyuki)kwani kutafanya kupunguza kwa mazao shambani.
DAWA ZA WADUDU
Ukiwa ni mkulima unayelima kitaalamu na unayetaka mafanikio kupitia kilimo yakufaa kuwa na dawa za wadudu zifuatazo.
1. Prosper 720EC yenye mchanganyiko wa sumu mbili(Profenofos 600g/L +Cypermethrin 120g/L),hii ni dawa ambayo ina ua wadudu katika wigo mpana(yaani ni broad spectrum). Na mchanganyiko wake ni 2mls au 2cc kwa maji lita 1.
2. Avirmec 1.8EC (Yenye sumu ya Abamectin) hii itauwa utitili shambani wa aina yote,na mchanganyiko wake ni 7mls kwa lita 20 za maji.
3. Dawa ya ukungu Agrilax 72WP,hasa kwa nyakati za baridi,hii ni dawa ambayo ina mchanganyiko ya wa sumu mbili yaani Mancozeb na Metalaxyl,ambayo mancozeb kwa ajiri ya kukinga(Preventive) na metalaxyl kwa kutibu(Curative).
Hivyo Agrilax hukinga na kutibu magonjwa yote yatokanayo na fangasi(yaani fungicide diseases).
MAVUNO.
Matango(YETU F1) huwa tayari baada ya siku 45-50 kutoka siku ya kupandwa.
Je utakuwa na miche mingapi kwa ekari moja? Kwa kawaida miche hufikia 11850.
Tuliangalia katika somo la matikiti kanuni ya kutafuta idadi ya miche yaani Plant population(I.e PP)
Plant population(PP) =(Area/Spacing) ×no of seeds per hole.
Kwa mfano:-Area(A)=1acre=4000m square.
-Spacing (SP)=150cm×45cm or 1.5m×0.45m.
-No of seeds to be sown per hole=2seeds.
-Required: Plant population (PP)
Then,from the formula;-
PP=((A/SP))×no of seeds per hole.
PP=((4000)÷(1.5×0.45))×2.
PP=(4000÷0.675)×2
PP=5925×2
PP=11,850Plants/acre
Therefore, there will be 11,850plants per acre.
Na haya matango kwa matunzo mazuri, huwa na matunda mengi sana ambayo yataweza kufikisha viroba 150 kwa makadilio ya chini kabisa ambayo utauza kwa sh 70,000/= kwa kiroba kimoja kwa bei ya chini kabisa.
Viroba 150@sh 70,000 ni sh 10,500,000/= kwa makadilio ya chini na hyo pesa ni kwa ekari moja tu.
Na hayo mapato ni kwa wale ambao wamepanda bila kuwekea nguzo(Non trellised)
Kwa wale watakao wekea nguzo(Trellised) wataweza kutumia eneo dogo na kupata mavuno mengi zaidi.
Na hivi ndivyo kilimo biashara kinavyotakiwa kuendeshwa(lima eneo dogo vuna mazao mengi)
Hebu tuangalie kwa wale watakao wekea nguzo(Trellised Cucumber)
Shamba la ekari moja(4000m square), Spacing =80cm×40cm(0,8m×0.4m),number of seeds per hole =1seed,Plant population (PP)=?
Therefore:-
PP=(Area/spacing) × no of seeds per hole.
PP=((4000)÷(0.8×0.4))×1.
PP=4000÷0.32
PP=12,500Plants/acre
- -Na kwa kuiwekekea nguzo(Trellised cucumber) huweza kuzaa matunda mengi zaidi kuliko bila kuyawekea nguzo.
- -Kwa kuyawekea nguzo mche mmoja huweza kuzaa matunda 15-30 kwa mche mmoja.
- -Tuchukulie kwa makadilio madogo kabisa mche mmoja umezaa matunda 15
1plant=15fruits
12500plants=x?
By crossing:
x=12500×15
x=187,500fruits/plants
- -Kwa hiyo utakuwa na jumla ya matunda 187,500 kwa ekari moja
- -Kwa kuuza kwa bei ndogo kabisa ya sh 50 kwa tunda moja,utakuwa na jumla ya fedha =187,500×50= Tzs 9,375,000/=
- -Kwa watakao uza kwa sh 100 kwa tunda moja,basi utakuwa na jumla ya pesa 187,500×100=18,750,000/=.
Kazi kwako kwa wewe mkulima unaye taka mafanikio,tumia mbegu bora (Hybrid seeds) zikuletee mafanikio.
No comments:
Post a Comment