Saturday 2 December 2017

Kombe la Shirikisho kuanza kutimua vumbi Desemba 22




Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa sasa itasimama kwa takribani majuma mawili sababu kubwa ni kupisha Kombe la Chalenji la CECAFA michuano inayoratibiwa na Baraza la Soka kwa nchi za Afrika Mashariki (CECAFA).

Kutokana na michuano hiyo kuingilia ratiba, kwa mujibu wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Desemba 22, 23, 24 na 26, zitakuwa siku za mechi za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam yaani Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Mechi zitakazochezwa katika siku hizo zitafahamika Desemba 5, mwaka huu ambako imepangwa droo ya timu 64 zitakazocheza Raundi ya Tatu ya ASFC.

Timu 64 maana yake ni kuwa timu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara; timu 24 za Ligi Daraja la Kwanza na timu 24 ambazo zimefuzu kutoka hatua awali; ya kwanza na pili.

Baada ya michezo hiyo, ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom itaendelea tena kwa michezo ya raundi ya 12 itakayofanyika Desemba 29, 30 na 31 kabla ya ligi tena kusimama kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Michuano ya CECAFA itafikia ukomo Desemba 17, mwaka huu na Shirikisho

No comments:

Post a Comment