Thursday, 30 November 2017

Kombe la Cecafa Challenge kuonyeshwa live na Azam TV



KAMPUNI ya Azam Media, imeingia mkataba na Baraza la Vyama vya Soka Afika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa ajili ya kuonyesha mechi zote za michuano ya kombe la Chalenji, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 3 hadi 16 mwaka huu nchini Kenya, yakishirikisha jumla ya timu tisa.

Akizungumza na Wanahabari jana katika studio za Azam Tv, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Tido Mhando, alisema kuwa, baada ya kuafanya vizuri katika Ligi Kuu Bara na mashindano mbalimba ya Ukanda wa Afrika Mashariki, zikiwemo nchi za Uganda, Rwanda na Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, Azam TV sasa imeamua kupiga hatua zaidi na kuingia katika michuano mikubwa zaidi Afrika.

Alisema huo ni moja ya mipango ya Azam kwenye mikakati yao ya muda mrefu kuonyesha michuano mikubwa zaidi ya soka kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana (AFCON) wa umri chini ya miaka 17, itakayofanyika Tanzania mwaka 2019.

“Kwa upande wetu maandalizi yanaendelea vizuri na timu nzima ya utayarishaji na urushaji matangazo ya moja kwa moja (Mubashara) tayari ipo katika vituo vyote nchini Kenya ambavyo vitatumikwa kwa mashindano ya mwaka huu,” alisema Mhando.

Aliongeza kuwa, Azam Tv wamejipanga kwa ajili ya kutoka burudani nzuri kwa wapenzi wa soka wa Afrika Mashariki na Kati kwa kuhakikisha wanafikisha matangazo hayo kwa uborea wa hali ya juu.

Mhando alisema huo ni mwanzo tu kwao kwao tayari wameanza mazungumzo na CECAFA kwa ajili ya kutangaza mashindano ya Kagame Cup yanayoshirikisha klabu mbalimbali.

No comments:

Post a Comment